Fight night: huku Canelo Alvarez kule Kamaru Usman

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Jumamosi kuamkia jumapili hii (tar 6-7) ni siku kubwa kwa wapenzi wa combat sports duniani; upande wa boxing kutakuwa na pambano kubwa linalomuhusisha bingwa na no1 P4P anayejulikana kwa jina la Saul Alvarez almaarufu kama Canelo ambaye ni mmexico, pamoja na mmarekani Caleb Plant ambaye pia ni bingwa katika uzito wa Super middleweight, hivyo watakuwa wakiunify mikanda yao na atakayeibuka mshindi atakuwa 'Undisputed Super Middleweight World Champion'. Pambano hilo la PPV linatarajia kuteka nyoyo za wapenda masumbwi duniani kutokana na amshaamsha zilizoanzia kwenye press conference yao ya kwanza.

UFC: kwenye upande wa Martial Arts kutakuwa na mapambano matatu ya kukata na shoka (PPV) ambayo yatakuwa headlined na wakali wawili wa Welterweight; Kamaru Usman (Mnaijeria) ambaye ndio Champion, na Colby Covington (Mmarekani) kama challenger. Wawili hawa wamewahi kukutana mara moja, pambano lao la kwanza lilikuwa mwakajana ambapo Usman alifanikiwa kuutetea mkanda wake, japo ilikuwa ni vita kali hadi Round ya mwisho Usman alipofanikiwa kushinda kwa TKO. Usman kwa sasa ndio no1 P4P kwa upande wa UFC, hivyo anapewa nafasi kubwa kuutetea mkanda wake.

Karibuni kwa updates hadi siku ya mapambano haya..

canelo_20211104_181348_0.jpg
ufc_20211104_175852_0.jpg
 
Naona Canello ana record na experience yakutosha, hapo nampa nafasi kubwa ya ushindi.
Yes anapewa nafasi kubwa, ukizingatia sahivi inaaminika ndio yupo kwenye prime, amekuwa bora sana baada ya ile loss ya Floyd
 
Jaamaa unajua vitu vzr Sana kuanzia boxing mpaka ufc na naona umemuweka mwamba Deontay Wilder (Hiki ni chuma haswa).Nakuambia Mimi shabiki Sana wa Canelo Ila atakaliswa.UFC ni mnaija anashinda

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Thanks mkuu kwa credit; kwamba unampa ushindi Plant? , Inahitaji ujasiri kumtabiria loss Canelo huyu aliye kwenye kiwango bora kuliko wakati wowote vivyohivyo kwa Kamaru Usman. Mimi sitaki kujipa presha, washindi wangu ni Canelo na Kamaru japo matokeo yakiwa kinyume sitashangaa sana maana kwenye hii michezo UPSET sio jambo la ajabu
 
Jumamosi kuamkia jumapili hii (tar 6-7) ni siku kubwa kwa wapenzi wa combat sports duniani; upande wa boxing kutakuwa na pambano kubwa linalomuhusisha bingwa na no1 P4P anayejulikana kwa jina la Saul Alvarez almaarufu kama Canelo ambaye ni mmexico, pamoja na mmarekani Caleb Plant ambaye pia ni bingwa katika uzito wa Super middleweight, hivyo watakuwa wakiunify mikanda yao na atakayeibuka mshindi atakuwa 'Undisputed Super Middleweight World Champion'. Pambano hilo la PPV linatarajia kuteka nyoyo za wapenda masumbwi duniani kutokana na amshaamsha zilizoanzia kwenye press conference yao ya kwanza.

UFC: kwenye upande wa Martial Arts kutakuwa na mapambano matatu ya kukata na shoka (PPV) ambayo yatakuwa headlined na wakali wawili wa Welterweight; Kamaru Usman (Mnaijeria) ambaye ndio Champion, na Colby Covington (Mmarekani) kama challenger. Wawili hawa wamewahi kukutana mara moja, pambano lao la kwanza lilikuwa mwakajana ambapo Usman alifanikiwa kuutetea mkanda wake, japo ilikuwa ni vita kali hadi Round ya mwisho Usman alipofanikiwa kushinda kwa TKO. Usman kwa sasa ndio no1 P4P kwa upande wa UFC, hivyo anapewa nafasi kubwa kuutetea mkanda wake.

Karibuni kwa updates hadi siku ya mapambano haya....View attachment 1998607View attachment 1998608
huyu usman ni wamoto namwelewa sana
 
Sijui DSTv wataonyesha channel gani.....inanikera sana kukosaga haya matukio
 
Mwaka 2015 Caleb Plant alipata majanga makubwa kwenye familia yake baada ya kufiwa na binti yake mwenye umri wa miezi 19 kwa matatizo ya kiafya ambayo madaktari walishindwa kuyapatia ufumbuzi, miezi miwili baadaye alifiwa na mamayake mzazi aliyekuwa na matatizo ya akili baada ya kupigwa risasi na Polisi; hii ilikuja baada ya huyu mama mwenye matatizo ya akili kuonekana akitishia kuua watu na kisu alichokishika. Caleb Plant aliahidi kwa binti yake aliyefariki kushinda Mkanda wa dunia na kumletea kaburini alikolazwa kwa ajili ya kumuenzi, mwaka 2019 alifanikisha hiyo ahadi yake na kumpelekea mkanda kama inavyoonekana pichani. Je kesho atafanikiwa kutwaa mikanda yote 'undisputed' na kuendelea 'kumfurahisha' binti yake? Let's wait....
instaboxingpromoter_20211106_081718_0.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom