Tindikali
JF-Expert Member
- Mar 26, 2010
- 2,070
- 2,806
Kuna huu ujumbe mzito ulienda Zurich, Uswisi, kuiombea ZFF uanachama wa FIFA ukiongozwa na Naibu Waziri Kiongozi wa wakati huo Juma Shamhuna, Naibu Waziri wa Michezo Joel Bendera na wengineo kutoka TFF na ZFF.
FIFA iliporudisha majibu faili likafichwa, wakakaa kimya kirefu kumbe wamepigwa chini. Imefahamika Bungeni leo kwa taarifa ya Nape Nnauye, Waziri wa Michezo alipolazimika kujibu swali la Mbunge wa Zanzibar, Hafidh Tahir.
Sababu zilizotolewa: FIFA imesema, kwa mujibu wa ibara ya 10 ya katiba ya FIFA, ZFF haiwezi kupata uanachama kwa vile Zanzibar hapa duniani sio nchi!
Je, Muungano unawazuia Zanzibar kupata misaada ya FIFA kama ilivyokuwa kwa OIC na hivyo kushindwa kuwa "Singapore"?
NB: Nimeongezea video ya Bunge hapo juu kwa vile mchangiaji mmoja amenishambulia kwamba nimeandika uongo kwa umma.