Fifa yakanusha kumuinizisha okwi kucheza yanga

Fifa yakanusha kumuinizisha okwi kucheza yanga

SOKON 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Posts
1,134
Reaction score
331
shirikisho la soka la Dunia limekanusha kumuinizisha Emanueli Okwi kuchezea yanga kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya vipengele kwani haruhusiwi kichezea timu tatu ndani ya msimu mmoja.
Ila mwenye more details aliyesikia vizuri atujuze sababu nimekutia katikati habari iyo wakimalizia kuliongelea!

Source: Radio one
 
Mnahangaika na mchezaji mmoja. Watanzania bwana. Badala ya kujipanga na Mbeya city nyie mwamuota Okwi tu.
 
Acha wa mchezeshe!!! Maana maana Yanga wanafikiri FIFA na CAF zinaendeshwa kwa majungu kama TFF yetu hapa....
 
shirikisho la soka la Dunia limekanusha kumuinizisha Emanueli Okwi kuchezea yanga kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya vipengele kwani haruhusiwi kichezea timu tatu ndani ya msimu mmoja.
Ila mwenye more details aliyesikia vizuri atujuze sababu nimekutia katikati habari iyo wakimalizia kuliongelea!

Source: Radio one

Kama huna uhakika unaanzaje kupost tena kwa kuiita Breaking News..!
 
kama ni kweli nitaamii TFF vilaza wa kutafsiri
 
Walitaka FIFA iseme 'Mimi, Sep Blatter, Rais wa FIFA, kwa niaba ya FIFA ninamuidhinisha Rasmi Emmanuel Okwi.........'? Hii haikuwa kesi ulikuwa ni ufafanuzi. Yeyote anayetoa ufafanuzi hafikii kutoa hukumu kwa kumtia ama kumtoa mtu hatiani. Hutoa vigezo na wasifu wa kipi kifuatwe ili kulipatia ufafanuzi. Ilichosema FIFA kwa mujibu wa huyo aliyesema FIFA imekanusha, ni kwamba yenyewe haina tatizo na Okwi kuchezea Yanga iwapo taratibu za uhamisho wake zimetimizwa. Sasa mlidhani TFF irudi tena FIFA kutaka ufafanuzi wa taratibu zake (TFF) yenyewe za uhamisho?
 
Mimi nasema siku zote tanzania hakuna wachambuzi wa michezo wala wanaojua kufuatilia kitu na kujua ukweli wa mambo ila ushabiki tu umewajaa, barua ya Fifa inasema kesi bado mijitu inanyanyuka na kutangaza kesi imeisha, imeishaje eti okwi hahusiani na madai ya simba na alivunja mkataba sababu hakulipwa mshahara wa miezi mitatu, haingii akilini hata kidogo mazee jidanganyeni tu mtakuja kujuta siku ya maamuzi
 
Post basi hiyo barua tuisome wote kwa pamoja hapa JF, maake inavyoonekana kuna wenzetu walioiona original wakati wengi tunafuatilia kwenye magazeti.
 
...ina maana TFF nao wamekurupuka!!!!!! ila; inawezekana kwani karibia viongozi wote wa TFF ni Yanga, wanaweza kufanya hivyo ili kuinusuru timu yao inayokabiliwa na mechi za Klabu Bingwa..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom