FIFA kuondoa offiside na kubadili upigaji wa penati

nasikia jamaa kafurahi.
cropped_REU_2375861__2_.jpg
Nimeangalia hiyo picha nikakumbuka haka kamjamaa
afad4f3d67d0d8cc6ff51428a55ba9f1.jpg
 
Huyu jamaa atapunguza ladha ya mpira, itafika hatua mwisho wa msimu mchezaji ana magoli 300 na ladha itakua ni ndogo sana. Football iachwe ivo ivo except ilo suala la kupunguza adhabu nalo ni muhimu. Wakati mwengine mchezaji anakua hana alternative way na wakati mwengine mchezaji anafanya kwa bahati mbaya unakuta amepigwa red card
 
Yaani mtu ashike mpira kama ule wa Suarez halafu apewe kadi ya njano? Hapana kwakweli.
Ni kuiongezea machungu tim pinzani.
 
Sawa kabisa. Magoli yatakuwa 20. Hebu tujiulize, ni wakati gani mpirani ambao tukio hushangiliwa zaidi? Wanataka kuongeza idadi ya matukio ya kushangilia zaidi ili watazamaji wafurahie zaidi. Matukio hayo ni wakati goli likiingia. Badala ya kushangilia mara moja tu au kutoshangilia wanataka ushangilieara 20, raha kabisa.
Wewe siyo mshabiki wa soka, utakuwa mshabiki wa netball ww!
 
Yanatakiwa yapitishwe fasta kabla hatujakutana nao, na hivi mwenyekiti wao amevurugwa tutaivunja rekodi yetu tuliyoiweka kwa kandambili
Teh teh teh.
 
Kitu cha maana hap0 ni kupunguza adhabu ya handba na kuongeza sub.vingine vitaharibu ladha ya mchezo.
Mkuu mi naogopa hapo kwenye offside, kutazalisha magoli mengi na kuharibu kabisa ladha mchezo wenyewe
 
Kuondoa offside hii ina changamoto nyingi sana, kwa kawaida wakati offside inatumika wachezaji walikuwa wanacheza half moja karibu muda wote wa mchezo kuogopa kuotea, sasa kwa zile km 8-12 average coverage za mchezaji kukimbia zitaongezeka mara 2 na hii inaweza kusababisha wachezaji kuzimia au muda mwingi watakuwa wanatembea wakiwa na mpira uwanjani na sio kukimbia kama ilivyo kuwa radha ya kabumbu, hivyo option ni tatu
1.wapunguze muda wa mchezo sema dk 60
2. waongeze idadi ya wachezaji kufika 20 kwa timu moja au
3. wapunguze ukubwa wa uwanja labda iwe upana kwa urefu 40*60

kwa hizo option tatu kwangu itakuwa ni ujinga mkubwa katika ulimwengu wa soka, kwa maoni yangu offside ihesabike angalau mita 3 kutoka kwa beki wa mwisho na sio kama sasa yaani mkono tu ni offside
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom