FIFA: Argentina bado wababe, Tanzania washuka

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,795
28,447
_92001759_c8297b0d-656a-40af-9abb-9d1f3b9ed63b.jpg


Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, ambapo vinara wamesalia kuwa Argentina.

Wanafuatwa kwa karibu na mabingwa wa dunia Ujerumani, kisha Brazil wanashika nafasi ya tatu.

Ubelgiji imeshuka nafasi mbili hadi nambari nne.

Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.

Tanzania sasa inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wamo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107.

Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138.

Nchi ya juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32.

Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24.

Mataifa 10 bora duniani
1.Argentina

2.Ujerumani

3.Brazil

4.Ubelgiji

5.Colombia

6.Chile

7.Ufaransa

8.Ureno

9.Uruguay

10.Uhispania
Mataifa 10 bora Afrika
31 Ivory Coast

32 Senegal

35 Algeria

38 Tunisia

45 Ghana

46 Misri

49 DR Congo

58 Mali

59 Cameroon
 
England hawana chao tena kwenye soka.

Tanzania kichwa cha mwendawa****.

Congo DRC wanafanya kweli.
 
Sijui Argentina ni ya kwanza kwa sababu gani. Au Messi naye ni kigezo cha kufanya ranking...!
Halafu hawa FIFA wanatuonea Tz, hata Malawi watupite?
 
Hizo rank za FIFA mi huwa naona hazina validity (ukweli) yoyote utakuta timu nyingine haifanyi vema lakini inapanda kiwango. wazinguaji tu.
 
Huo ukinara wa Argentina unatokana na nini hasa?
Mkuu NN,
Ukinara una pimwa kwa njia ya points za ushindi wa mechi za kitaifa za FIFA.. hujumulishwa points kadri ya ushindi za mechi zenye uzito.... ARG wao wanaongoza michezo ya ligi na urafiki... pointi zao zipo juu zaidi !!
 
Back
Top Bottom