Fid Q vs Jo Makini

Nimekubalia analysis yako, angalia these names: Kurasa, Magazijuto, Salu T, Solo, JCB, JMo nk..hawa watu wako real, they know wat hiphop music means.

Hao mabwana wote ni "wakali", na kwasasa ni kama mafahali wawili wasiopikika, kila mtu anakitaka "kiti".
Tatizo lao kubwa wote wanaimba kitu wasichokiamini, matokeo yake ni hawana hadhi sana mbele ya wafuatiliaji wa "real hiphop"

Kwanza wote wanalegeza sana, hawakazi kama ilipokuwa pale mwanzo mfano, msikilize Fid Q wa kipindi kile yupo na "heartfull Dodgerz" ie (wakina mapacha, Big 4 the geez, spado J, J murder na Sqeezer) huwezi kumlinganisha na Fid wa saiv. Joh makini wa saiv huwezi kumlinganisha na Joh makini wakipindi kile cha "hawapendi", "hao" kipindi hicho anatolewa na Prof Ludigo.

Kuthibitisha hilo, Fid Q alimkana mwanae wa toka enzi za utoto "Kiraka Rado".... hili lilinithibitishia u-blazameni wa Fid kwa kiasi kikubwa sana,

Kwenye Track ya "hao" Joh Makini aliziponda sana Tuzo za kill, na baadae alikataa hata kushirikishwa kwenye hizo tuzo ila baadae kuthibitisha kuwa alikuwa hajui anachopigania na wala alikuwa hajui anapigana na nani akageuka kuwa mpiga debe wa hizo tuzo tena hadi kushiriki kwenye ule wimbo mbovu wa "kill all star 2010".

Hoja kuu ya utetezi marazote imekuwa eti wasanii wetu ni njaa, hiyo kweli! Lakini huwezi kujiita mwanaharakati wakati hujazijua changamoto za hizo harakati zako, kwahyo hapo ni bora anyejitambulisha kama yeye ni **** toka mwanzo na akabaki na ufala wake hivyohivyo, kuliko hawa wanafiki.

Wote (Fid na Joh) wanataka tuwatambue kama ma-legend wa hiphop ya bongo, wakati hawana mpango unaofahamika wa kuacha legacy yoyote. Wameingia kwenye game wamakuta "hiphop haiuzi" ndio msemo unaokandamiza kazi zao, na wao wamejiunga kwenye huo wimbo eti kwa kususia kutoa album au kuzisambaza wao wenyewe kitu ambacho hakijaonyesha ukombozi kwa wadogo zao,

sawa basi wao wameshindwa kuanzisha harakati hizo za kimapinduzi ya soko lakini je wametoa support gani kwa wanaofanya hizo harakati mfano wa Sugu (au hata Kala Pina aliwahi kujaribu), si Joh wa Fid waliowahi kuunga mkono hizo harakati za hao watu kwa wazi wazi, wanogopa watabaniwa na watakula wapi..... ndio jibu! Basi hamna mkali hapo ni waganga njaa tu kama "bongofleva" wengine.

Ok msije mkaniambia natoka nje ya mada, lakini ni bora tufafanue vitu kwa undani japo kidogo katika kuonye kitu bora zaidi kuliko kushabikia kishabiki kila kitu unacholetewa.

Kwa kurudi kwenye swali, umezungumzia ukali katika maeneo ya "style", "lyrics" na "ryhmes".
Kwa sababu hawa ni watu ambao wametokea kwenye upenzi wa ndani sana wa hiphop, hivyo vitu wote wanavyo japo Fid ana-added advantage sababu ni anasoma sana vitabu hivyo mara zote anaonekana kumzidi Joh.

Papo hapo Joh anakitu "elimu ya mtaa" ambayo ni kitu muhimu sana kwenye hiphop, ndio maana mistari ya Joh inagusa sana watu wa mtaa, pia binafsi Joh amekuwa ananikuna sana coz marazingine amekuwa sio muoga kuuchana mfumo husika anaoona haujakaa poa ie "wasomi bado watumwa kwa wanasiasa....."track ya karibu tena kwenye show za joh".

Lakini ili kuutendea haki huu mjadala nadhani tungeangalia pia wanavyomeet "5 mic" kama element kuu za hiphop, wote wanapwaya sababu kuna makosa mengi yanatokana na mfumo wetu wa kimuziki, hivyo nyimbo zao zinakosa element za "dj", "graffit" na "black dancing"

Mwisho nimalizie tu kuwa hawa majaa kwangu hamna mkali ni wa kawaida sana ukiingia kwenye content ya track zao, wanaimba vitu vyepesi sana, nadhani nimeathirika na kusikiliza watu kama wakina;
"Hashimu Dodo (Bongo psychological)", "Salu-T", "Kwanza unit (Zavara na wenzake)", "Magazijuto", "Himamu Abas (underground souls)" "Kurasa", "A-bass", "Solo thang"...... hii kwa bongo tu, sasa ukisikiliza watu wa mtoni kama "Gangstarr (Guru), Rakim, Jeru, Nas, Rza na Gza, Pharaoh, Roots, Blackstar, Canbus nk nk nk..."

kwa sasa kuna vijana wanoka kwa "Duke", One, Stereo, Mpita, Nick Mbishi.
Mtaa bado una azina kubwa sana, wanaosema hiphop ime/inakufa inabidi wajikaze sana!
 
all i knw ni kwamba Ngosha ndo mc mkali zaid ya joh..jaribu kuckiliza Neno ft lod iez ndo utakubaliana nami pili fid anasoma sana vitab tht's y anadrop consciouz za maana
 
wote mabitozi tu, ila Fid Q ana akili na yuko matured kifikra na kwa hoja
 
Hakuna kitu hapo, wote hao ni wanabees, hawako real kuanzia lyrics hadi mavazi yao, wanaACT kama kina jay z, 50 cent, ice cube na wengineo. Hivi huwa hawajiulizi hakuna wasanii wakubwa wa hip hop kwenye nchi za FRANCE, GERMAN, ENGLAND, SOUTH AFRICA, CANADA, RUSSIA na nyinginezo? Nani anayewajua hao wanahip hop wa hizo nchi na japo ni nchi kubwa duniani. Wawe real, huwezi kushindana na wamarekani kamwe that's why Ali Kiba anatusua ulaya cause anafanya kitu tofauti. Kuna maunderground wangapi marekani ambao hawajatoka na wala hakuna mtu yeyote anayewasikliza? Nawaonea huruma sana hawa wasanii wa hip hop hapa bongo. Utakuta msanii wa hip hop bongo anahojiwa anakwambia ndoto zake ni kuwa msanii mkubwa duniani, hiyo ni ndoto ya mchana.
 
Farid Kubanda a.k.a Fid Q:
'BAYA LISILONIDHURU NI JEMA LISILO NA FAIDA.....'
'MIHADARATI YA UKUBWANI INAFANYA USICHUNGE ULIMI.....'
'MADENI KUZIDI MALIPO MWIKO....'
'NAMAMBO YAKIENDA KOMBO YAACHE USIENDE NAYO'.
Prof. Chuo kikuu cha gheto, namkubali balaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom