Ni muhimu sana kujifariji na kujitia moyo, pamoja na machungu na hali ngumu unayoipitia ni vema ukafanya vitu vitakavyokufariji na kukupunguzia machungu ili nawe ujione unastahili kuishi kwa raha na akili na mwili wako unaburudika kwa maisha unayoishi tofauti na hivyo ni kukata tamaa ya maisha na unaweza hata kujiua. Huyo pichani pamoja na kukosa nyumba/ofisi lakini bado anajifariji kuwa anaofisi akiwa na matarajio ya kuwa na nyumba/ofisi siku moja! hapo hawezi kupasuka moyo kwa uchungu wa kutokuwa na vitu hivyo maana amejitengenezea faraja ambayo itamtia nguvu kutafuta kwa bidii vitu hivyo!