Chumchang Changchum
JF-Expert Member
- Nov 1, 2013
- 6,130
- 6,409
WE NDIO MBURULA.....mtoa mada kazungumzia mshahara sio matumizi.........unaonyesha umbulula wako UK mlo unapata hadi GBP 2 mshamba wewe....chips kuku/burger/chinese mitaani huku hazina bei....chakula bei ya kutupa.....mcdonals,kfc,burger king ukiwa na GBP 4 unakula fresh tu.....
Du! Mkuu Excel unadhani kule wanafanya kazi kwa masaa matano au nane kwa siku? Free market ndo nzuri fursa kwa wote kuzalisha kwa ubora na kupeleka mzigo sokoni, sio free market ya mahouse girl uarabuni. Wadada wa dar ndo nini, unadhani kusista duu ataenda huko au hata aliye na elimu yake?! nawasisi sana na,kiwango cha msomi aneenda kuwa mfanyakazi wa ndani huko??!!? Kila atakae wezeshwa ataweza tuu, karoti, matikiti maji, nyanya, mabiringanya na makabichi ya ajabu yale ya rangi ya zambarau unadhani zinachukua hata miezi mitano kukomaa na kuvunwa?!?! Ndugu kilimo hicho rahisi sana hatuwezeshwi, weka pambeni spinach, chiniz na mchicha, vipi ndugu!
lakini mkuu tatizo liko wapi? wapi palipokosewa hasa?
hmm! nimesikia kwamba mbunge wa temeke, sijui ndo hiidd haazzan sijui nani eti anahusika?
hmm! nimesikia kwamba mbunge wa temeke, sijui ndo hiidd haazzan sijui nani eti anahusika?
mkuu, samahani kwa usumbufu lakini, tukifananisha maisha ya UK na USA, wapi kuna ugumu?
ya UK magumu
hio tsh 200,000 ni mshahara wa siku moja[8hrs] kwa kazi kama hio UK.
Ingawa mambo mengi yamechanganywa humu kuanzia uarabini,uingereza na pia bado exel auliza kuhusu utofauti wa maisha baina ya UK na US, hebu niongelee kuhusu falme za kiarabu ambazo ni sita tu Saudia, UAE, Kuwait, Bahrain, Qatar na Oman.
Wafanyakazi wengi wa ndani na madereva wa familia wanatoka India, Sri Lanka ,Philippines, na far east kwa ujumla lakini wengi wa kutoka Philippines ni wataalamu huwa wanachukuliwa kama nurse,
Unapokwenda huko unakuwa na sponser wako ambapo utakaa kwa miaka miwili au zaidi inategemea na permit, na mshahara ni mdogo kwani unakula na kulala kwake kazi zote utafanya kama ni safari utaenda nao,
Hayo ni Arab world ,
Sasa hao wamepitia maisha hayo magumu na kuamuwa kuwaachia nyie na nyie mkaja shtuka baada ya miaka 50 tough!
Kwa $125 kwa mwezi sina uhakika maana nakumbuka miaka ya nyuma sana walikuwa wanapata $100 that's almost 30 yrs ago,
Uongo unakuja kwa madalali kuwahadaa watu,kama ukiambiwa maisha mazuri chakula bure pa kulala bure na mshahara laki 2 nafikiri wengi wenu mtakurupuka na kwenda
Lakini mkae mkijua mlo pekee ni elfu 8
Ok haya ya UK ni mengine huko nako kwa mshahara wa kiwango cha chini huwezi kula burger kila siku kwani ni £4 sasa una familia unaenda kula MacDonald umebaki na nini? Maisha ni ghali sana kwani unalipa kachumba £100 (260,000) kwa wiki bado bills,chakula,petrol,insurance,na mengine mengi sasa niambie hata £10 SAA bado unapumulia mrija yaani ni maskini tu
Nafikiri utafiti wako nimeutosheleza ingawa ni mengi ya kueleza, lakini mada ni Arab world,
Kwa MACHO yangu NILISIKIA BBC kademu toka Uganda kakilalama kuwa kalidhulumiwa kijinsia na kufanywa mtumwa wa ngono kwa miaka 3 bila kutoka nje.
Huu ushuhuda mpya nao wa kuangaliwa sana. Waarabu ni habari nyingine
Kama sikosei ni Abbas Mtemvu