Feedback Baada ya Kununua PowerBank na Ushauri Kwa Wengine

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
Hello JF Tech.... Poleni n Pirika Za Uchaguzi

Siku chach kabla ya Uchaguzi Nilikuwa Dillema Katika Kwenda Kununua Power Bank Na Wasiwasi Mkubw ni Kuwa Power Bank Nyingi Ni Fake..

Sasa Juzi Hapa Kabla Ya Zoezi la Kupiga Kura Nikaenda Maduka ya Simu Ninayoamini yanauza Vitu Genuine au 'Orginal' Nikachukua Power Bank Moja Inaitwa MI

Baada ya Kuichukua Nikaitest Pale Pale na Ikawa Inafanya Kazi Vizuri Kulingana Na Simu yangu....

Nikaja Nayo Home na Kuicharge Mpaka Full Charge maana Umeme Ulikuwepo. Huku Nikiwa Naangalia Jinsi ya Kutambua Fake Power Bank za MI Youtube na Nikahakikisha Kuwa Yangu Ni Original kabisa... Kabla Ya Kununua Nilikuwa nilihakikisha Kuwa Power Bank Output yake Inafanana Na Charger Yangu Ila Wasiwasi Wangu ulikuwa je nitapata Matokeo Yale yale kama nikiwa Na Charger yangu Kwenye Umeme wa Kawaida.. Chief-Mkwawa alisema Kwa Vile Simu yangu inatumia Quick Charger kwahiyo nisitegemee matokeo yale yale kama Ya Charger yangu Ikiwa Nimeiweka Kwenye Umeme wa Kawaida..

Ila I Thank God kwamba Matokeo niliyopata Ni Yale Yale kama Ya Charger yangu nikiwa Nimechomeka kwenye Umeme.. (AC)


USHAURI

Power Bank Zinatofautiana Nilipokuwa Pale Nilijaribu Power Bank Nyingine.. ambayo ni Genuine pia Ila Simu yangu ilikuwa Haina Charge kabisa kwahiyo nilipoijaribu ikakataa kuicharge Kabisa Ikiwa haina Moto hata Kidogo... ila Nilipoiweka Kidogo Kwenye Moto nikaiwasha Ile Power Bank Ikaweza Kuicharge..

Kwahiyo Nilikuwa Nawashauri Watu Ambao. wanataka Kununua Power Bank Please kanunueni kuliko Kuagiza Maana Unaweza Pata Hasara Hiyo Power Bank Ikashindwa Kucharge Simu yako...
 
Last edited by a moderator:
Power Bank... MI 10400mah
 

Attachments

  • 1445928494984.jpg
    1445928494984.jpg
    9.3 KB · Views: 307
kwa kuongezea zaidi hio ni powerbank ya xiaomi, hata hapa kwetu kuna jamaa alienda china ametuletea ni nzuri sana na ukichaji haipati joto.
 
Kuna rafiki yangu anauza product za Anker (http://www.amazon.com/s/ref=nb_sb_noss?url=search-alias=aps&field-keywords=anker) pale posta mpya opposite CRDB Bank next to ile benki nyingine pale nadhani ni Postal Bank. Anazitoa Amazon reviews zake ukiangalia ni nzuri sana. Pia mimi ninayo ya AData nilinunua pale mitaa ya Clock Tower karibu na ile bustani kona ya India/Aggrey St ni nzuri ile inachaji polepole pamoja na kwamba wanadai inatoa 2 Amps.

15mk5nc.jpg
 

Attachments

  • 15mk5nc.jpg
    15mk5nc.jpg
    42.7 KB · Views: 138
Mm nashindwa kuelewa power Bank 12000 mah lakini inachaji mara 3 kwa Simu yenye Betti ya mah 2000 hili likoje
 
Mm nashindwa kuelewa power Bank 12000 mah lakini inachaji mara 3 kwa Simu yenye Betti ya mah 2000 hili likoje

hapo pagumu sana yangu hivyo hivyo ila jana nimepoteza kwenye tahmeed waungwana hawakunikumbusha kama naisahau wakaikomba nimeumia sana
 
Mm nashindwa kuelewa power Bank 12000 mah lakini inachaji mara 3 kwa Simu yenye Betti ya mah 2000 hili likoje

1. unapochaji kuna umeme unaopotea, ila kupoteza 6000mah kwenye kila 6000mah ni pakubwa hapo labda haipo optimized vizuri

2. inawezekana pia ikawa fake haina 12,000mah wakawa wameandika tu
 
hivi najuaje kama ni original au feki?

Zingatia Unanunua Power Bank Kwenye Duka Linaloaminika

Angalia Jina La Power Bank Au Brand Name Yake Then Ingia internet Search Website yao kama ipo

Ingia Kwenye Internet Search Pia Fake Power bank ya Brand Yako kam Zipo


Mi ndo Nilivyofanya Kugundua Power bank Fake za MI.. na Nikajiridhisha kwamba hii niliyonunua Siyo Fake
 
Zingatia Unanunua Power Bank Kwenye Duka Linaloaminika

Angalia Jina La Power Bank Au Brand Name Yake Then Ingia internet Search Website yao kama ipo

Ingia Kwenye Internet Search Pia Fake Power bank ya Brand Yako kam Zipo


Mi ndo Nilivyofanya Kugundua Power bank Fake za MI.. na Nikajiridhisha kwamba hii niliyonunua Siyo Fake

Mkuu tuelekeze ulinunua duka gani kama hutojali
 
Back
Top Bottom