Fedheha kwenye vyombo vya usafiri wa umma

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,955
6,885
Habari zenu watu wa Mungu.

Dah, hapa sina kazi ya kufanya nimekumbuka Jana jioni nilikwazika sana, Kiufupi mimi nikijana mpenda amani sana, sio muongeaji sana, na pia muda mwingi napenda kuwa mwenyewe mwenyewe, Hua sipendi fedhea kabisa haswahaswa vita za maneno yenye Matusi au kuaibishana na mtu, ingawa nina sifa zote hizo ambazo zinaweza kufanya mtu kuhisi Mimi Ni ennocent sana lakini bado Nina midhambi kibao

Matusi ninayo sana, Uzinzi nauwaza sana, Nikipata nafasi ya kufanya dhambi hua naifanya sana tu, Ila yote hayo nafikiri ni kwa sababu mshauri mkubwa wa Mimi ni mimi mwenyewe, najiamini kwenye maamuzi japo Kuna wakati sipo sahihi kabisa, Wakati huo ndo huu umenifanya niandike uzi huu maana hua naishia kujilaumu baadae.

Okay twende kwenye point, Ni kwamba Jana usiku nimepanda daladala kutoka M-moja hadi Tabata ambapo ndo ninapoishi, Kabla ya kufika nikampa konda sh.5000 akate 400 yake anirudishie change, Nikawa nasubir change konda akawa bize kuchukua nauli kwa wengine Hadi nikafika kituo changu husika

Gari liliposimama abiria wanaoshuka pale wakaanza kushuka mi nikaona hawa wakimaliza kushuka hapa gari linaweza kuondoka me nikiwa bado ndani nasubiri change, Ikabidi nimshtue konda "Oooy vp nipe change yangu nishuke.." Konda akanipatia change kisha akaniuliza "Unashukia hapa" nikamuambia ndio (wakati huo dereva kashaanza kudrive

Yule konda akogonga gari kumshtua dereva asimame kwani Kuna mtu hajashuka bado ambae ndo Mimi, Ubaya unakuja pale konda aliponiambia "Shuka chini sasa muda wote gari limesimama ulikuwa unasubiri nini" nikamjibu "nilikuwa nasubiri change" konda akajibu kwa sauti ya juu sana ya jazba "AYA USHAPEWA HELA YAKO SHUKA CHINI" Me kile kitendo kikaniuma sikushuka Ikabidi nimuulize kwanini ananiongelea vile wakati yeye ndo alienichelewesha?

Jamaa akanijibu "Ndio nakujibu" Dah me nikashindwa kuvumilia nikajikuta nimemtukana "We Mse.... Kweli" jamaa akanijibu "Msee... Mwenyewe" Gari wakati linaondoka nikaruka chini kisha nikamuonesha ishara ya kumtukana kwa Dole.... Jamaa nikamuona kwa mbali kama imemuingia sana hio ya ishara maana watu wote waliona lile tukio yeye alikosa target ya kunijibu tusi la mwisho wakacheka.... Mimi binafsi baada ya lile tukio sikupenda maana nilikuja kulitafakari baadae nikaona sikufanya fea Bora Yule jamaa baada ya kunipa change yangu hata alivyonipandishia sauti nisingepanick maana pengine Yule jamaa akili yake haikuwa sawa, Ila kusema ukweli Ile kitu ilinikata sana nikashindwa kujizuia,

Ebu nipeni visa vyenu vyenye fedhea vilivyowatokea kwenye usafiri huu wa UMMA ili nijifunze kuchukua maamuzi mazuri juu ya Hawa makonda wa daladala maana kitu kidogo mnaweza mkadhalilishana, Na ukumbuke wewe abiria ndo unaedhalilika zaidi maana Mavazi ya wale jamaa tu yanatosha kueleza kuwa wewe hupaswi kugombana nao? Siwasemi vibaya Ila tuchukulie mfano mtu umevaa Suti yako au T-shirt na Jeans yako safiii alafu ugomvi uanze kati yako na konda Nani anajiaibisha zaidi?
 
Mambo mengine mnajitafutia stress na kudharaulika bure tu.

Jifunze ku ignore mambo ya kipuuzi. Haikuwa na haja kuanza kunibishana na konda huyo ungechukua change yako hata kama alikutolea maneno makali unamtizama unamwacha tu mwishowe yeye atajiona mjinga tu.

Sasa hebu fikiri umejichoresha vipi kwa watu kwa kuanza kutukanana na konda?

Hebu fikiri wakati mnatoleana matusi gari imeanza kuondoka ukaruka je ungepata majeraha labda umevunjika ingekuwaje?

Hebu jiulize ni watu wangapi waliokuwa kwenye hilo bus ambao kuna potential ya kuja kufanya nao kazi/biashara au kuunganika nao kwa njia yoyote? Je siku unakutana na mtu mfano mfanye jambo la msingi akakumbuka aliwahi kukuona ukirushiana matusi na konda unadhani atakuweka katika kundi gani?

Jifunze kuwa na busara kaka. Hata ukiwa umechukizwa kuwa na tabia ya kumpuuza unaeona anakushusha kiwango kwa kuanza kujibishana nae.

Buddha amewahi kusema

1. "Stop trying to calm the storm. Calm yourself the storm will pass."

2. "Do not be upset with people or situations, both are powerless without your reaction".
 
Uko na haraka zako Gari limeshajaza level seat linaanza kusimama kituo kimoja kimoja kujaza abiria (konda anasema leupe kabisa)

Tabia ingine ambayo hunikera unakuta Daladala linatumia muda mrefu kupakia abiria wengi kwenye kituo cha katikati ambacho sio kituo kikuu/stendi na hata akiwa stendi kashajaza level siti na mistari miwili bado atapoteza muda hapo weee hadi muanze kufoka ndio wanatoka

Sent from my SM-J720F using JamiiForums mobile app
 
Kuna Ile Tabia umebanwa Hadi unapumulia watu migongoni alafu gari linasimama kila kituo makonda anapiga kelele utasikia "gari leupeeee halina watu kabisa"
Huwa namtukana sn konda kimoyomoyo

Watu wa daladala tuna maisha magumu sn walah

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Lol. Usiombe upande daladala zile zipo juuuu halafu dereva ana breks za ovyo.
 
Mambo mengine mnajitafutia stress na kudharaulika bure tu.

Jifunze ku ignore mambo ya kipuuzi. Haikuwa na haja kuanza kunibishana na konda huyo ungechukua change yako hata kama alikutolea maneno makali unamtizama unamwacha tu mwishowe yeye atajiona mjinga tu.

Sasa hebu fikiri umejichoresha vipi kwa watu kwa kuanza kutukanana na konda?

Hebu fikiri wakati mnatoleana matusi gari imeanza kuondoka ukaruka je ungepata majeraha labda umevunjika ingekuwaje?

Hebu jiulize ni watu wangapi waliokuwa kwenye hilo bus ambao kuna potential ya kuja kufanya nao kazi/biashara au kuunganika nao kwa njia yoyote? Je siku unakutana na mtu mfano mfanye jambo la msingi akakumbuka aliwahi kukuona ukirushiana matusi na konda unadhani atakuweka katika kundi gani?

Jifunze kuwa na busara kaka. Hata ukiwa umechukizwa kuwa na tabia ya kumpuuza unaeona anakushusha kiwango kwa kuanza kujibishana nae.

Buddha amewahi kusema

1. "Stop trying to calm the storm. Calm yourself the storm will pass."

2. "Do not be upset with people or situations, both are powerless without your reaction".
Yah, kuonesha ninajali na ninaelewa hilo ndo maana nikaandika kuwa nimejutia kufanya vile
 
Back
Top Bottom