DOKEZO Fedha za nauli za Walimu wa Sekondari katika Halmashauri ya Madaba Mkoani Ruvuma hazijalipwa

DOKEZO Fedha za nauli za Walimu wa Sekondari katika Halmashauri ya Madaba Mkoani Ruvuma hazijalipwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa Halmashauri ya MADABA Mkoa wa RUVUMA katika idara ya elimu sekondari.

Changamoto kubwa tunayoipitia kama Walimu ni kuwa fedha za nauli ya likizo ya malipo kwa Mwaka 2024 Mwezi wa 12 mpaka sasa hivi haijalipwa lakini Walimu wa Elimu ya Msingi wao fedha za malipo ya nauli wamepata.

Lakini pia Walimu waliopaswa kulipwa fedha za nauli kwa ajili ya likizo Mwaka 2025 kwa mwezi wa sita mpaka sasa hakuna matumaini kabisa na majibu ya kueleweka. Kwa hiyo walimu waliopaswa kulipwa fedha kwaajili ya nauli 2024 mwezi wa 12, na mwezi wa sita 2025 wote wanadai, kwa walimu wa elimu ya msingi hakuna anaedai kwanini sisi walimu wa sekondari?

Naomba kama thread hii inaweza fika kwa wenye mamlaka watusaidie majibu fasaha, mazingira ya kazi shida, hata kupata stahiki zetu inakuwa changamoto.
 
Subiri Brigedia Generals amesikia, na atafanyia kazi.
 
Mkuu nipo madaba tangu jumanne., nimekuja kutembelea kaburi la marehemu mama angu maeneo ya kipingo.

Embu sogea hapa VIP lounge tupate chupa kadhaa za kuchangamsha akili. Hii serikaki yetu changamoto huwa haziishi
 
Sio yetu tu.
 
Back
Top Bottom