Fedha za Mishahara ATCL zisitoke Serikalini

kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,868
2,760
Hii inaweza kuwa habari mbaya kwa uongozi wa ATCL Ila serikali ikisitisha kulipa mishahara wafanyakazi wa ATCL kampuni itajiendesha kwa ubunifu. Tokea kuwasili kwa ndege kampuni bado haijapata wafanyakazi wabunifu ili kuweza kulifufua shirika na kuweza kujiendesha kibiashara. Uongozi hauna mkakati wowote endelevu kwasababu wanajua hata wakiboronga mishahara inatoka hazina. Sasa ni muda Muafaka serikali isitishe mishahara ya watumishi wa ATCL ili wawe wabunifu na kujilipa wenyewe.
 
Something like this sounds good na pili mishahara yao ingetokana na income ya mwez kampuni iliyo ingiza kma kuna hasara mshahara unadrop kwa percentage ambayo IPO fixed na kma kuna faida vice verse ifanye
 
Hebu acha ujinga huo! imagine mzazi wako yupo huko anategemea alete chakula nyumbani kwenu!
Halafu mtu anashauri anyimwe mshahara
 
Hebu fanya utafiti uone linaendeshwaje and what are the outside interferences?
 
Hebu acha ujinga huo! imagine mzazi wako yupo huko anategemea alete chakula nyumbani kwenu!
Halafu mtu anashauri anyimwe mshahara
Sijasema wanyimwe mshahara. Nimesema wajilipe kutokana na mapato yao
 
Hawa watakuwa wanawaza kujenga nyumba na kununua magari, sina uhakika kama wanajua kuwa mteja mmoja anayeenda one way Mwanza au arusha ndiye chanzo cha uwepo wao!
 
Hawa watakuwa wanawaza kujenga nyumba na kununua magari, sina uhakika kama wanajua kuwa mteja mmoja anayeenda one way Mwanza au arusha ndiye chanzo cha uwepo wao!
Hawako independent na hawana maamuzi
 
Kuna mashirika walikuwa wanafanya vizuri wakawa wanajilipa 40 millioni, juma akakataa sasa na wewe unashauri nini maana wakijituma wakapata kingi na kujilipa pesa kubwa watu roho zinawauma
 
Kuna mashirika walikuwa wanafanya vizuri wakawa wanajilipa 40 millioni, juma akakataa sasa na wewe unashauri nini maana wakijituma wakapata kingi na kujilipa pesa kubwa watu roho zinawauma
Wajilipe hata milioni Mia lakini hawatakiwi kupokea hela toka serikalini.
 
Hili shirika lifutwe tu tujue moja Pangaboy zipelekwe jeshini maana hakuna wa kuyapanda mandege ya vita ya kwanza ya Dunia hayo
 
Back
Top Bottom