FEDHA za MIKOPO zayeyuka UDOM... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FEDHA za MIKOPO zayeyuka UDOM...

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by VUTA-NKUVUTE, Jun 19, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ni ishara na uthibitisho wa ufisadi.Ni pale Chuo Kikuu cha Dodoma almaarufu kama UDOM.Fedha kwa ajili ya mkopo wa ada kwa wanafunzi waliomaliza chuoni hapo mwaka jana zimeyeyuka.Wanafunzi hao ambao wanamiminika Chuoni hapo kwa ajili ya kuchukua 'Transcripts' na vyeti vyao wamejikuta wakidaiwa fedha kuanzia laki tatu na arobaini na kuendelea hadi milioni moja na ushee.

  Kilichotokea

  Taarifa zilizonifikia zinaonyesha kuwa wanafunzi hao walitakiwa kusaini(walipokuwa mwaka wa kwanza 2008) fomu maalumu toka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuonyesha kupokea kwao fedha walizolipiwa na Bodi.Zilitakiwa zijazwe fomu mbilimbili.Uongozi wa Chuo ukawasainisha fomu mojamoja.Tatizo kubwa.

  Fedha zikaonyesha zimelipwa nusu ya kiasi kilichotakiwa.Wanafunzi walipokwenda Bodi-Tawi la Dodoma kuulizia kuhusu madeni wasiyoyatarajia,walielezwa kuwa fedha hizo zilishapelekwa UDOM na hazikuwahi kurudishwa.UDOM wakadai fedha hizo zilisharudishwa Bodi.Dana dana.Maumivu kwa wanafunzi.Wengi wa wanafunzi wameshindwa kuchukua vyeti vyao.Fedha zimeyeyuka.Nani amekula pesa hizi? Na ajitokeze...
   
 2. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mlacha na kundi la mafisadi wenzake ndo wamekula hizo pesa.Nasikia hako ka mchezo ka kutokusainishwa baadhi ya fomu za majina ya wanafunz wanaoendelea kusoma hapo hasa semister hii ya mwisho hawajasaini! Na weng wao ndo wanamaliza chuo na tayar wameshaanza U.E wakimaliza tu ni kwao wakirudi hapo chuoni kuja kuchukua vyeti vyao watakuwa na madeni ya ada ya kufa mtu hata wakifanya clearance haisaidii kitu. Sasa basi mhe. J.K huu ndo uongozi bora kwa chuo chako ilhali watoto wa maskini wanaibiwa mchana kweupe?.J.K mulika mwizi wa UDOM KUKWEPA LAWAMA NA LAANA YA KUANGUKA KWA UTAWALA WA CCM JUA KUWA HILI NI BOMU TENA LA NYUKLIA.MTOE MLACHA UMPELEKE KWINGNE AU UMPE UBALOZI AKAFIE MBALI.MLACHA NI KIRUSI ZAID YA KILE CHA UKIMWI CHUONI UDOM.
   
 3. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Yaani,wizi kila kona...
   
Loading...