Fedha za MCC tunazihitaji, masharti yanatekelezeka

Fedha za MCC tunazihitaji, masharti yanatekelezeka

Uchaguzi mpya ufanyike haraka iwezekanavyo mambo yaishe, maalim naye aheshimu sheria aache mambo yake ya kujitangaza utafikiri yeye ndo ana mamlaka
Kujitangaza Maalim Seif kuwa kashinda siyo issue.
Mbona Makamba naye alimtangaza JPM kuwa anaelekea kushinda Urais kabla NEC haijamtangaza mshindi?
Hapo sioni kama kufutwa kwa uchaguzi huo kunatokana na Maalim Seif kujitangaza mshindi.
Hivi kama aliyeshinda sio Maalim Seif, hivi hicho ndiyo kizingiti kikubwa kilichofanya ZEC ishindwe kumtangaza huyo mwingine aliyeshinda?
 
kwani lowassa angejitangaza hapa Tz bara uchaguzi ungerudiwa,kuna haja gani ya kufanya uchaguzi kama una uhakika mgombea wako atashinda.acha mahaba ya kike

Bila matusi huwezi kutoa hoja mkuu?
 
Ni rahisi kwako kusema hivyo
lakini wanaotegemea hizo pesa kwa maisha yao watateseka tusipozipata
sikumbuki kama nipo sahihi lakini ARV za bure si ndo zinatolewa kwa pesa hizi?

Sina uhakika kama ununuzi wa ARV zinategemea fedha hizo. At least muda sasa hatujapata fedha hizo na serikali imemudu. Ndio mwanzo wa self reliance.
 
Shirika la Kimarekani linalolenga kusaidia kuondoa Umasikini Afrika, mbona maneno hayarandani Hata.... Sioni kama kuna ukweli wowote. Unaondoaje umasikini huku unafadhili zaidi ya nusu ya vita zinazowatia umasikini Waafrika?
 
The culture of conceding defeat and peaceful hand over of power is still in its infancy stage in most African countries including Tanzania.The Tanzania mainland situation would have been the same to the current situation in Zanzibar if Lowassa had won.
We still need an external force to enforce democratic elections.Period.

Nchi hii ya Nyerere INA kanuni zake za uendeshaji, na hii ni kwa faida ya wote, kwa hiyo tulia.
 
Hivi hii MCC si ndio imetuletea Richmond/Symbion inayotunyonya mabilioni ya pesa kila siku?basi wakwende zao.
 
Tuachane na mambo ya misaada.tukivuka hili tutaambiwa tunakandamiza haki za mashoga.malawi wameondoa kesi mahakamani kuhusu mashoga kuoana,kisa walizuiwa msaada wa pauni milioni 400.wakaona bora wawaache walawitiane kuliko kuzikosa ?400 milioni
 
Hatimaye Tanzania imekosa fedha za Millenium Challenge Corporation (MCC) zilizotarajiwa kutolewa kwa lengo la kupunguza umaskini nchini. MCC ni shirika la Kimarekani linalolenga kupunguza umaskini barani Afrika. Njia inayotumiwa na shirika hilo ni kutoa fedha za kimsaada kuelekeza katika sekta za kimaisha ili kupunguza umaskini.

Nchi mojawapo iliyokwishanufaika na fedha hizo ni Tanzania. Mara hii Tanzania imesitishwa kupewa msaada huo wa MCC kwakuwa kuna masuala ya kiutawala yanapaswa kufanyiwa kazi. Masuala hayo ya kiutawala yanayopaswa kufanyiwa kazi ndiyo hasa masharti ya kutimizwa na Tanzania kama nchi katika kupata msaada huo.

Katika taarifa ya MCC, masuala hayo ya kiutawala hayakutajwa. Hatahivyo, wachambuzi wa mambo wameyataja kama ni mgogoro wa kikatiba na kisiasa Zanzibar pamoja na Sheria ya Makosa ya Kimtandao. Ndiyo kusema, Tanzania ikishughulikia mgogoro wa Zanzibar na 'kuweka sawa' baadhi ya vifungu vya Sheria tajwa, Tanzania itapata fedha za MCC.

Iko wazi kuwa Tanzania Tanzania inazihitaji fedha hizi za MCC ili kusaidia katika sekta mbalimbali za kimaendeleo. Ndiyo maana hata Serikali ilikuwa ikijivunia kuwekwa kwenye orodha ya kupata fedha za MCC kwa kupitishwa kwenye vikao vya MCC (kumbuka kauli ya mmoja wa viongozi wa Serikali wakati wa sakata la Escrow).

Tunapaswa kama nchi kutatua mgogoro wa Zanzibar. Kama kilichoripotiwa leo ni kweli, kwamba Rais Magufuli amekutana na Maalim Seif Sharrif Hamad Ikulu, basi kuna dalili kuwa Serikali imedhamiria kuutatua mgogoro wa Zanzibar. Mgogoro wa Zanzibar unapaswa kutatuliwa kwa kutenda haki na kusonga mbele kama Taifa.

Kuutatua kwake ni aidha kuendelea na mchakato wa kutangaza matokeo (kwa kuachana na kauli ya Mwenyekiti Jecha wa ZEC kufuta uchaguzi wote Zanzibar) au kwa kukubali kufanya uchaguzi upya. Ifahamike kuwa mgogoro haupo kwenye Urais tu. Upo pia kwenye Uwakilishi na Udiwani kwakuwa wote hao wameathirika na kauli ya Mwenyekiti Jecha.

Lakini, kwanini Dr. Shein naye asifanye mazungumzo na Rais Magufuli au wote watatu kwa pamoja? Kuhusu sheria, inapaswa kurekebishwa Bungeni na mambo mengine kuendelea. MCC wakijiridhisha juu ya hilo, Tanzania itapata fedha ambazo inazihitaji. Yote yasemwe lakini fedha za MCC zinahitajika na masharti yaliyowekwa yanatekelezeka.

Zanzibar hakuna mgogoro, hakuna chama kilicho toa malalamiko mpaka uchaguzi umeisha, na kila alie shinda alipewa nakala maalum ya ushindi, sasa kufutwa matokeo ni uhuni na hatuko tayari kurudi kwenye uchaguzi.

Kutatua mgogoro wa zanzibar, usalama wa taifa ni kuiyachia tume kuendelea na kutoa matokeo, kwani mwenyekiti ametekwa nyara na usalama.

Waangalizi wa kimataifa walishuhudia na kumuona mwenyekiti akichukuliwa chini ya ulinzi.
 
kaka hacha kunifurahisha,hi kiti ni plan toka miaka hiyo ya vita baridi walipo anzisha mgogoro wa chumi kwa nchi nyingi kwa kutumia uhaba wa mafuta uliopelekea nchi kuporomoka kiuchumi.hukumbuki miaka ile nyerere anawambia wananchi wafunge mikanda ilikuwa shida ni kutokubaliana na mashariti na mabadiliko ya kisera na itikadi wananchi wengi walivyo wajinga hawakuliana hili.
Kiufupi kama ilishindikana kipindi cha nyerere hapa ni majuto mpaka hapo afrika itakapo ungana au bank ya BRICS itakapo anzishwa.
Mkuu ningpenda kuiweka perspective ya aliyosema Mwalimu tufunge mikanda.
Ilikuwa baadaya vita ya kumg'oa Idi Amin mwaka 1979, vita iliyotugharimu sana kiuchumi. Mwalimu alisema tutafunga mikanda kwa miezi 18!
Hayo ya kutokubaliana na IMF yalifuata.
 
Uchaguzi mpya ufanyike haraka iwezekanavyo mambo yaishe, maalim naye aheshimu sheria aache mambo yake ya kujitangaza utafikiri yeye ndo ana mamlaka

Ukweli daima utatuweka huru. Kujitangaza ni kkosa moja na kushinda ni suala lingine bwana mito. La msingi hapa ni kuwaombea kwa Mungu wetu Allah ili wayamalize kwa amani na salama na kwa wakati muafaka ilia waendelee kula matunda ya uhuru na amani yao iliyodorora. Uchaguzi wa nini wakati mambo yako wazi???????????????? Maalim ni shujaa leo na kesho na daima.
 
Mnafik mkubwa wewe. Eti unaishi bila umeme tangu nchi hii ipate uhuru wakati unashinda hapa JF usiku kucha kuperuzi na kumwaga pumba. Achana na hiyo lugha ya kuzungusha mikono aisee, imepitwa na wakati.

Sasa kashfa za nini wakati huo ni mtazamo binafsi????????????? kama wewe una mawazo makubwa zaidi msaidie bana, Unaboa sana man.
 
ukawa ni walemavu wa akili waliokubuhu kwenye utegemezi.
 
Back
Top Bottom