Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Hatimaye Tanzania imekosa fedha za Millenium Challenge Corporation (MCC) zilizotarajiwa kutolewa kwa lengo la kupunguza umaskini nchini. MCC ni shirika la Kimarekani linalolenga kupunguza umaskini barani Afrika. Njia inayotumiwa na shirika hilo ni kutoa fedha za kimsaada kuelekeza katika sekta za kimaisha ili kupunguza umaskini.
Nchi mojawapo iliyokwishanufaika na fedha hizo ni Tanzania. Mara hii Tanzania imesitishwa kupewa msaada huo wa MCC kwakuwa kuna masuala ya kiutawala yanapaswa kufanyiwa kazi. Masuala hayo ya kiutawala yanayopaswa kufanyiwa kazi ndiyo hasa masharti ya kutimizwa na Tanzania kama nchi katika kupata msaada huo.
Katika taarifa ya MCC, masuala hayo ya kiutawala hayakutajwa. Hatahivyo, wachambuzi wa mambo wameyataja kama ni mgogoro wa kikatiba na kisiasa Zanzibar pamoja na Sheria ya Makosa ya Kimtandao. Ndiyo kusema, Tanzania ikishughulikia mgogoro wa Zanzibar na 'kuweka sawa' baadhi ya vifungu vya Sheria tajwa, Tanzania itapata fedha za MCC.
Iko wazi kuwa Tanzania Tanzania inazihitaji fedha hizi za MCC ili kusaidia katika sekta mbalimbali za kimaendeleo. Ndiyo maana hata Serikali ilikuwa ikijivunia kuwekwa kwenye orodha ya kupata fedha za MCC kwa kupitishwa kwenye vikao vya MCC (kumbuka kauli ya mmoja wa viongozi wa Serikali wakati wa sakata la Escrow).
Tunapaswa kama nchi kutatua mgogoro wa Zanzibar. Kama kilichoripotiwa leo ni kweli, kwamba Rais Magufuli amekutana na Maalim Seif Sharrif Hamad Ikulu, basi kuna dalili kuwa Serikali imedhamiria kuutatua mgogoro wa Zanzibar. Mgogoro wa Zanzibar unapaswa kutatuliwa kwa kutenda haki na kusonga mbele kama Taifa.
Kuutatua kwake ni aidha kuendelea na mchakato wa kutangaza matokeo (kwa kuachana na kauli ya Mwenyekiti Jecha wa ZEC kufuta uchaguzi wote Zanzibar) au kwa kukubali kufanya uchaguzi upya. Ifahamike kuwa mgogoro haupo kwenye Urais tu. Upo pia kwenye Uwakilishi na Udiwani kwakuwa wote hao wameathirika na kauli ya Mwenyekiti Jecha.
Lakini, kwanini Dr. Shein naye asifanye mazungumzo na Rais Magufuli au wote watatu kwa pamoja? Kuhusu sheria, inapaswa kurekebishwa Bungeni na mambo mengine kuendelea. MCC wakijiridhisha juu ya hilo, Tanzania itapata fedha ambazo inazihitaji. Yote yasemwe lakini fedha za MCC zinahitajika na masharti yaliyowekwa yanatekelezeka.