Fedha za maafa Kagera zimetafunwa?

Fedha za maafa Kagera zimetafunwa?

amos eglan

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2015
Posts
310
Reaction score
464
Ndugu zangu, habari za muda huu!

Nawasilisha Uzi huu kutaka kujua sintofahamu juu ya pesa walizochangia wananchi kuhusu maafa ya tetemeko la Kagera maana watu bado wanateseka wanalala nje wakipigwa na baridi ilhali watanzania wenzao walijinyima kuwasaidia.

Sasa mpaka muda huu sijaelewa ni kwanini pesa hazijawafikia na wakati ni swala la dharura ili bidi iwafikie punde wananchi hao waliofikwa na tetemeko au wanafanyiwa uhakiki.

Kwa hali hii wananchi watashindwa kusaidia wenzao pindi wanapofikwa na maafa maana hawatakuwa na imani juu ya uwasilishwaji wa msaada.

Kwa sababu haujatoka serikalini bali ni utu wa wazalendo au kuna siasa katika hili? Mwananchi mmoja aliongea kwa masikitiko eti anaambiwa anza kujenga kwanza ukifika juu tutakusaidia kweli jamani.
 
Sorry uthibitisho muhimu sana mkuu kama kweli Fedha zimeliwa,
 
SERIKALI ITAKUWA HAINA HELA....HELA ZA MAAFA WATAKUWA WAMEZITUMIA KWA SHUGULI ZINGINE TU....

OVA
 
Kwanza lazima uelewe serikali ilishatamka kuwa haitamjengea mtu nyumba
 
Pengine ziligeuka Posho Masikini....we kama ni Kweli... Wanaohusika wanatakiwa wapewe Show cause letter waeleze kinagaubaga
 
Katika hili kama hawatawajengea nyumba wananchi watapata dhambi kwa mungu na huenda ndio fedha za kujengea makazi ya serikali dodoma wakat watu wanalala nje..,wao wamekazana kuhakiki wakat watu walitoa kwa moyo mo1 tena wengine wafanya biashara ambao walitukanwa sana enz za nyuma hapo kwamba hawakuombwa hata shilingi
 
Huu utawala hautafika salama kabla hayajatimia.
 
Huu utawala hautafika salama kabla hayajatimia. Ni urafi uliopitiliza
 
Ndugu zangu, habari za muda huu!

Nawasilisha Uzi huu kutaka kujua sintofahamu juu ya pesa walizochangia wananchi kuhusu maafa ya tetemeko la Kagera maana watu bado wanateseka wanalala nje wakipigwa na baridi ilhali watanzania wenzao walijinyima kuwasaidia.

Sasa mpaka muda huu sijaelewa ni kwanini pesa hazijawafikia na wakati ni swala la dharura ili bidi iwafikie punde wananchi hao waliofikwa na tetemeko au wanafanyiwa uhakiki.

Kwa hali hii wananchi watashindwa kusaidia wenzao pindi wanapofikwa na maafa maana hawatakuwa na imani juu ya uwasilishwaji wa msaada.

Kwa sababu haujatoka serikalini bali ni utu wa wazalendo au kuna siasa katika hili? Mwananchi mmoja aliongea kwa masikitiko eti anaambiwa anza kujenga kwanza ukifika juu tutakusaidia kweli jamani.
Masikini wananchi wa Kagera !
 
Kwa hiyo wanataka wafanyie nini maana msaada ule wa fedha NI kununua mabati cement watu wakarabati nyumba au wananulia unga NA mchele
 
Back
Top Bottom