Fedha za maafa Kagera zakarabati shule ya CCM

Fedha za maafa Kagera zakarabati shule ya CCM

gasto genaro

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2014
Posts
780
Reaction score
554
Bukoba. Wakati baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wakilalamikia kukosa misaada iliyotolewa na wahisani kwa wathirika wa tetemeko la ardhi, imedaiwa kuwa Shule ya Sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM imekarabatiwa kwa fedha hizo.

Madai hayo yalitolewa na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronikus Karumuna kuwa sehemu ya miundombinu ya shule hiyo yakiwamo mabweni yalikarabatiwa ili kupokea baadhi ya wanafunzi waliohamishwa kutoka sekondari za Ihungo na Nyakato ambazo zinajengwa upya.

Akichangia taarifa ya tetemeko la ardhi iliyowasilishwa jana katika Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera (RCC), Meya huyo alishutumu matumizi mabaya ya fedha hizo. Alisema haikuwa haki kutoa kipaumbele cha ukarabati wa shule inayomilikiwa na CCM badala ya sekondari za Serikali.

Meya huyo alisema kamati ya maafa kushindwa kuzishirikisha kamati za mitaa na kata kumesababisha malalamiko mengi.

Chanzo: Mwananchi
 
Chadema wana matatizo sana,mnataka watoto wa kagera wasisome?
 
Lengo si limeelezwa ili wanafunzi wa ihungo na nyakato wapate hifadhi.
Hizo shule zinatumiwa na wananchi wote.

Kama kulikuwa na shule nyingine ya serikali yenye sifa ya kupata msaada huo ili kuhifadhi hao wanafunzi wa boarding na wakaamua kuipa kipaumbele shule ya wazazi hapo ni kosa.

Nchi haiwezi kuendelea kwa majungu na uchonganishi
 
Lengo si limeelezwa ili wanafunzi wa ihungo na nyakato wapate hifadhi.
Hizo shule zinatumiwa na wananchi wote.

Kama kulikuwa na shule nyingine ya serikali yenye sifa ya kupata msaada huo ili kuhifadhi hao wanafunzi wa boarding na wakaamua kuipa kipaumbele shule ya wazazi hapo ni kosa.

Nchi haiwezi kuendelea kwa majungu na uchonganishi
Ili kuondoka hayo majungu na uchonganishi.... Mngetoa conflict of interest kwa kukarabati shule ya mtu binafsi mwingine but sio CCM!! Tunawahisi kama mlimplan hiviiii.
 
Huu ni upumbavu wa watanzania,hakukupaswa kuwa na kitu kinachoitwa kitegauchumi,wala Shule zinazomilikiwa na CCM,Shule,viwanja vya mipira,jengo la Lumumba na mali nyingine nyingi ambazo CCM inajinasibu kuwa ni zake,si zake kihalisia,zilipatikana/kujengwa chini ya mfumo wa chama kimoja,baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza,CCM ikajimilikisha Mali za umma na kuziita Mali za Chama.

Tuamke na kudai Mali za umma zilizojengwa kwa kodi zetu,na sasa zinatumika kuwaneemesha ma-interahamwe wa CCM.
 
Acheni wakarabati shule yao na 2020 itawakumbushia watu kuwa paliwahi tokea tetemeko na watu wakalala nje
 
Mi nafikiri meya angepigania toka mwanzo wanafunzi wa Ihungo na Nyakato wahamishiwe shule nyingine ambazo Hazina uhusiano na ccm lakini kunyamaza kwake mapema kumefanya hoja take kukosa nguvu
 
Hawana hata fedha ya kuwalipa mishahara Uhuru media watatoa wapi ya kukarabati shule?
Wanakamata fursa
 
Hawana hata fedha ya kuwalipa mishahara Uhuru media watatoa wapi ya kukarabati shule?
Wanakamata fursa
 
Chadema wana matatizo sana,mnataka watoto wa kagera wasisome?
Shule ya CCM ni shule binafsi.. Si shule ya serikali..

Kwanini shule binafsi ikakarabatiwe kwa fedha zilizokusanywa ili kuwasaidia wahanga??
 
Inafundisha masuala ya CCM au Masomo ya Kawaida?
Kwakuwa shule za Feza hazifundishi masomo ya CCM basi ni muda muafaka kwa serikali kuanza kuzitengea fedha kwa matumizi mbalimbali!
 
HIYO SHULE WANASOMA WANA CCM TUUU,? ACHENI UCHAWI KIJANA MDOGO MCHAWI, NA WATU WENGI WENYE KELELE KAMA ZAKO HAWAJACHANGA, BORA HATA MJUMBE WA KAMATI KUU KAKODI NDEGE YA MILIONI THELATHINI KWENDA KUCHANGIA MILLIONI SITA HAHAHAAAAA.
 
Back
Top Bottom