Hili sakata la Escrow ni ufisadi ambao uko kwenye ngazi ya kitaifa. Ndio maana unaona hata Raisi mkuu wa nchi amechanganyikiwa, atafuta mahali pa kujificha, maana yake ni kwamba the president himself knows too much. Ufisadi mkubwa kama huu unahusisha wengi kwenye baraza wa mawaziri na viongozi wakuu wa nchi. Sio sakata la mchezo, hapa tunaongelea karibu dola million 200. Raisi mwenyewe anajikanyagakanyaga anatoa hotuba isiyokuwa na mbele wala nyuma. Anatoa maelezo yanayoonyesha kama vile hana authority ya kuamua ... "Tumemuomba, prof Tibaijuka, atupishe tuteuwe mwingine, na Muhongo nimemuweka kiporo". Hicho kiporo unamwaachia nani. Na kwanini uache kiporo kiendelee kuwa madarakani wakati uchunguzi ukiendelea?. Inatakiwa wakati uchunguzi unaendelea kiporo, Muhongo, awekwe pembeni mpaka uchunguzi ukamilike. Mimi ninachoona hapa ni kwamba Hata prof Muhongo anajua kwamba raisi hathubutu kumgusa, kwa sababu wote wanayajua mengi.