FedEx and TRA issue at Dar Airport

FedEx and TRA issue at Dar Airport

Ndugu wadau wa Ughaibuni na Bongo,

Ni matumaini yangu mpo salama na mna enjoy spring season hasa kwa wale wenzangu tulio kenye ukanda wa baridi.

Nilikuwa napenda kujua kama kuna mwenye this experience anapotuma mzigo kwenda Dar na kuandikiwa ridiculous tax invoice isiyolingana na thamani ya mzigo? Kuna matukio mawili hivi: Mosi kuna siku nilikuma mzigo una thamani ya $278 na uzito wa 21 pounds, ulipofika Fedex Dar wakadai nitoe Tsh. 50,000/= processing fee na 200,000/= ya kulipa agent afanye clearance ya mzigo airport. Pili kuna mzigo mwingine nimetuma kwenda Dar kwa njia ya Fedex una thamani ya $625 na uzito wa pound 23, Fedex wakanambia upo Customs ya TRA airport, zinahitajika tsh. 50,000/= processing fee ya Fedex na Tsh.470,000/= (Laki 4 na Sabini Elfu) kuutoa mzigo kwenye custom ya TRA airport.

Kinachonishangaza, kuna rafiki yangu nipo nae hapa New York alituma mzigo wake wenye thamani na uzito sawa na scenerio namba 1 kwa Fedex kwenda Morogoro akautoa kwa kulipia Tsh. 30,000/= (Thelasini elfu tu). Ninachojiuliza, Je issue ni Fedex au custom ya TRA au kitu kingine zaidi? Mbona nikituma kwa njia ya USPS mizigo yenye thamani na uzito wa ranges kama nilizozitaja hapo juu na ikifika Posta ya Dar, wanachaji siyo zaidi ya Tsh. 10,000/= (Elfu kumi tu)?

Kingine kinachonishangaza zaidi kuna mzigo mwingine wa thamani ya euro 700 na uzito wa kg 25, niliouagiza hivi karibuni toka Germany kwa njia ya DHL, umefika Dar na ukakombolewa kwa Tsh. 2,800/= (Elfu mbili na mia nane tu).

Ninachojiuliza, je issue ni Fedex au Custom ya TRA airport au something else nisichokijua? Je ni nani yupo sahihi ( kwenye makato ya kutoa mizigo ) kati ya Fedex na TRA aiport kwa upande mmoja na Shirika la Posta na DHL Dar kwa upande mwingine?

Binafsi nahisi kama kuna kitu hakipo sawa hapo kwenye custom ya TRA airport, kuna kama kamchezo kanachezwa kutuibia kwa kutubambikia kodi zisizo na kichwa wala miguu. Kwa mfano sioni sababu ya Fedex na TRA kulazimisha agent alipwe pesa za kuutoa mzigo wakati unaweza kutolewa na mpokeaji kwa kufanya malipo ya kodi kwenye custom za TRA airport bila kumtumia agent.

Natanguliza shukrani kwa wale watakao share experience zao kwenye hii issue.

Kinyasi N Monyi
Rochester, NY.
5/02/2016
Hawa Fedex kweli ni wezi, Leo yamenikuta gharama nilizotajiwa kwa mzgo wa kg3 $100, nipo mbioni kuwaachia mzgo wabaki nao.
 
Ili kuweka sawa haya mambo mkuu naomba utaje ni mzigo gani uliotuma ili tujue ni kodi zipi zinapaswa kuwa charged yani hio bidhaa mfano ni nguo au electronic device( kifaa gani husika) maana TRA mizigo hua inakua charged kwa kutumia Invoice yako na mingine kodi yake hutegemea uzito au quantity
 
Ili kuweka sawa haya mambo mkuu naomba utaje ni mzigo gani uliotuma ili tujue ni kodi zipi zinapaswa kuwa charged yani hio bidhaa mfano ni nguo au electronic device( kifaa gani husika) maana TRA mizigo hua inakua charged kwa kutumia Invoice yako na mingine kodi yake hutegemea uzito au quantity
Mfano Mimi ni laptop,. Nimeambiwa agent fee 170elf, nilipowambia Nina agent wangu nipeni doc nikatoe mzigo wanadai doc zinauzwa 88,500, na akasema hapo ni mwanzo tu bado Kodi za tra, sijui Swiss port, tbs nk
 
Mfano Mimi ni laptop,. Nimeambiwa agent fee 170elf, nilipowambia Nina agent wangu nipeni doc nikatoe mzigo wanadai doc zinauzwa 88,500, na akasema hapo ni mwanzo tu bado Kodi za tra, sijui Swiss port, tbs nk
Sasa laptop kama ni mpya inatakiwa ulipie 18% Vat, Customs Processing Fee sikumbuki ni asilimia ngapi ila haizidi 1% na Railway Development levy ambayo ni 0.60% ila kama ni used inaongezeka na excise duty ambayo inakua ni nusu ya bei uliyonunulia, kuhusu kununua documents hio ni standard maana ili upewe hizo document inapaswa ulipie hicho kiasi cha hela ulichotajiwa..ni kweli kuna hela za swissport i.e storage, handling fees etc, na TBS lazima wagonge mhuri wako sasa hio sijajua umeagiza kwa kupitia courier i.e Fedex, USPS au Aramex ila huo ndo utaratibu kwaio ungewe kuzinunua documents na ukampelekea agent wako ambae anakuchaji agancy fees pia, hairihusiwi mtu binafsi clear mzigo mwenyewe sababu hayo ni maswala ya kitaalamu i.e kuna HS Code agent anakua anaiweka hicho kifaa chako cha laptop..kama unaswali lolote unaweza uliza..
 
Back
Top Bottom