Kinyasi
Member
- Nov 22, 2010
- 72
- 31
Ndugu wadau wa Ughaibuni na Bongo,
Ni matumaini yangu mpo salama na mna enjoy spring season hasa kwa wale wenzangu tulio kenye ukanda wa baridi.
Nilikuwa napenda kujua kama kuna mwenye this experience anapotuma mzigo kwenda Dar na kuandikiwa ridiculous tax invoice isiyolingana na thamani ya mzigo? Kuna matukio mawili hivi: Mosi kuna siku nilikuma mzigo una thamani ya $278 na uzito wa 21 pounds, ulipofika Fedex Dar wakadai nitoe Tsh. 50,000/= processing fee na 200,000/= ya kulipa agent afanye clearance ya mzigo airport. Pili kuna mzigo mwingine nimetuma kwenda Dar kwa njia ya Fedex una thamani ya $625 na uzito wa pound 23, Fedex wakanambia upo Customs ya TRA airport, zinahitajika tsh. 50,000/= processing fee ya Fedex na Tsh.470,000/= (Laki 4 na Sabini Elfu) kuutoa mzigo kwenye custom ya TRA airport.
Kinachonishangaza, kuna rafiki yangu nipo nae hapa New York alituma mzigo wake wenye thamani na uzito sawa na scenerio namba 1 kwa Fedex kwenda Morogoro akautoa kwa kulipia Tsh. 30,000/= (Thelasini elfu tu). Ninachojiuliza, Je issue ni Fedex au custom ya TRA au kitu kingine zaidi? Mbona nikituma kwa njia ya USPS mizigo yenye thamani na uzito wa ranges kama nilizozitaja hapo juu na ikifika Posta ya Dar, wanachaji siyo zaidi ya Tsh. 10,000/= (Elfu kumi tu)?
Kingine kinachonishangaza zaidi kuna mzigo mwingine wa thamani ya euro 700 na uzito wa kg 25, niliouagiza hivi karibuni toka Germany kwa njia ya DHL, umefika Dar na ukakombolewa kwa Tsh. 2,800/= (Elfu mbili na mia nane tu).
Ninachojiuliza, je issue ni Fedex au Custom ya TRA airport au something else nisichokijua? Je ni nani yupo sahihi ( kwenye makato ya kutoa mizigo ) kati ya Fedex na TRA aiport kwa upande mmoja na Shirika la Posta na DHL Dar kwa upande mwingine?
Binafsi nahisi kama kuna kitu hakipo sawa hapo kwenye custom ya TRA airport, kuna kama kamchezo kanachezwa kutuibia kwa kutubambikia kodi zisizo na kichwa wala miguu. Kwa mfano sioni sababu ya Fedex na TRA kulazimisha agent alipwe pesa za kuutoa mzigo wakati unaweza kutolewa na mpokeaji kwa kufanya malipo ya kodi kwenye custom za TRA airport bila kumtumia agent.
Natanguliza shukrani kwa wale watakao share experience zao kwenye hii issue.
Kinyasi N Monyi
Rochester, NY.
5/02/2016