FBI waondoka Zanzibar bila polisi kujua

FBI waondoka Zanzibar bila polisi kujua

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,104
Reaction score
34,926
Zanzibar. Askari wa Upelelezi wa Marekani (FBI) waliokuja Zanzibar kusaidia uchunguzi wa kumpata aliyemuua kwa kumpiga risasi, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki wameondoka nchini.
Askari hao waliondoka Zanzibar bila kukamatwa mtu yeyote anayetuhumiwa, licha ya polisi hivi karibuni kutoa mchoro wa mtu anayedaiwa kumuua padri huyo.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema jana kuwa askari hao waliokuja kushirikiana na wenzao wa Tanzania, wamerudi Nairobi na wanaendelea na uchunguzi wao.
"Hawa jamaa wamerudi Nairobi. Lakini, huwezi kuwaamini sana wanaweza kusema wako watatu kumbe wako 100," alisema Kamishna Mussa na kueleza kwamba hakumbuki tarehe waliyoondoka nchini.

FBI waliitwa nchini ili kusaidia uchunguzi wa kuuawa kwa Padri Mushi Februari 17 mwaka huu, wakati anakwenda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Kamishna Mussa alisema kwamba hadi sasa hawajapata mtuhumiwa ambaye wanaweza kumfikisha mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji hayo.
Mussa mara kadhaa amekuwa akisema kwamba "tunakamata, tunahoji na kuachia" na kueleza kuwa, polisi wamepewa majina mbalimbali baada ya kutoa mchoro wenye taswira ya mtu anayedaiwa kumuua Padri Mushi.
Kuuawa kwa Padri Mushi kulikuja baada ya viongozi wengine wa dini, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhil Soraga kumwagiwa tindikali na kupigwa risasi kwa Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki Zanzibar.
Tangu kuuawa kwa Padri Mushi kumekuwa na taarifa za kukamatwa kwa baadhi ya watu wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo, lakini polisi wamekuwa wakikanusha.
Serikali iliahidi kwa njia zozote kuhakikisha inawakamata watuhumiwa, huku Rais Kikwete akiahidi kutumia vyombo vya upelelezi vya ndani hata ikiwezekana vya nje kuwakamatwa wahusika.
Chanzo:Mwananchi

Mkuu MziziMkavu hakuna cha kustaajabisha hapo. Kuna ndege ya kigeni iliingia nchini usiku na kubeba kinyemela wanyama mbali mbali wakiwemo Tembo, Simba, Twiga n.k. hakuna hata aliyestuka polisi na wajeda walikuwa wamechapa usingizi fofofo huku rasilimali za nchi zinaibiwa. Sasa waambie CHADEMA wameandaa maandamano kupinga ufisadi uliokithiri nchini utawaona wanavyojifanya wanaipenda na kuijua kazi yao!!!!!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu BAK Tanzania hakuna Serikali kuna Siri-Kali huko nyumbani.
kp26122012.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MziziMkavu hakuna cha kustaajabisha hapo. Kuna ndege ya kigeni iliingia nchini usiku na kubeba kinyemela wanyama mbali mbali wakiwemo Tembo, Simba, Twiga n.k. hakuna hata aliyestuka polisi na wajeda walikuwa wamechapa usingizi fofofo huku rasilimali za nchi zinaibiwa. Sasa waambie CHADEMA wameandaa maandamano kupinga ufisadi uliokithiri nchini utawaona wanavyojifanya wanaipenda na kuijua kazi yao!!!!!

hiyo ndege haikuingia usiku.walikuwa kia kwa muda wa wiki pale tena ya jeshi.jeshi moja linapoingia kwenye nchi nyingine lazima mkuu wa majeshi na amiri jeshi wawe na taarifa.sasa ilikuwaje tukaambiwa wameiba wanyama wakati wale wanyama walikamatwa kwa kutumia ndege zetu za jeshi? hawakuiba walipewa wanyama na jk
 
Huwezi ukagawa kitu ambacho si chako bila ya ridhaa wa wenye mali. Kufanya hivyo ni WIZI hata ukiwa na cheo kikubwa namna gani.

hiyo ndege haikuingia usiku.walikuwa kia kwa muda wa wiki pale tena ya jeshi.jeshi moja linapoingia kwenye nchi nyingine lazima mkuu wa majeshi na amiri jeshi wawe na taarifa.sasa ilikuwaje tukaambiwa wameiba wanyama wakati wale wanyama walikamatwa kwa kutumia ndege zetu za jeshi? hawakuiba walipewa wanyama na jk
 
Mungu ibariki Tanzania Dumisha Umoja na Amani wake kwa waume na watoto, Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Ibariki Tanzaniax2 Tubariki watoto wa Tanzania..
Amen
 
huwezi ukagawa kitu ambacho si chako bila ya ridhaa wa wenye mali. Kufanya hivyo ni wizi hata ukiwa na cheo kikubwa namna gani.
wale jamaa hawakuja kinyemela kama ulivyosema.raisi alijua,jeshi la wananchi waliusika,polisi walijua,wizara ya maliasili waliusika.kwahiyo sio kama waliuchapa usingizi kusema hawakujua kinachoendelea.walijua.kwahiyo walishilikiana kuiba mali za watanganyika.wote wezi,sio. Waliobeba pekee.waliwindwa kwa kutumia ndege zetu za jeshi,wakasafishwa kupitia bararbara zetu ambazo askali wapo.
 
Zanzibar. Askari wa Upelelezi wa Marekani (FBI) waliokuja Zanzibar kusaidia uchunguzi wa kumpata aliyemuua kwa kumpiga risasi, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki wameondoka nchini.
Askari hao waliondoka Zanzibar bila kukamatwa mtu yeyote anayetuhumiwa, licha ya polisi hivi karibuni kutoa mchoro wa mtu anayedaiwa kumuua padri huyo.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema jana kuwa askari hao waliokuja kushirikiana na wenzao wa Tanzania, wamerudi Nairobi na wanaendelea na uchunguzi wao.
“Hawa jamaa wamerudi Nairobi. Lakini, huwezi kuwaamini sana wanaweza kusema wako watatu kumbe wako 100,” alisema Kamishna Mussa na kueleza kwamba hakumbuki tarehe waliyoondoka nchini.

FBI waliitwa nchini ili kusaidia uchunguzi wa kuuawa kwa Padri Mushi Februari 17 mwaka huu, wakati anakwenda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Kamishna Mussa alisema kwamba hadi sasa hawajapata mtuhumiwa ambaye wanaweza kumfikisha mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji hayo.
Mussa mara kadhaa amekuwa akisema kwamba “tunakamata, tunahoji na kuachia” na kueleza kuwa, polisi wamepewa majina mbalimbali baada ya kutoa mchoro wenye taswira ya mtu anayedaiwa kumuua Padri Mushi.
Kuuawa kwa Padri Mushi kulikuja baada ya viongozi wengine wa dini, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhil Soraga kumwagiwa tindikali na kupigwa risasi kwa Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki Zanzibar.
Tangu kuuawa kwa Padri Mushi kumekuwa na taarifa za kukamatwa kwa baadhi ya watu wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo, lakini polisi wamekuwa wakikanusha.
Serikali iliahidi kwa njia zozote kuhakikisha inawakamata watuhumiwa, huku Rais Kikwete akiahidi kutumia vyombo vya upelelezi vya ndani hata ikiwezekana vya nje kuwakamatwa wahusika.
Chanzo:Mwananchi

Kwa hali ya utendaji kazi wa polisi wetu, naamini hata kama FBI wangeamua kutosema wakati wanakuja kamwe wasingejulikana kuwepo kwao! Kuna wakati hawa polisi wanakuwa kama ile misanamu tunayofunga shambani kutishia ngedere-sura na umbo la mtu ila ni sanamu tuu!
 
Back
Top Bottom