Ushirikiano katika kusaka wahalifu ni jambo la kawaida kwa nchi zote, na kwa wakati wote. Najua, wapo wachache watakaopinga jambo hili, kwa kuwa kwa namna moja au nyingine ama wanahusika direct or indirect, au wana maslahi katika jambo hili. Kuna watu hata watathubutu kukimbia, ingawa tayari wamekwisha chelewa, kwa kuwa mipaka ya ndani na nje ya nchi, imekwisha dhibitiwa. Acha wakamatwe, na mwisho wa siku wajutie madhambi yao, wakati wale waliokuwa wanawadanganya eti wanawapeleka kwenye mafunzo nje ya nchi, watakapo wakana mara tatu.