Fataki na kinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi.

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,094
538
Kuna matangazo nayasikia mara kwa mara kwenye vyombo vya habari ambayo waandaaji wa matangazo hayo wanaamini ni njia mojawapo ya kupeleka ujumbe wa kuwakinga wanawake/wasichana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Moja ya matangazo hayo ni lile ambalo msichana mmoja anajitambulisha kama cheupe wa tanga na lile la dereva wa bajaji kumpitisha fataki kwenye njia ndefu ili achelewe kufika eneo alilokusudia.

Swali ninalojiuliza ni kuwa hivi kweli matangazo haya yanaeleweka kwenye jamii na yanafikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii husika?
 
Back
Top Bottom