Fastjet wamewafuma Watanzania

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Kwa muda sasa, hili Shirika la Ndege la Fastjet limekuwa likilalamikiwa na wengi, lakini hakuna hatua wala mabadiliko yanayoonekana. Kero kuu niliyonayo kwa Fastjet ni kwenye mizigo.

Najua tofauti yao ya uendeshaji ikilinganishwa na mashirika mengine ya ndege. Lakini hili la kukataa kubeba mizigo ya abiria isiyozidi kilo 20 bila kuilipia nadhani ni uonevu uliopitiliza.

Wiki mbili zilizopita nilishuhudia jamaa mmoja pale KIA akiwa na kisu alichonunua mjini Arusha. Alipofika uwanjani wakati wa ku-check in akafuata taratibu zote-za kueleza kuwa ana kisu.

Jambo la ajabu akatakiwa alipe Sh 36,000 kusafirisha kisu alichonunua kwa Sh 10,000. Alibembeleza, lakini hatimaye alikwama. Akasaidiwa na binti mmoja kwa kukiweka kwenye mizigo yake.

Juzi tena, mzee mmoja akiwa na ki-sanduku kidogo akitoka Mwanza kwenda Dar, alilazimika kuacha sanduku na kubeba mkononi blanketi kwa sababu alilazimishwa kulipia Sh 35,000 hicho ki-sanduku, na yeye akawa hana.

Hoja yangu hapa ni hii; hivi kweli hiki kinachofanywa na Fastjet ni sahihi? Haki za abiria katika nchi hii kwa nini hazilindwi na mamlaka husika, hasa TCAA? Hiki kiburi cha Fastjet kinatokana na nini?

Kuna umuhimu wa kulichunguza shirika hili na kuona kama kweli linastahili kuendelea kuwapo. Pengine huu ndio wakati wa kuwa na Shirika letu la ndege la Taifa.

Nawasilisha
 

hivi wewe unaijua hiyo serikali unayoishauri we unadhan wao hawajui hayo? nakushau uhamie kwenye uzi wa lowasa kuchukua form ya uraisi kwa sasa maana huyu ndio pekee mwenye kuweza kuufanyia kazi ushauri wako kikamilifu tafadhali.
 
haya weka pembeni lowasa kwanza.
 
Mbona kama mtoa mada ndo mwenye tatizo la uelewa! Sera yao ya kuhusu mizigo iko wazi mbona? Tujifunze kusafirim smart!
Mzee manyerere tumia kichwa chako vizuri
 
Ndugu yangu hivi unafikiria nchi hii yupo wa kuangalia maslahi ya wasafiri?
 
Mbona kama mtoa mada ndo mwenye tatizo la uelewa! Sera yao ya kuhusu mizigo iko wazi mbona? Tujifunze kusafirim smart!
Mzee manyerere tumia kichwa chako vizuri


Nadhani nimesafiri kwa ndege mara nyingi na kwa pande zote za dunia. Sera yoyote inaendana na mazingira ya sehemu/nchi husika. Kwa mfano, mwekezaji hawezi kuleta sera hapa Tanzania ya kwamba mfanyakazi wake akifiwa jirani, asipeweruhusa kwenda kushiriki msiba. Huko kwao hayo yanatekelezeka, kwani hata msibani wanakwenda kwa mialiko na aina ya mavazi yanayopangwa na wafiwa. Kwa Mwafrika, kama mama anatoka Ukerewe kwenda kumsalimu mwanaye Dar es Salaam, ni kawaida akawa na samaki vibambara (ng'onda) au hata viazi. Hizo ni mila za Kiafrika- kwa mgeni kwenda ugenini akiwa na kiji-zawadi japo kidogo. Fastjet kuwanyima haki hiyo Watanzania/Waafrika ni kuwaonea. Kama tunapinga sera za kishoga, hizi nyingine nazo tunapaswa kuzipinga kwa maslahi ya mila na utamaduni wetu. Huwezi kumzuia mzee kupakia blanketi yake katika kisanduku kisa eti sera yako ya biashara hairuhusu. Huo ndiyo uwekezaji tunaoutaka?
 
subiri lowassa aingie ,unalalamikia majinga ya ccm?????
 
Hizi ni low cost airlines, na huwa zinakuwa na karaha zake.
Popote duniani penye low cost airline inakuwa na huduma ambazo ''hazijatimia kiwango'', na nia yao ni kusafirisha binadamu na sio mizigo. Ukitaka kuingia na kilo zako 20 panda kina Kenya Airways, otherwise fastjet wakiruhusu unachotaka basi jiandae kulipa nauli kubwa!
 

Maneno ni yako mazuri, lakini malengo ya dunia ni kufanana katika hatua zote za kimaisha na kimaendeleo.Si kil kila kilichokwetu afrika kinapaswa kuendelezwa,na si kila cha wazungu kinapaswa kufuatwa. Msingi mkuu wa kufuata kitu ni tija au ufanisi ktk kitu husika.
Ila utamaduni wetu tukiwa safarini si mzuri kabisa hata tukiwa ndani ya daladala, Naamini hata ajali zikitokea madhara huwa makubwa kulingana utaratibu wetu usio na tija tulijizoesha tukiwa safari. YAAAANI MIZIGO UTAFIKIRI TUNAHAMA.

Naomba nisieleweke vibaya, pili jambo hili sidhani kama ni lazima tuliongelee kisiasa,itakuwa ni uvivu wa kufikiri kama tunadhani kila kinachotokea ni matokeo ya kisiasa.
MANENO YANGU SI SHERIA RUKSA KUTOKUYAKUBALI
 
Mkuu, hapa Tanzania sijaona hiyo Low Cost Airline. Juzi tu, TCAA wameiandikia Fastjet wakisema nauli zake zinatofautiana mno kwa wakala mmoja hadi mwingine. Wameacha wahuni wajipangie bei wanazotaka. Booking ya wiki moja kwenda Mwanza kwa mtu mmoja (One Way) ni Sh 217,000. Hapo kuna Low Cost? Ninachoona hapa ni kwamba Tanzania ni shamba la bibi, na bahati mbaya bibi mwenyewe alishafariki dunia! Kila anayetaka kuchuma anakuja kwa staili kama hii ya low cost. Ni wajibu wa watumiaji wa usafiri huu kuhoji haya mambo na kuyapatia jawabu la kudumu.
 
Utamaduni wa kusafiri ni tofauti sana na vile wengi tunavofikiria.
Sio TCAA au sjui TAA ambayo ina-control ivo vitu.
Kufanya booking ya ndege na wale wanaouza tiketi za ndege ni kama vile kufanya gambling.
Wenye ndege daima wanataka kupata faida hata kama wanasema ni budget airline (low-cost).
Mfano Qatar Airways huwezi kubeba zaidi ya kilo 23 kwa bag moja na unaruhusiwa mawili lkn hakuna moja litakaloruhusiwa kuzidi kilo 23 kwa "economy class".
Na mzigo unaoingia nao kwenye ndege (hii ni kwa mashirika yote) mfano huwezi kuingia na lotion au hata colgate inayozidi nadhani kama gram 100 au au lita 0.1. Huu ni utaratibu.
Ukizidisha kilo moja au bag likizidi vipimo mfano kwa Qatar Airways unalizpa nadhani $40 kwa kila kilo moja (sina hakina unaweza ku-confirm hapa Excess Baggage Rates | Qatar Airways).
Nikirudi hapo nyuma kwamba kununua tiketi ya ndege ni kama "gambling" ni ukweli kuwa ukienda kubook tiketi masaa matano mfano kabla ndege haijaondoka ni dhahiri kwamba utalipa hela nyingi sana.
Kwa fastjet ilivo kuwa ni budget watajitahidi kutumia kila namna ya kumaximize profit. Ndio maana kabla hujaanza kulalamika kuwa hawafai lazima ulijue hilo mazingira wanayofanyia kazi.
Lkn upungufu mkubwa ambao nimeona kwa fastjet ni tofauti ya wahudumu.
Mfano mara moja nimesafiri na bag tokea dar kwenda Mwanza sikulipia. Wakati narudi wale wa kule mwanza wakanikomalia kwamba natakiwa kulipia. Hili linatokana na kuwa wafanyakazi wao nadhani hawajaelekezwa vizuri kwenye hilo.
Huyo jamaa mwenye kisu alitaka kuingia nacho kwenye cabin? (Ambako hata wembe hauruhusiwi)

Lkn kingine badala ya kulalamikia kwanini watu wasiende kupanda hizo ndege za mashirika mengine? Mana kwenye usafiri wa ndege pia sidhani kama kuna regulation kwenye tozo la nauli, sababu huduma zinazotolewa ni tofauti.
TIketi ya kawaida kwa mfano ya KLM kwenda USA (East Coast Airports) itakuwa around $ 1500, hiyo umebook walau mwezi mmoja kabla. Lkn Qatar airways unaweza bado ukapata tiketi ya $1500 hata ukibook wiki moja kabla ya kusafiri na kama nafasi zipo hata ndani ya siku kadhaa kabla ya kusafiri. na mashirika haya yote ni 5-Star Airlines. Sasa huwezi anza kulalamika kwamba ooo KLM gharama kubwa inabidi washushe sjui na nini. Kuna vitu vingi sana vinaingia hapo.
Kwa hiyo ni vema ukajiridhisha na taratibu za usafiri huu ambao kwa wengi wetu pengine ni fastjet ilitusaidia tukapata experience ya kusafiri hewani kuliko kabla ya hapo halafu sasa tunataka tusafiri na kuku, na visu na kila kitu. Above all usafiri wa ndege ni kwa wale wanaoweza kumudu gharama na wenye haraka au emergencies ambao swala lao lla kwanza ni kufika wanakotaka kufika na gharama linakuwa swala la pili.
Acheni watu wafanye biashara zao.
 
Bado Fastjet ni ndege rahisi mno kulinganisha na zingine. Huwezi kusafiri kwenda Entebbe kwa laki 1 au Johannesburg kwa laki 2 ila kwa Fastjet tu.
Tatizo lililopo ni kuwa hatusomi instructions ikiwemo ya kubeba mizigo. Either, hatuzingatii masharti hata tukiyajua. Unabebaje zaidi ya kilo zinazotakiwa 20 kwa mfano? Unadhani hilo ni bus? Lazima waweke restrictions ili waweze ku operate.
Tatizo lao ninaloona ni bei zao, kuna wakati ni ghali mno especially ukitaka kusafiri hapo kwa hapo. Book mapema utaona faida yake. Ni ndege gani inaweza kukupeleka Kilimanjaro au Mwanza kwa Tshs 120,000/= return lets say in the next four weeks? Angalia website zao sasa hivi utakuta hiyo kitu. Lets be fair, inasaidia sana. Ila wana vijimambo vidogo vidogo wanatakiwa kurekebisha.
 
Mkuu kama unaona hujatendewa haki si Uache kupanda kwani umelazimishwa??kutoka Arusha kuja Dar kuna Ngorika,Sai baba,Dar Express nk mabasi yako kibao si upande hayo ambayo nauli ni chini na bado unaweza kusafiri na mzigo wako hata kilo100,kwan ni lazima upande FastJet??jikune mkono unapofika usilazimishe usiyoyaweza waachie wenyewe!!
 
Dawa ni kuwepo mashirika mengi ya aina ya ''Fastjet'' (yaani budget/low cost airlines) mengi na itapelekea ma-travel agent kuzidi kupunguza bei ya tiketi.

Hivyo siyo haki kuilaumu Fastjet maana wao ni low cost airline na wao ili kupunguza gharama za uendeshaji wa shirika mbinu moja ni kutumia mawakala wa tiketi na FastJet kuwa na wafanyakazi wachache ili nauli kwa abiria kuwa ya nafuu kama wadau wengine walivyoainisha ktk michango yao ya thread hii. Air Tanzania hawazingatii haya.

Mbinu nyingine ya low cost airline ni kujaza abiria wengi kadri iwezekanavyo na hii maana yake ni mizigo michache au kiwango cha kilo za bure za mizigo kwa abiria kuwa kidogo na hivyo gharama ya tiketi kwa abiria kuwa nafuu.

Kuna mengi FastJet/low cost airline hufanya kama kuhakikisha ndege inakuwa angani muda mwingi ikifaya flights kibao mfano wa mabasi ya daladala yanavyokula vichwa vya abiria ku-maximize vipato kila siku(ktk saa 24) na nauli kuwa nafuu. Kupakia mizigo mingi na kuishusha hupoteza muda na gharama pia ni kubwa kuwalipa wakala (SwissPort).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…