Fast jet yaahirisha ndege zaidi ya mara tatu

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
821
1,338
IMG_20171024_053430.jpg
Serikali iingilie kati hii hali,wananchi wake wanapata shida nafikiri waziri aseme chochote juu ya hawa jamaa wanaoendesha ndege kijanja janja,niko airport sasa hivi na nimekutana na wenzangu waloahirishiwa ndege zaidi ya mara tatu na ya kwangu ikiwa imeahirishwa huku wote tukitoa macho bila kujua hatma yetu......na mamlaka husika za airport zipo na zinajua.Tangu saa kumi usiku watu wamekuja airport hapa Ofisi zao zimefungwa hakuna mtu wa kutoa maelezo au kusaidia abiria waliokata hizi tiketi zao,lakini wao unapochelewa ndege yao hua wakali na hawataki maelezo yoyote !! MAMLAKA HUSIKA LEO TUNAOMBA TUSIKIE HATUA MNAYOCHUKUA JUU YA HAWA FASTJET.....na hawajazuia watu kufanya booking system zao zipo na zinaendelea kupokea booking huku wao wakiendelea ku cancel
 
Pole sana haya mambo yanahitajika sana! Natumahi utapata ufumbuzi na kuweza kuwahi kwenye shughuli zako, utatujulisha kwa lolote mkuu. Safari njema.
 
Kuna siku ilishawahi kunikuta hili selekaseleka
Na hivi walishaga wahi kunitosa ati kisa kitambulisho,,kila nikiwafahamisha na kuwa bembeleza ndio nachochea kuni kwenye moto,,,
Siku hio sasa na mimi
Ilikuta hio
Seleka nililala hoteli 3stars hotel siku2 msosi nlikula
Kama kesho nakufa vile,,,
Beer sasa hadi opener ilipinda
Hawana ham namimi hao Fast Jet kila nkifungua Beer nawaita‘Hhheeeeeyyy SLOWJET njoo ufungue BEER”
 
siku ikinikuta hii wataisoma namba wana bahati nimepanda mara tano tu enzi hizo wako vizuri saizi niko zangu na wazalendo kwenye bombedier
 
Kuna uzi mmoja wa mwanasheria mmoja alikuwa na mtafaruku na hao fast jet na alilipwa kias fulan cha hela baada ya kuwapeleka mahakaman sikumbuk vzur, so kama wanaweza wakawafungulie case tu moja matata ya kulipa fidia watashika adabu

NB: Nisaidie kupata namba ya mmoja wa hao wadada hao wawili hapo kwenye picha
 
Kuna uzi mmoja wa mwanasheria mmoja alikuwa na mtafaruku na hao fast jet na alilipwa kias fulan cha hela baada ya kuwapeleka mahakaman sikumbuk vzur, so kama wanaweza wakawafungulie case tu moja matata ya kulipa fidia watashika adabu
jamaa alikula milioni 30 kulainiiii
 
Back
Top Bottom