Fashisti Nduli.............. apigwe ateketezwe kabisa!

Fashisti Nduli.............. apigwe ateketezwe kabisa!

kiroba

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
324
Reaction score
115
Ndugu zangu wana wa Tanzania, ninawaomba niwaambie kitu kimoja kikubwa sana na muhimu sana kwa uhai na amani ya taifa letu.

Nia ya kumpiga tunayo, sababu ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao pia. Huyu si mwingine bali ni fashisti nduli Mwigulu Lameck Nchemba. Hivi kama unafikia kiwango cha kutesa na kutoa uhai wa mwanadamu mwenzako achilia mbali kuwa ni mtanzania mwenzako. Mtu kama huyu ni sawa na fashisti nduli tuliyeungana na majeshi yetu kumpiga na hatimaye tukamshinda. Kwa adui huyu fashisti nduli wa sasa ni ngumu sana kumshinda kirahisi kwa kuwa kwa sasa ni wananchi tu ndio wameungana lakini majeshi yetu yapo upande wa huyu fashisti nduli. Hapa inahitajika nguvu na ujasiri wa hali ya juu sana kumshinda huyu fashisti nduli. Na kikubwa kuliko vyote ni sala na maombi kwa bwana mungu wetu ili atupe ujasiri na hekima za kumshinda huyu fashisti nduli.

Baada ya kumteketeza nduli Idd Amini, niliamini sasa Tanzania yetu ni salama kabisa kwani yule mpuuzi na mwenye roho ya ukatili kwa mwanadamu tayari ametokomezwa kabisa. Kumbe alikuwepo bado mfuasi wake ila tu tulijidanganya kuwa mfuasi huyu ni mwenzetu hawezi kutudhuru. Sasa anatudhuru tena kwa kiwango kikubwa sana. Huyu fashisti nduli wa sasa ni ngumu sana kupambana naye kwa kuwa vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama ameshaviteka na vinamtumikia yeye. Sasa hivi tumekuwa kama yatima hatuna mtetezi kabisa kwani ni sisi kama raia tukipambana na yeye akiwa na msaada wa vyombo vyote muhimu kwa ulinzi na usalama wa taifa letu.

Vijana kwa wazee na pia wake kwa waume sasa wakati umefika wa kujilinda na huyu fashisti nduli kwani anatumaliza kabisa na pia analiacha taifa letu likiwa vipande na likiwa halina tena amani. Najua kuna baadhi ya maofisa wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama walio wema na wenye mapenzi ya nchi yao lakini hawana uwezo wa kufanya lolote kwa kunusuru wananchi na huyu nduli. Wamefichwa kwenye kichaka cha serikali ya chama tawala ili watumike kukandamiza haki za raia. Hawo ndio maofisa wachache ambao kwa namna moja au nyingine tutakuwa nao pamoja katika mapambano na huyu nduli bali wao kwa heshima na utiifu kwa taifa lao watakuwa upande wa wananchi. Mungu wape mioyo ya ujasiri hawa maofisa wetu na pia uwalinde kwani kazi hii kwao ni hatari sana na inaweza kugharimu hata uhai wa maisha yao.

Wananchi pia hawana budi kuchukua tahadhari kwani vita hii ni vita kali sana kuliko ile ya kumtoa nduli Idd Amini kwani hapa wananchi hawana mlinzi wa kuwalinda wao na mali zao. Mlinzi mkuu tayari yupo upande wa nduli akimsaidia. Kama tulivyofundishwa tukiwa jKT kila mtu anapaswa kutambua ana wajibu wa kuilinda na kuitetea nchi yake. Tunapokuwa katika mikusanyiko basi kila mtu awajibike na ulinzi ili kuhakikisha hali inakuwa shwari kipindi chote cha mkusanyiko. Pia kwa wale maofisa wachache waliobaki watiifu kwa Tanzania yao basi wasisite kutoa taarifa za kiitelejensia kwa wananchi ili wachukue tahadhari na kujilinda na mashambulizi yatakayofanywa na huyu fashisti nduli.

Mwisho namaliza kwa kusema historia itamkumbuka na haitasahau kwa ukatili ulofanywa na huhyu Nduli Mwigulu Lameck Nchemba. Vizazi vyetu vitamsoma katika vitabu vya historia kuwa ni mtu hatari na mkatili aliyepata kutokea hapa Tanzania kwa kutekeleza mauaji ya ndugu zao. Kweli atalaaniwa huyu Nduli kwa haya mauaji anayofanya. Ipo siku atadhalilika kama wengi wanaotekeleza vitendo hivi wanapofika mwisho wao. Kama taifa tufunge na tusali ili kumuombea maisha mafupi Nduli huyu kwani atatumaliza na kuichafua nchi yetu iliyokuwa na amani na utulivu. Ushauri wangu kwa wanananchi wenzangu ni kuwa ifikapo siku ya tarehe 1/7/2013 tufunge kwa siku saba na siku ya nane tuende kwenye nyumba za ibada tukasali na hapo na hakika chochote tutakachokiomba basi mwenyezi mungu atasikia duwa zetu atatunusuru na huyu Nduli. Mungu ibariki Tanzania.
 
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
 
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.

Na je ni kwa nini mtu huyu atajwe kwenye kila mauaji? Mkuu hapa hatufanyi siasa bali tunalia damu za ndugu zetu. Tuache mambo ya siasa hata kwenye uhai wa mwanadamu. Nasikitika sana kuona baadhi ya watu wakitanguliza siasa hata kwenye uhai wa mwanadamu mwenzao. Iweje utoe uhai wa mwanadamu mwenzako kwa kutaka upate mvuto wa kisiasa?
 
mvuta bangi anayeweza kutukana kwenye hansard ni wapi ambapo hatafanya uuaji?Baba yao akishaachia nchi wengine watajifia kwa kihoro kabla hata kisasi hakijawafikia.Kama WATESAJI WA WAAFRIKA WAKATI WA MAU MAU wameshatubu hadharani,haidhuru mafao waliyosema watalipa ni kiduchu ,2015 si itakuwa issue?
 
mvuta bangi anayeweza kutukana kwenye hansard ni wapi ambapo hatafanya uuaji?Baba yao akishaachia nchi wengine watajifia kwa kihoro kabla hata kisasi hakijawafikia.Kama WATESAJI WA WAAFRIKA WAKATI WA MAU MAU wameshatubu hadharani,haidhuru mafao waliyosema watalipa ni kiduchu ,2015 si itakuwa issue?

Mkuu inatia sana simanzi kuona mtu akitekeleza mateso na mauaji kwa watanzania wenzake. Ni kitu gani hasa chenye thamani kuliko uhai wa mwanadamu hadi unakuwa mnyama kiasi hiki? Kwa kweli kama taifa hapa tulipofika ni kubaya sana tuchukue hatua.
 
Back
Top Bottom