Farid Mussa apaa safari kwenda Hispania

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Posted by: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE Posted date: 4/16/2016 08:59:00 AM / comment : 0




Kiungo wa Azam FC, Farid Mussa (kushoto) akiwa na mmoja wa viongozi wa timu, Abdulkarim Amin ''Popat' (kulia) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam Alfajiri ya leo wakati wa safari ya kwenda Tunisia ambako katikati ya wiki ijayo klabu yake itamenyana na wenyeji, Esperance katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika. Farid ameondoka mapema kabla ya wenzake wanaoondoka kesho kwa sababu anakwenda kushugulikia mipangop ya safari ya kwenda Hispania kwa majaribio

Farid (kushoto) akiwa Uwanja wa Ndege wa Istanbul, Uturuki kusubiri kuunganisha ndege ya Tunisia
 
Nilisikia anaenda Ubelgiji na Himid Mao.
Kila la kheri Fareed,hata ukipata timu ya daraja ka 3 wewe cheza tu.
 
uache zinaa na uzingatie lishe na kama ulikua unatumia ule moshi wa Haruna wacha sasa
 
ila najiuliza alikua hazina siku ya mechi na waarabu sasa kuondoka kwake huenda ikawa pigo
 
...dogo namkubali;huwa ana kipaji sana cha kupandisha timu!
 
Ila tuna safari ndefu! wakati sisi tunamtegemea Samata tu wenzetu kama Ivory Coast, Nigeria, DRC, na kwingineko wamejaza hazina ya maproo! Nenda kijana ipo siku na sisi tutakua tunajivunia maproo wetu ughaibuni.
 
Wakati fulani tuliwahi kucheza mechi ya kirafiki
kama taifa (Taifa Stars) na tulicheza na taifa
kubwa katika soka Duniani, Brazil wakati ule
tuliambiwa Tanzania ni nchi ya TATU
ulimwenguni kwa kuwa na vipaji halisi vya soka
(watu wanazaliwa na vipaji hivyo hawafundishwi
popote) katika orodha ile ipo Brazil,Nigeria &
Tanzania.... sijui kama ni kweli.!!
Tafakari yangu inanifanya niamini katika hilo toka
kizazi cha akina Kibadeni,Tenga,Mkwasa,Manara
njoo katika zama za akina Mwameja,Lunyami
la,Mohamed Hussein,Amlima,Kenny Mkapa je
kuhusu akina Ali Mayai,Pawasa na wengineo??
inawezekana kweli si ndiyo?? Ndiyo sisi tuna
vipaji vingi sanaaaaa...!!
Nenda Songea,Mwanza,Mtwara,Lindi,Musoma
sijui wapi utawakuta watu wamejariliwa kweli
kweli, lakini nini kinatuangusha? Mfumo?
Uongozi,hulka yetu ya Simba na Yanga? malezi?
au?? inasikitisha sana kuona mpaka sasa hatuna
wachezaji walau wa5 wanaocheza nje ya nchi,
ndiyo inauma sanaaaa..!!
Ujio wa klabu ya Azam nadhani umeongeza wigo
wa kuwaona vijana wengi wenye vipaji, panapo
majaliwa,kijana Farid anapanda ndege kuelekea
Hispania miongoni mwa nchi zilizo na ligi bora na
maendeleo ya kweli katika ulimwengu wa soka,
tumuombe afanikiwe tuwe na wachezaji wengi
wanaocheza nje ambao wataleta uzoefu katika
timu yetu ya Taifa,Taifa Stars, ndiyo tufanye
hivyo kwa faida ya maendeleo ya nchi yetu
kumbe tufanyaje??
Iko hivi kufanya vizuri kwa akina
Samata,Ulimwengu,Ngassa na sasa Farid sijui
ingekuwaje kama Haruna Moshi "Boban" kama
angeendelea kuwepo katika soka la Ulaya uwepo
wao kule utafungua milango kwa vijana wengi
ambao sasa wametambua kuwa soka ni ajira,
ndiyo ajira za maofisini siku hizi hakuna,kwa nini
wasitumie vipaji vyao?? huu ndiyo wakati wao.
Kama vipaji tunavyo tena vingi vya "kumwaga"
nini tunasubiri?? kwanza vyama vya michezo
hasa vinavyosimamia soka waelewe kuwa sasa
soka ni ajira tosha wawepo watu wa kweli wa
mpira siyo "wapiga dili" ieleweke kuwa upigaji
wao dili unaua soka letu, tupate mawakala wengi
na wa" ukweli" ambao watafungua milango ya
vijana wengi ambao wametapakaa kila kona ya
nchi hii makocha waendee huko vijijini vipaji vipo
vingi nani alikiwa anamjua yule dogo wa Yanga
Godfrey Mwashiuya?? bhaaa! hao wapo wengi
nawaambia nendeni huko msikalie tuu hapo
Karume mnapigwa na viyoyozi..cheee!!
Kuna kocha mmoja alikuwa wa Kameruni,yule
bwana mkubwa alifanya mashindano ya nchi
nzima tena vijijini huko akawaibua watu kama
akina Njitap,Kala Nkongo yule beki kisiki na
wengine wengi ambao wakapata kuonekana na
vilabu vya Kameruni mbona hakukaa pale Younde
kupiga mvinyo?? Watumieni wachezaji wa zamani
waliotapakaa kote nchini kuwa "maskauti" wa
vipaji vinavyoishia kunywa gongo na pombe za
kienyeji huko vijijini kwa wakazi wa Mtwara
mnamkumbuka jamaa mmoja alikuwa anaitwa
Mussa Kichawi?? alikuwa anakaa kule Magomeni
yupo wapi?? viongozi wa soka msaikae
maofisini.....!!
Mengi ningeandika kuhusu nafasi na kupotea kwa
vipaji vyetu vingi nichelee kusema nenda
Farid,kafanye kweli kwani hayo ndiyo maisha
yako,Mungu amekupa kipaji,kitumie, kipaji mtaji
Mungu akuongoze katika safari yako ya majaribio
Hispania tena nasikia unaenda La liga,si ndiyo
kule yupo Messi,C7,Suarez,Neymar na yule kocha
mwehu mwenye midadi? Simeone?? aaaah
kafanye kweli bwana nafasi ndiyo hii haiji mara
mbili...!!
Kila la heri Farid miongoni mwa vipaji vya kweli
vya soka vilivyochomoza miaka ya karibuni hapa
nchini.
 
mkolaji mpaka ccm waondoke madarakani ndio nchi hii itafanikiwa kimpira ,eti mwehu hatari simeone huyu alikuwa beki mpambanaji kama masatu mimi nampenda na ile staili yake ya kuhamasisha yaani hakaichini mwanzo mwisho sasa hivi anakiduku chezea
 
Umezungumzia khabari ya Claude leroy alikuwa bushsweken huko kakuta watu wanapiga ndiki kavutiwa na jamaa mmoja kipande cha mtu kamuuliza vp kuhusu soka jamaa akamjibu huwa tukitoka penye mashamba yetu ya viazi basi huja na kuburudishana hapa ila sio kazi yangu mpira kocha katoa nauli kesho njoo younde huyo jamaa ndie Raymond kalla akacheza na world cup na kufunga goli baaden kuna timu nadhani Russia ilimchukua tatizo umri ulikuwa umemtupa mkono.
So vipaji vingi vinapotea kwa kutokutunzwa hakuna programme nzuri mashindano kama copa Coca Cola na uhai hayana faida zaidi ya kukutana ila kama kila mwaka wangekuwa wanachukua vijana na kuwatunza mahala pamoja ndani ya miaka 3 matunda yangeonekana.
Kuna umuhimu wa kuwa na watu kama said salim bakhresa kama kumi hivi tunaweza songa mbele hizi yanga na simba zibaki kuwa timu za mioyoni kwetu tu basi vinginevyo zibadilike wana mtaji mkubwa sana wa wanachama na wapenzi tatizo viongozi makajanja.
Mtu leo nenda bush unakuta katia nyuzi ya man u au Chelsea kama sio real madrid why isiwe uzi wa jangwani au msimbazi?wapenzi wanataka raha na si kusoma timu zina migogoro isiyo kwisha.
 
Title yako na maelezo hujamtendea haki Farid uloyemfungulia uzi, umepiga porojo nyingi sana bila hata kutuambia anaenda lini, ni trial au na je mpaka sasa yuko wapi na chanzo chako cha habari ni nini!
Umeileta habari hii kijeri muro jeri muro hivi.
 
Back
Top Bottom