Farhan Kihamu amchana vikali mchezaji wa yanga Albert Kangwanda

Farhan Kihamu amchana vikali mchezaji wa yanga Albert Kangwanda

kibaigwa finest

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2026
Posts
225
Reaction score
256
Mtangazaji wa clouds amesema "Utakuwa hujui mpira kutokiri kuwa Albert anajua sana mpira ila utakuwa Mjinga kutokubali kuwa Jamaa ana dharau na mpira wenyewe yaani ni kama haheshimu thamani ya Jezi aliyovaa, anacheza kama yupo Club, anacheza kama hataki na anacheza kama kalazimishwa licha ya kipaji.

Bahati nzuri kwake amekuja Yanga nyakati ambazo Mashabiki sio wale ‘Vichaa’ wa mpira, amekuja nyakati ambazo Watu wapo bize na simu wanatazama Uwanjani goli likifungwa ila Jamaa ana miyeyusho sana Uwanjani."

anaandika Farhan M Kihamu
 
Waache uchambuzi maandazi, hao wanaojiita wachambuzi wana elimu gani ya mpira?
 
Ni mchezaji mzuri Yanga wamvumilie. Lakini viongozi wa Yanga nao wanajukumu la kuzungumza na mchezaji ili kujua anapitia masaibu gani. Haiwezekani jamaa wakati anafika bongo alikuwa anacheza vizuri sana lakini ghfla tu kawa mchezaji wa kawaida.
 
Yupo sahihi kabisaa. Kangwanda anacheza kama hana ndoto yoyote, hakamii wala nini. Mpaka tunahisi labda kuna ka mgomo baridi. Hana uchu hata kidogo.
 
Back
Top Bottom