Fao la kujitoa PPF

Fao la kujitoa PPF

Ayunta

Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
7
Reaction score
0
WAKUU

SALAM. Naomba mwenye ufahamu anijulishe je inachukua muda gani kwa mtu aliyeacha kazi kupata fao la kujitoa PPF baada ya kusubmit documents zote zinazohusika ofisini kwao?

asanteni sana.
 
ndani ya mwezi kama document zote ziko clear unatakiwa uchukue chako na so far sijackia mtu amepata usumbufu wowote!
 
PPF sijui ila naskia wako Mamkini kuliko NSSF. NSSF wao wanadai mwezi mmoja ila practically ni meizi 3, mwezi mmoja halali(process imekamilika) na miezi 2 ya ziada ya kuzungushwa ili utoe ganji. mbinu zenyewe ni hizi: Utambiwa kadi yako haisomi, computa haitambui alama za vidole, mtoa cheki leo hayupo njoo kesho, jina lako haliendani na majina kwenye kitambulisho cha kupigia kura, hivyo uanze upya.....nk. Note: Kila mtu anataka umpe ganji. na hapa NSSF mwanza kuna driver anaitwa Machumu anapenda kuvaa suti, miwani na anajua kutambua wenye shida....naye atakupeleka kwa watu wa level yake(makarani) nao watakula kidogo, mtoa cheki naye kidogo.Generally kama haupo makini na ni mwepesi mwanamke utatoa kitumbua na mwanaume kwa wastani utapoteza around 25% of your total pension
 
Mmhh nssf me mbona nilivyoambiwa mwezi na ulikua mwez kweli nikavuta changu
 
NSSF ni mwezi but kwa PPF nasikia wapo faster than nssf
 
NSSF ni mwezi but kwa PPF nasikia wapo faster than nssf
Lakn NSSF wanatoa package kubwa zaidi kuliko PPF, niliwahi kusikia maprofesa (PPF) wakilalamika kuzidiwa pension na masekretari wao (NSSF), ingawa mshahara na walikuwa wanawazidi.
 
Tanzania ndo nchi pekee duniani inayotoa fao la kujitoa. Nchi zingine ukijitoa unaambulia patupu..
 
Hivi LAPF nao vipi maana me nategemea kuchukua mshiko mwez huu..walinambia mwezi ss keshokutwa ndo mwez sijui wataweka hela...au ndo walee
 
mimi nilikamilisha kila kitu...nikapeleka fomu PPF since mwezi wa 10 mwaka jana hadi leo ninazungushwa tu, wanasema kuwa cwez kujitoa bali wanaweza kutransfer hizo hela zangu NSSF ambako nipo sasa kwa mwajiri mpya...Mwajiri wa zamani (TBL) nilikuwa nachangia kupitia PPF. Cjui kama inawezekana kuhamisha hela kutoka PPF kwenda NSSF maana najua ni mifuko miwili tofauti na kila mfuko una formula zake.
 
Kwa ufupi umedanganywa, hakuna kitu kama hicho, zamani ilikua hivi, kama unafanya kazi kwenye mashirika ya umma kama NSSF wenyewe, PPF, Tanesco, Bandari n.k, uliwajibika kua member wa PPF, NSSF/NPF ilikua ina deal na wafanyakazi wa sekta binafsi tu, kuanzia mwaka 2003/4 hakuna kitu kama hicho, una join mfuko unaoupenda mwenyewe, kama umeacha kazi kwa mwajiri A na umepata kazi kwa Mwajiri B then una option ya aidha kuendeleza michango yako au kuchukua chako na kuanza upya, hapa sasa wadau ndio hua tunahama na mfuko kabisa. Binafsi nimeisha kua memba wa hii mifuko 2 kwa nyakati tofauti but the truth is NSSF ni wasumbufu sana, wanapenda rushwa hao balaa, kwa kumalizia, nadhani wanataka utoe chochote hapo, hakuna kingine.
 
mimi nilikamilisha kila kitu...nikapeleka fomu PPF since mwezi wa 10 mwaka jana hadi leo ninazungushwa tu, wanasema kuwa cwez kujitoa bali wanaweza kutransfer hizo hela zangu NSSF ambako nipo sasa kwa mwajiri mpya...Mwajiri wa zamani (TBL) nilikuwa nachangia kupitia PPF. Cjui kama inawezekana kuhamisha hela kutoka PPF kwenda NSSF maana najua ni mifuko miwili tofauti na kila mfuko una formula zake.
Tatizo ni kwamba ulijichanganya katika kutoa maelezo.PPF ukishakamilisha kila kitu mara nyingi unapelekwa kwa maofisa wa 'marketing' ambao wanakushawishi kutojitoa kwani unaweza kupata kazi tena ukaendeleza michango yako n.k lakini ulitakiwa uwaambie kuwa unajitoa kwani 'hutegemei kuajiriwa tena' na siyo kuwa umepata kazi kwingine.Kwa taratibu za sasa za SSRA unaweza kuhamisha michango (transferability).
 
Back
Top Bottom