CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 853
Kwa muda mrefu, kumekuwepo zuio la kujitoa kwenye mifuko ya jamii maarufu kama 'fao la kujitoa'.
Sababu zimekuwa kwamba, ni utekelezaji wa sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii na ile ya SSRA.
Hapo mwanzo, kabla ya tarehe 11-Mei-2016, ilikuwa mtu akiacha kazi au kupoteza ajira, basi alikuwa anaenda kujitoa kwa maana ya kuchukua michango yake yote.
Zuio la kujitoa limekuwa mjadala mpana na ambao haujaisha hadi hivi sasa. Nimekuwa nikifuatilia hili kwa kuwa mimi pia ni mhanga mkubwa. Na taarifa zilizopo hivi sasa ni kuwa, serikali imekuja na 'fao la kukosa ajira' kama mbadala wa 'fao la kujitoa'.
Taarifa hiyo, haijaeleza kwa kina mbadala huo wa 'fao la kukosa ajira' ukoje. Wapo wanaodai kuwa, mtu aliyepoteza ajira atalipwa 30% ya mshahara wake kwa miezi 6, lakini hakuna conclusion ya baada ya miezi sita kuisha bila mtu kuwa na ajira au kupata ajira itakuaje.
Maoni yangu na maoni ya wengi kuhusu hili suala ni kurejeshwa fao la kujitoa kwa sababu zifuatazo.
1. Ajira (hasa sekta binafsi) si za uhakika na hazina security. Leo ni mfanyakazi kesho umemkosea bosi kwa kupiga chafya tu mbele yake basi ajira hauna.
2. Mishahara kwenye sekta binafsi, ukweli ni kwamba ni midogo mno. Ni midogo kiasi kwamba hakuna mtu mzima anaweza kuweka akiba kwa mishahara hiyo. Kwa mazingira kama haya, ikitokea mtu kapoteza ajira kutokana na mazingira yaliyopo, ukweli ni kwamba mtu huyo aliyepoteza ajira atakuwa na wakati mgumu. Hatoweza kuanzisha hata biashara ya mtaji wa laki moja tu.
Angalizo: Siku zote sheria (kwa uelewa wangu mdogo) huanzishwa kama makubaliano ya jamii yote kwa ujumla. Sheria huanzishwa ili kukidhi mahitaji ya jamii husika, kwa maana hii ni lazima kuwepo makubaliano kwa wahusika ama wadau wakuu. Sheria kuanzishwa bila makubaliano kwa wahusika wakuu ni utengenezaji wa mgogoro.
Kila nikisoma maoni kuhusu hili suala la mafao kupitia social medium, nagundua jambo moja kuu; kwamba wahusika wakuu au wadau wakuu ambao ni wafanyakazi na wanachama wa mifuko ya jamii hawakuhusishwa, huo ndiyo ukweli--hata mimi ninayeandika haya sijahusishwa. Nachukua nafasi hii kusema kuwa, suala la fao la kujitoa lazima lizingatiwe kwa umuhimu wake, wadau wakuu wahusishwe na kusikilizwa na si kama ilivyo hivi kwa hivi sasa.
Wenu katika uhuru wa kutoa maoni.