Fao la kujitoa lipo---LAPF

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
Nchi ina mambo ya ajabu hii!

Watu wa LAPF wanatoa fao la kujitoa, wengine akina PPF wanazuia pesa za watu. Vyombo vyote hivi viko chini ya SSRA, chombo kinachosimamia na kudhibiti mifuko hii. Jambo la ajabu, na kushangaza ni serikali kupitia haohao SSRA, wanazuia pesa za watu kupitia PPF na NSSF. Hivi hii serikali wafanyakazi tumeikosea nini? Hawa wanaojiita vyama vya wafanyakazi na shirikisho la vyama hivyo, wanafanya nini, why are they standing a side and look while we suffer from this issue? Tuseme nini wafanyakazi ili tueleweke, au tufanye nini ili tueleweke na ionekane kweli tunaumia? Hivi kijana wa miaka 30 ama 20 unapomwambia asubiri hadi afikishe miaka 55 au 60 ndipo aje kuchukua pesa zake, unakuwa na nia gani naye? Kazi hazina uhakika, leo upo job kesho jobless kutokana na uhuni wa waajiri sekta binafsi. Aya nimepoteza ajira, halafu unanambia nisubiri mpaka nizeeke ndipo nije kuchukua pesa zangu. Jamani, hivi kweli haya huwa wanazungumza wakiwa wana kileo kichwani au ikoje. Maana si kawaida!

frank mayige

Member
Jan 5, 2013
60
95
For my thinking capb na waajiri wanatakiwa kutupa mishahara ya ya miaka iyo in adv.
nikweli jamani mimi pia ni muhanga wa hilo jambo tajwa hapo juu nimefanya kazi miaka 3 kampuni fulani kwanza ulipaji wa mishahara nilikuwa shida sana pia michango haiendi kwa wakati, mpaka sasa michango iliyo pelekwa ni 720,000/ out of 4,500,000, ukiwauliza PPF wanasema mwajiri kapelekwa mahakamani tangu 2012 mpaka sasa hakuna kitu kabisaaa sasa mpaka nifikishe miaka 55 au 60 sina kazi mtoto wa masikini inakuwaje,
 
Namuomba Rais wetu mpendwa JPM aliangalie hili kwa upana wake ili sisi watoto wa wakulima tupate haki zetu maana nimeshazungushwa sana na hyo kampuni mpaka wananiambia nenda kokote, sasa najiuliza sisi watu wa hali ya chini tukimbilie wapi?
 
BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,157
2,000
This is serious
hivi nani alisikia huyo anajiita mpango alivokua anasema mafanikio makubwa yaliyoletwa ndan ya mwaka.1
 
nG'aMBu

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
1,237
2,000
Daaah umenikumbusha machungu sana nina 15 mil na mkataba umeisha mwaka huu, ningejichukulia hiyo pesa niingie porini ila nashukuru Mungu kampuni imenipa tena miaka 3 mpk 2019 sijui fao litakuwepo ni NSSF
 
frank mayige

Member
Jan 5, 2013
60
95
Namuomba Rais wetu mpendwa JPM aliangalie hili kwa upana wake ili sisi watoto wa wakulima tupate haki zetu maana nimeshazungushwa sana na hyo kampuni mpaka wananiambia nenda kokote, sasa najiuliza sisi watu wa hali ya chini tukimbilie wapi?
leo hii tuna nyanyasika na makampuni binafsi mishara shida kupata kufukuzwa kila kukicha tunafamilia nyuma zinatutegemea, sasa hata kidogo tunacho kipata tunaambiwa kusubiri mpaka miaka 55 jaman, serikali ituangalie kwa hili.
 
Hivi muhusika mkuu wa mimi kurepot issue yangu ya michango kwanza mpaka leo haijapelekwa niipeleke wapi?
 
CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
Namuomba Rais wetu mpendwa JPM aliangalie hili kwa upana wake ili sisi watoto wa wakulima tupate haki zetu maana nimeshazungushwa sana na hyo kampuni mpaka wananiambia nenda kokote, sasa najiuliza sisi watu wa hali ya chini tukimbilie wapi?
Frank haya mambo ya kuomba wakati haki ni yako, huwa mabaya sana, Unachotakiwa kufanya ni KUDAI, kwa sababu ile ni haki yako. Ni hela yako ile. Wakati unafanya kazi hakuna aliyekusaidia, kodi ulilipa. Sasa kama hata kodi ulilipa, kisha anakuja mtu anazuia pesa zako na wewe unaanza kumuomba akupe badala ya kudai, utaishia kustaajabu tu. Tufungane mkanda, mimi wewe, na yule na tuidai haki yetu.
 
uniquelady

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
422
250
Mbona Mimi nimeenda NSSF juzi hapa ila kwa bahati mbaya nilikuwa sijafikisha miezi sita toka niache Nazi wakasema ikifika tu nipeleke barua ya kuacha kazi nijaze form ya madai ya FAO la kujitoa ,imekaaje hii wadau
 
CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
652
1,000
Mbona Mimi nimeenda NSSF juzi hapa ila kwa bahati mbaya nilikuwa sijafikisha miezi sita toka niache Nazi wakasema ikifika tu nipeleke barua ya kuacha kazi nijaze form ya madai ya FAO la kujitoa ,imekaaje hii wadau
wanakudanganya, na usithubutu kuacha kazi mwenyewe, utakuwa umeliwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom