Fanya Yafuatayo Ili Kuhamia Mtandao Mwingine Bila Kubadilisha Namba

johnmlay

Senior Member
Mar 27, 2012
150
56
Mobile Number Portability (MNP)
Ni Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe
01 Machi 2017.

Huduma ya MNP ina faida zipi?

Utaendelea kutumia namba yako ya awali unapohama kutoka mtoa huduma mmoja kwenda mwingine na hivyo kufurahia uhuru na huduma za mtoa huduma
mpya.
• Utapokea simu na meseji bila kujali ni mtandao upi umehamia na bila kuwa na haja ya kuwataarifu marafiki, familia na wafanyakazi wenzako au washirika katika shughuli zako kwamba umebadilisha mtoa huduma wako.
• Utaokoa fedha kwa kuwa hutakuwa na haja ya kununua laini mpya kwa kila mtoa huduma au kuwa na simu ya kiganjani zaidi ya moja.
• Utaweza kuchagua mtoa huduma ambaye unaona
anatoa huduma bora zaidi, anakidhi matarajio yako na
ana ubunifu katika kutoa huduma.

Ili kujua Ni Nini Unatakiwa Kufanya Ili Kupata Huduma
Hii Tembelea Hapa..

Fanya Yafuatayo Ili Kuhamia Mtandao Mwingine Bila Kubadilisha Namba – SMARTPHONES TANZANIA
 
Nimepitia hio link ila hii inshu haipo clear kuelezewa, Je number angu ya simu itakuwa hii hii mfano niko voda nataka kushift Tigo je nikihamia tigo ntabakiwa na hio hio number ya voda? Na hio inshu ya kwenda kwa wakala tena niaje mara sijui ninunue chip mpya ya huko ninakotaka kuhamia more elaboration please
 
Mimi nataka kuhama lakini swali langu mfano namba yangu ni 0717 100 100 nikitaka kuhamia voda, zantel, airtel ama halotel itabaki hivyo hivyo ama hizo namba za kitambulishi cha mtandao (0717) zitabadilika kuendana na mtandao husika nitakao hamia?

Kama zitabadilika watu wangu wa karibu watanipataje?

Kama hazita badilika vocha nitatumia ya mtandao upi?
 
Mobile Number Portability (MNP)
Ni Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe
01 Machi 2017.

Huduma ya MNP ina faida zipi?
Ni Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe
01 Machi 2017.

Utaendelea kutumia namba yako ya awali unapohama kutoka mtoa huduma mmoja kwenda mwingine na hivyo kufurahia uhuru na huduma za mtoa huduma
mpya.
• Utapokea simu na meseji bila kujali ni mtandao upi umehamia na bila kuwa na haja ya kuwataarifu marafiki, familia na wafanyakazi wenzako au washirika katika shughuli zako kwamba umebadilisha mtoa huduma wako.
• Utaokoa fedha kwa kuwa hutakuwa na haja ya kununua laini mpya kwa kila mtoa huduma au kuwa na simu ya kiganjani zaidi ya moja.
• Utaweza kuchagua mtoa huduma ambaye unaona
anatoa huduma bora zaidi, anakidhi matarajio yako na
ana ubunifu katika kutoa huduma.

Ili kujua Ni Nini Unatakiwa Kufanya Ili Kupata Huduma
Hii Tembelea Hapa..

Fanya Yafuatayo Ili Kuhamia Mtandao Mwingine Bila Kubadilisha Namba – SMARTPHONES TANZANIA
Mtoa Mada embu tufafanulie vizuri hapa inakuwa hivi mfano 0754 123456 voda 0713 123456( tigo) 0784 123456( airtel) 0625 123456(halotel) 0772 123456 (zantel) AU INAKUWAJE YAANI BAADA YA KUFANYA APPLICATION??
Mimi nataka kuhama lakini swali langu mfano namba yangu ni 0717 100 100 nikitaka kuhamia voda, zantel, airtel ama halotel itabaki hivyo hivyo ama hizo namba za kitambulishi cha mtandao (0717) zitabadilika kuendana na mtandao husika nitakao hamia?

Kama zitabadilika watu wangu wa karibu watanipataje?

Kama hazita badilika vocha nitatumia ya mtandao upi?
 
Mtoa Mada embu tufafanulie vizuri hapa inakuwa hivi mfano 0754 123456 voda 0713 123456( tigo) 0784 123456( airtel) 0625 123456(halotel) 0772 123456 (zantel) AU INAKUWAJE YAANI BAADA YA KUFANYA APPLICATION??
Inabaki namba yako ile ile hamna k8nachobadilika
 
Haz
Mimi nataka kuhama lakini swali langu mfano namba yangu ni 0717 100 100 nikitaka kuhamia voda, zantel, airtel ama halotel itabaki hivyo hivyo ama hizo namba za kitambulishi cha mtandao (0717) zitabadilika kuendana na mtandao husika nitakao hamia?

Kama zitabadilika watu wangu wa karibu watanipataje?

Kama hazita badilika vocha nitatumia ya mtandao upi?
Hazitabadilika vocha utatumia za mtandao uliohamia.. namba yako itabaki ile ile
 
Mnasumbuka kumuuliza maswali wakati na yeye amecopy na kupaste

maana anasema hakuna gharama za kununua laini mpya, wakati majuzi kwenye maelezo yao nilisikia kuna kununua line nyingine

pia salio latakiwa kumalizwa lote kabla ujahama, hawatahusisha kuhama kwa akaunti uako ya pesa ( m-pesa, tg, au airtel money)

kifupi ni usumbufu flani ambao hauna maana
 
Kwa uelewa wangu Mimi hichi kitu kipo hivi ;-
Tuseme we Upo mtandao X na Namba yako ni 0$#@ 123456 na unataka kuhamia mtandao Y, utaomba kubadili Namba tajwa hapo juu, na watakubadilishia mtandao ma sim card kutoka X kwenda Y, kwa maana SIM CARD ya X haiwezi kusoma Y, ila Namba yako itabaki ile ile ya 0$#@ haidhuru Namba ya utambulishi ya Y ni 0&+* , ni kusema wewe utakua mtandao Y kwa Namba 0$#@ 123456 .
TAHADHARI ;- itabidi ujisajili upya kwenye kutumia miamala ya fedha, vile vile itakua Hamna Namba ya utambulisho wa kampuni kwa hio zile dakika za Bure tuwe makini, utadhani huyu bado yupo X kumbe yupo Y na hela zitaliwa zaidi.....
FAIDA;- uhuru wa kuwa na Namba ile ile Bila ya wahka wa kupoteza watu wako wengi, unahama tu !!!
 
Exac

Exactly hiyo ndo maana yake
 
maana anasema hakuna gharama za kununua laini mpya, wakati majuzi kwenye maelezo yao nilisikia kuna kununua line nyingine

pia salio latakiwa kumalizwa lote kabla ujahama, hawatahusisha kuhama kwa akaunti uako ya pesa ( m-pesa, tg, au airtel money)

kifupi ni usumbufu flani ambao hauna maana
Faida yake utabaki na namba yako ile ile bila kubadilika hata kidogo...
 
Haina maana yeyote hii huduma,tena niusumbufu mkubwa usiokuwa na maana
 
Back
Top Bottom