Fanya unachokipenda

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
156
168
FANYA UNACHOPENDA

Siku zote unapofanya unachopenda unapata mafanikio yenye furaha sababu una amani na unacho kifanya ..sisemi kuwa kama unafanya usichokipenda kuwa hakileti mafanikio la hasha! Kina leta mafanikio ila mafanikio yake ni tofauti na unachokipenda..

Vijana wengi duniani wanafanya vitu wasivovipenda hii ni kutokana na familia zetu kupenda kuona watoto wao wanafanya kazi na kuingiza kipato bila kujua kipato kile wanachopata sio moja ya malengo yao wala ndoto zao.. Wengi hucheka usoni lakini moyoni wanaumia zaidi kutokana na kufanya wasivo vipenda..

Maisha ya mtu ili yawe na amani na furaha lazima awe anaishi ndani ya kitu anacho kipenda, ukifanya kitu unachokipenda unajitolea nusu ya maisha yako kufanya kitu hicho sababu unataka kuona mafanikio ndani ya kitu hicho..

Wengi hufeli maisha sababu hawana furaha na kazi zao wanazofanya, sababu kazi wanazofanya sio moja ya machaguo yao wamefanya hivo kwaajili ya familia, marafiki na jamaa waliowazunguka ...usiogope kufanya unachokipenda sababu waliokuzunguka karibu watakusema au kukucheka vyote hivyo ni changamoto ya maisha tu..kumbuka mafanikio hayaji bila changamoto.

Mafanikio ni kama dhahabu au almasi ili kupata vyote hivi yakupasa upasue miamba mikubwa na uchimbe mbali zaidi uki kufikia vitu hivyo na mafanikio ndivyo yalivyo.

Kuwa tayari kukaa mbali na ndugu jamaa na mafariki na kufanya unachopenda kitu kinachokupa amani ya moyo kuliko kukaa nao karibu na kufanya kitu usichokipenda kamwe..watu wengi wamefeli maisha kutokana na kuacha kufanya wanachokipenda na kufanya wasichokipenda kwasababu ya marafiki mpenzi au hata familia wanataka afanye kitu hicho.

kumbuka hao wanaokuambia ufanye usichokipenda hawana moyo wako hawajui maumivu unayoyapata kwa kufanya usicho kipenda.

Cristiano Ronaldo aliamua kuacha shule na kwenda kucheza mpira sababu ndio alikua anaupenda wazazi hawakupenda swala hilo lakini moyo wa Ronaldo haukuwa tayari kuumia kisa wazazi wanapenda asichokipenda..sisemi kuwa uache shule hapana soma kwa bidii sana maana wakati mwingine unachokipenda kinahitaji elimu ila sikiliza moyo wako sikiliza unapopenda na uruhusu moyo wako uishi ndani ya unachopenda ...

Sisemi kazi unayoifanya kwasasa uiache hapana ila unapapata kazi unayoipenda ruksa kuacha uliyonayo na kufanya unayoipenda



.
.
.
..
By Jay Speed
 
ni kweli kabisa tatizo changamoto ni kubwa sana kupata unachokipenda
Najua hilo hasa kwa Tanzania ni changamoto kubwa ....lakini kuna mambo ambayo kufanya unachokipenda ni lazima ufanye tu mfano kama unapenda kuwa dkt lzma usome na utakuwa unavopenda kuwa injinia utakua tu ukisoma na baadhi ya vingine pia mambo mengine yote unaweza kufanya kama unapenda endapo ukajiwekeza vizuri ulipo na baadae kufanya unachopenda

@mitalenamidimu
 
Back
Top Bottom