Umuhimu wa kuwa ndani ya mfumo

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
UTANGULIZI

Maisha ya mwanadamu yamefungwa ndani ya mifumo, hakuna kitu ambacho kiko nje ya mfumo, wakati Mungu anamuumba mwanadamu aliweka mifumo Kwanza Kabla ya kumweka mwandamu ili mifumo iweze kumsaidia mwanadamu kuishi ndani ya mifumo

Matendo ya Mitume 17:26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

Mungu alipomweka mwandamu alimwekea na mifumo ndani yake ili iweze kumsaidia katika Maisha yake ya kila siku ndio maana akaweka nyakati /majira na mipaka maeneo etc

Mifumo ili kuwa mifumo inawekwa Kwa sheria ambayo Sheri unatengeneza mapatano ndani ya mfumo, sheria ndio inayoongoza mifumo kufanya kazi maana pasipo sheria mifumo haiwezi kufanya kazi

Duniani kuna mifumo miwili kuna mfumo wa nuru ambao huko chini ya sheria ya dhambi na mauti na kuna mfumo wa nuru ambao uko chini ya sheria ya roho wa uzima

Warumi 8:2Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Mifumo ndio inayotoa maamuzi juu ya Maisha yako Katika maeneo yafuatayo:-
A. Kazi yako
B. Ndoa yako
C.Kesho yako
D. Etc

Kazi yako

Mfumo unakutengezea wewe ufanye kazi gani? Ukae nchi gani , na ni mazingira gani ya wewe kustawi , ndani ya mifumo ndio kuna lunch yako

Watu wengi wamekuwa na sababu mbalimbali kwa sababu hawana kazi wamekuwa ni rahisi kuilalamikia serikali lakini wamesahau kwamba kuna mifumo ambayo Hiko juu ya mifumo ya serikali

Unaweza kutafuta kila sababu juu ya mifumo ya ajira etc Ila ujue mifumo ya ajira hiko ndani ya ulimwengu mbili kwa hiyo ili uweze kupata ajira ndani ya mfumo ni lazima kuwa ndani ya mfumo husika

Mfumo wa nuru ndio unaweza kuwa ndani ya mfumo wa Giza na ukafanya kazi lakini mfumo wa Giza hauwezi kuwa ndani ya mfumo wa Nuru

Danieli 1:19-20 Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme.
.
[20]Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake.

Daniel na wenzake waliingia kwenye interview ambayo walishindana na waganga na wachawi na walionekana wanahekima na maharifa mara 10 zaidi ya waganga na wachawi wakapata ajira

Kwa hiyo ukiwa ndani ya mfumo wa nuru haijalishi unakwenda kufanya interviw kwenye mfumo wa Giza au unashindana na watu wa ufalme wa Giza uwe na uhakika kama Mungu kakuwekea nafasi yako hapo hakika ni lazima Upate kazi

Haijalishi kuna watu kazini Mungu atafungua mlango wa kukusaidia hata ikiwezekana watoke wewe uingie , au ukuwai kusoma habari ya ester WA kitabu cha ester aliyemwondoa vasti katika nafasi ya umalkia?
 
Back
Top Bottom