Fanya haya ili uishi vyema

Fanya haya ili uishi vyema

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,614
HABARI ZA LEO WANA JF;
Fanya yafuatayo ili uishi vyema...
1. Weka neno la Bwana moyoni mwako daima. Zab. 119:11
2. Epuka kuketi mahali pa watu wenye mizaha. Zab 1: 1; Zab 26:5
3. Ulalapo tafakari kitandani mwako mambo mema. Zab 4:4
4. Kamwe usilikose kusanyiko la wacha Mungu. Zab. 27:4 Zab 122:1
5. Chagua marafiki wacha Mungu. Mithali 13:20
6. Mazungumzo mabaya huaribu tabia njema. 1 Kor.15:33
7. Epuka kutazama kusikia mambo yasiyofaa. Isaya 42:18-20; Zab. 119:37
8. Kila ulalapo hakikisha hasira na makwazo yote umesamehe. Waefeso 4:26

MPENDWA TAFAKARI VYEMA UWEZE KUISHI VYEMA.
 
umenena vyema. Hofu yangu ni kwenye namba 2 na 5 kwamba kama utajtenga nao watajuaje mazuri?
 
Wana macho, wana masikio, wanaishi katika jamii hii hii, kama wamechagua kuwa hivyo ya nini kuketi nao?
 
siku hizi na wewe watupa neno la Mungu tu........

Maisha yanabadilika jaman tunashukuru
 
unataka kuniambia Biblia inabagua??
 
Hili neno lipo tu, ila ninachokifanya ni kukolezea tu. Watu wako busy na mambo ya dunia, SMS za ajabu ajabu lakini utamkuta m2 anamaliza hata miezi mitatu pasipo kusoma neno la kumwongezea hekima ya kiMungu.
 
Ubarikiwe
 
unataka kuniambia Biblia inabagua??

Imani yangu ni kwamba haibagui (Biblia) Ila wanadam ndo tunakuwa na choice - kuisoma au kuitunza tu; kuifuata au kuiacha kama ilivyo.
 
HABARI ZA LEO WANA JF;
Fanya yafuatayo ili uishi vyema...
1. Weka neno la Bwana moyoni mwako daima. Zab. 119:11
2. Epuka kuketi mahali pa watu wenye mizaha. Zab 1: 1; Zab 26:5
3. Ulalapo tafakari kitandani mwako mambo mema. Zab 4:4
4. Kamwe usilikose kusanyiko la wacha Mungu. Zab. 27:4 Zab 122:1
5. Chagua marafiki wacha Mungu. Mithali 13:20
6. Mazungumzo mabaya huaribu tabia njema. 1 Kor.15:33
7. Epuka kutazama kusikia mambo yasiyofaa. Isaya 42:18-20; Zab. 119:37
8. Kila ulalapo hakikisha hasira na makwazo yote umesamehe. Waefeso 4:26

MPENDWA TAFAKARI VYEMA UWEZE KUISHI VYEMA.

It is hard not to like Christ and Christianity!
Asante
 
Nakubaliana na wewe ila namba 2 na 5 nadhani sio sahihi. Ukisoma bible sidhani kama kuna andiko ambapo Yesu alijitenga na wenye dhambi na kwamba aliambatana na wale wanao mcha Mungu tu. Yesu hakuchagua watu wakuongea nao ila alikemea maovu yao. Nadhani kuishi maisha ya kikristu ni pamoja na kumpeleka Kristu kwa wale ambao hawajamjua bado na utampelekaje Kristu ni jinsi utakavyoonesha utofauti wako kati yao hao ambao wamefuata njia isiyo njema.

Mawazo haya waliyonayo Wakristu wengi ndiyo yanayofanya watu wengi ambao hawajamjua kristu kuwa na mtazamo hasi juu ya Ukristo. Unakuta mtu ameokoka, na labda anaishi katikati ya watu ambao hawajamjua Mungu, sasa badala ya yeye kuwa chachu ya kuwafanya wale wamjue Mungu, anakuwa wa kwanza kuwanyanyapaa na kuwatenga eti kwa sababu wao hawamjui Mungi! Trust me, IT IS NOT RIGHT!
 
Mkuu; haya si maneno yangu, nimenukuu kutoka kwenye Biblia; na kumbuka KILA NENO LENYE PUMZI YA BWANA LAFAA KWA MAFUNDISHO.
 
Fanya yafuatayo ili uishi vyema...

2. Epuka kuketi mahali pa watu wenye mizaha. Zab 1: 1; Zab 26:5

5. Chagua marafiki wacha Mungu. Mithali 13:20

6. Mazungumzo mabaya huaribu tabia njema. 1 Kor.15:33

7. Epuka kutazama kusikia mambo yasiyofaa. Isaya 42:18-20; Zab. 119:37

na tuyashike makatazo haya, maana humpendeza Mungu
 
Back
Top Bottom