Fanya biashara hizi kama una mtaji kiduchu

Fanya biashara hizi kama una mtaji kiduchu

Biashara ya kukaanga mahindi bisi kwa ajili ya popcorn,,je hii waionaje mkuu au mwaionaje?
Nashida na mashine popcorn sijui naipataje
ipo ninayo ila kioo cha mbele cha kuweka kingne
 
Kuna sista duu mmoja naye alipigwa za uso kubabake heka moja alivuna matikiti nane mimi mwenyewe niliyahesabu tena madogo kama ndimu.Ukitaka kuvunja mazungumzo nae we taja tikiti tu.
Huna akili mkuu! Matikiti 8 inakuwaje hiyo? Mimi nililima ekari 1 na nusu Kasulu, nilivuna lakini ni pungufu ya matarajio. Unaenda sokoni nako Waha wanayakusanya na kuvunga kama wananunua kumbe wanakukalisha ili ukate tamaa ikifika saa 10 ushushe bei. Hawa niliwakomesha maana nilikuwa na pick up ya kazini muda ulipoenda nikayakusanya nikapakia kwenye pick up maana hayaharibiki mbona walinifuata mpaka nyumbani. Nikawasikia wanaanza kusemezana kwa Kiha, lo mmeyakanyaga kwa Msukuma maana hajalimia shida huyu. Pumbavu kabisa Waha wote!😁😁
 
Biashara hapo hakuna hata moja.
Bodaboda ndio biashara pekee dereva anaweza kuanza na mtaji wa nguvu na akili zake pekee.
Unatafta boss,mkataba mezani unaamsha chuma.
 
Huna akili mkuu! Matikiti 8 inakuwaje hiyo? Mimi nililima ekari 1 na nusu Kasulu, nikivuna lakini ni pungufu ya matarajio. Unaenda sokoni nako Waha wanayakusanya na kuvunga kama wananunua kumbe wanakukalisha ili ukate tamaa ikifika saa 10 ushushe bei. Hawa niliwakomesha maana nilikuwa na pick up ya kazini muda ulipoenda nikayakusanya nikapakia kwenye pick up maana hayaharibiki mbona walinifuata mpaka nyumbani. Pumbavu kabisa Waha wote!😁😁
Sina akili tena? Unatumia kipimo gani kupima akili za watu humu mtandaoni?!
 
Ulivyoropoka tu mkuu ni uthibitisho tosha! Matikiti 8 kwa ekari siyo mchezo mkuu!
Ungeuliza kwanini sasa alipata matiki nane tena mimi ndiyo niliyoyahesabu😂😂😂.Huu sio utani .Je nikukuambia bimkubwa wangu kalima heka nne za mpunga kapata gunia nne utaamini?! Mwaka jana ndio alizira hata kuvuna ,maana angepata visado tu.Usicheze na kilimo kama huna capital,unategemea bwawa la maji ya mvua.Kwanza huyo dada tu kwenye mbegu wazoefu wanadai alipigwa bado factor nyingine naziacha.Narudia hana hamu na kilimo tena.
 
Biashara ya mtumba nilifanya kitambo nikiwa form 6 leaver 2012 hii kweli inalipa nilifanyaga na rafiki yangu tulikua tunanunua nguo kwa kupoint siku ya soko mzigo unapofunguliwa then tunazipunguza na kuzirekebisha ziwepoa alafu tunatembeza kwa watu maofisini na maeneo ya kazi. Tuli deal na wanavyuo pia na watu tunaowajua hawana maneno mengi. Tulipiga hela kweli ukinunua nguo ya 3k unauza 5k to 7k kwa wakati ule ilikuwa sio mbaya. Jamaa yangu alikua Yuko vizuri kwenye kushona xo Mimi nilideal na sales zaidi. Baadae tulienda vyuo Kila mtu akaenda na mishe zake. Jamaa mpaka Sasa anakiwanda kidogo anatengeneza mabegi hivi vidogo wanapenda kuvaa vijana wa 2000 na pia ya wanafunzi.
Hii ya dagaa nilimuona rafiki yangu mmoja anaifanya kwa mafanikio alinishawishi ila sikuweza kwakuwa dagaa wa mwanza ni ghali hivyo unahitaji watu wa kipato Cha kati kukuelewa hivyo mm mwenyewe nililose interest maana ilifika mahali jamaa akawa ananisaidia Hadi kuuza ikiwa wake wameisha niliamua kufanya mengine
Hii ya juice brother wangu mtoto wa baba mdogo aliwahi kufanya na rafiki yake ilikuwa inalipa ila jamaa yake alikua anazingua maana ameoa wake wawili na wanategemea hichohicho kipato wakashindwana na mshikaji ila kinalipa maana mshindani wao alikuwa na mtaji mzuri alinunua Hadi Mazda kwa kupitia hii biashara ila bàada ya uchaguzi wa 2020 kupitia na Mh. Magufuli kufariki walipata kashkash yakuvunjiwa vibanda.
Biashara ya duka la mangi linalipa ila linahitaji uvumilivu ni issues yakudunduliza ila ukiwa na mtaji mzuri na kuwa na uwezo wakujua pindi bidha zinaposhuka bei ununue kwa wingi na baadae uweze kuuza kwa faida kubwa bindi zinapopa. Pia kujua machimbo ya bei nafuu, pia location yenye uhitaji ni muhimu hii Bado naifanya ingawa nimemuachia mtu (my partner)kwa Sasa. Nilianza na mtaji kwa bidhaa chini ya laki tano ingawa sikuwa nikiitegemea baadae mtaji ulipofika 2m ndio nikaanza Kuona faida (SIKUWA NIMEPANGA FREM NILITENGEZA KIBANDA CHA CHUMA BAADAE NDIO NIKACHUKUA FREM MTAJI ULIPOKUA).
Biashara ya saloon shemeji yangu anaifanya na uzuri yeye anafundisha mabinti hivyo pia wanamfanyia kazi ana hela nzuri (Anapush Rav 4 mjini) Hivyo ukiwa na uvumilivu safi mambo yanaenda.
Pia kupamba/ makeup kwa maharusi inasaidia maana kupamba kunaanzia 50k Hadi 600k kikubwa ni mtaji wako na management. Licha ya skills Brand ina matter sana. Kuna watu wanamake Hadi 2M per day hasa mwezi Oct Hadi Dec. Hii nimeishuhudi kwa wakazi wa Arusha watembelee Cherry Suzie Beauty kwa Dar Tembelea Nuru Beauty Sinza au wengine wengi tu. Research inahitajika.
umeshusha nondo mkuu lipo la kujifunza hapa
 
Nilifanya huu upuuzi. Walinishawishi mafala flani training kule Makumbusho. Nilikua nikilala naiona Harrier nyeusi. Aisee nilipigwa za shingo.
Kilichobaki ni kununua ndinga kali tukisubiri mafao tu 😀😀 sitini yenyewe kwa life la sasa sijui kama itafika
 
Back
Top Bottom