JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Shule za ufundi zimetakiwa kuuza ramani za majengo zinazobuniwa na kuchorwa na wanafunzi wakati wanapokuwa mashuleni ili kuwaingizia kipato.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu mhe.Chelestino Mofuga alipokagua shughuli zinazofanyika katika shule ya Sanu Technical Secondary School na kujionea shughuli za kiufundi zinazofanywa na wanafunzi.
Miongoni mwa shughuli hizo ni ubunifu wa michoro ya majengo,ujenzi wa nyumba,ufundi wa magari,ufundi umeme pamoja na udereva.
Akiwa katika ukaguzi huo Mkuu huyo wa wilaya ya Mbulu alivutiwa zaidi na mwamko wa watoto wa kike kusoma masomo ya ufundi wa majengo,ufundi umeme pamoja na ufundi wa magari huku wakiachana na dhana kuwa kazi hizo ni za wanaume.
Aidha Mofuga alitembelea miradi ya kimaendeleo katika Halmashauri ya mji wa Mbulu kama vile mradi wa unenepeshaji wa ng'ombe,kiwanda cha mikate,mradi wa tanki la maji la Ayamohe.
Na
Henock Mark