Fani ipi ina soko kati ya Excavator na Greda

Fani ipi ina soko kati ya Excavator na Greda

sio kukuvunja moyo ndugu, wengi wanaoenda shule kusoma izo mashine walikua wanaendesha kama kibarua kapata mchongo wa ajira anachofata ni cheti ili atimize vigezo,

wengine washapata connection, either wana ndugu tarura, halmashauri, migodini, kwenye makampuni ya ujenzi nk, anajua ata akitoka chuo hajajua vizuri atapata kwenye hayo maeneo atakingiwa kifua adi atajulia hapohapo,
Lakini bila ivyo utasoma utamaliza na cheti utapata, ukiomba kazi lazima wakufanyie test hapo ndio zoezi linapokua gumu maana interview za hiyo mitambo hazina ubabaishaji.
Uko deep mkuu umemfanunulia vzr mno ajitahidi kupambana hasa
 
Naomba unisaidie namba ya mwalimu yeyote mwenye chuo Cha veta shinyanga niweze kupata maelekezo ya kujiunga na chuo
 
Daka
Screenshot_20220917-014336.jpg
Screenshot_20220917-014356.jpg
 
Loader kozi bei yake ni 570,000/ kwa miezi miwili
na Grader ni 570,000/ miezi miwili
Excavator 620,000/ miezi miwili
ila malazi milo mitatu kwa siku 300,000/
hapo ni Shanyanga Chuoni
contact nitakutumia PM
Champ mambo vipi, nisaidie nambari zako za simu nataka unielekeze kitu kuhusu icho ulichoandika. Nitashukuru.
 
1. Excavator
Hii unaweza chukua mda mfupi kuijua kama uko makini na unaipenda hivyo miezi miwili inaweza kutosha kuwaamisha watu kuwa unajua na ukakabidhiwa chombo, ila uwe unaendesha kila siku mana vyuo vingi wanafunzi wengi kuliko machine. Imagine mwanafunzi aliyesoma miaka miwili anakuja field haijui hiyo machine.
2. Grader
Inachukua mda mrefu sana kuijui mana ina mambo mengi sana hivyo kwa hyo miezi miwili usitarajie kuijua vizuri kiasi kwamba ukaweza kushindan na watu wengine walioifanyia kazi mda mrefu, mana kwa mfumo wa vyuo vingi unaweza kuta wana grader moja halafu wanafunzi 100, kusababisha kukosa mda wa kutosha kukaa na machine na wengi wanatoa less than 2 hours per day ambao ni mda mdogo sana kwa grader.

Ushauri
1. Jifunze moja wapo wa hizo machine nashauri grader kwavile ina masirahi makubwa ukipata sehemu nzuri na pia haina watu wengi kama excavator,.
2. Jifunze ili kupata leseni tu kisha tafuta sehemu ambayo unaweza jifunza kwa vitendo kwa mda mrefu ikibidi kwa kujitolea, ila kama utapata connection ni vizuri mana utatumia mda huo kujifunza kazi.
3. Wengi waliobobea kwenye hizo machine wamejifunza kwa vitendo kwanza then wajatafuta leseni mf. Mtu alikuwa kwenye kampuni fulani akatoa mda wake kidogo kujifunza au kuna washikaji zake wapo huko wakamfundisha kazi, mana kuna tofauti kubwa kati ya kujua machine na kujua kazi na watu wanataka ujue kazi.
3. Mwisho itakuchukua zaidi ya mwaka kuijua machine tena ukiwa unafanya kazi hivyo kuwa mpole, na kama hauna connection kwenye haya makampuni usitarajie hela yako kurudi kwa kipindi kifupi
Champ, unaweza kunisaidia mawasiliano yako nataka kujifunza kitu kwako kimaelekezo.
 
Back
Top Bottom