Fani ipi ina soko kati ya Excavator na Greda

kindoki

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2018
Posts
213
Reaction score
218
Wadau,

Nimeomba nafasi ya kusoma katika chuo cha ku-operate mitambo mikubwa pale kijitonyama dsm na nimepata nafasi, mtihani unakuja ktk soko la izo fani baada ya kumaliza kozi yangu ya miezi miwili na ada yake bado sijalipa lakini naomba ushauri nisomee EXCAVATOR au GREDA?

Nakaribisha ushauri ili nijue fani ipi ina soko zuri ili nikimaliza masomo yangu nianze kula mapene.
 
kama unaweza unganisha vyote bila kusahau na bobcat ni ajira tele kwa nchi zinazoendelea
 
Usijidanganye ukimaliza hiyo kozi ya miezi miwili basi utakua operator kamili wa kuweza kufanya kazi na kulipwa,

bado utahitaji muda mwingi wa mazoezi ili uive vizuri, changamoto inakuja kampuni gani itakukabidhi machine zake ujifunzie na uwaharibie kazi kampuni nyingi zinataka anaekuja kwaajili ya field awe anajua kazi.

Jiandae kisaikolojia usije ukapagawa baada ya kupoteza ada
 
Sawa nimekuelewa japo unanivunja moyo lakin nitapambania kombe mpaka mwisho
 
sio kukuvunja moyo ndugu, wengi wanaoenda shule kusoma izo mashine walikua wanaendesha kama kibarua kapata mchongo wa ajira anachofata ni cheti ili atimize vigezo,

wengine washapata connection, either wana ndugu tarura, halmashauri, migodini, kwenye makampuni ya ujenzi nk, anajua ata akitoka chuo hajajua vizuri atapata kwenye hayo maeneo atakingiwa kifua adi atajulia hapohapo,
Lakini bila ivyo utasoma utamaliza na cheti utapata, ukiomba kazi lazima wakufanyie test hapo ndio zoezi linapokua gumu maana interview za hiyo mitambo hazina ubabaishaji.
 
1. Excavator
Hii unaweza chukua mda mfupi kuijua kama uko makini na unaipenda hivyo miezi miwili inaweza kutosha kuwaamisha watu kuwa unajua na ukakabidhiwa chombo, ila uwe unaendesha kila siku mana vyuo vingi wanafunzi wengi kuliko machine. Imagine mwanafunzi aliyesoma miaka miwili anakuja field haijui hiyo machine.
2. Grader
Inachukua mda mrefu sana kuijui mana ina mambo mengi sana hivyo kwa hyo miezi miwili usitarajie kuijua vizuri kiasi kwamba ukaweza kushindan na watu wengine walioifanyia kazi mda mrefu, mana kwa mfumo wa vyuo vingi unaweza kuta wana grader moja halafu wanafunzi 100, kusababisha kukosa mda wa kutosha kukaa na machine na wengi wanatoa less than 2 hours per day ambao ni mda mdogo sana kwa grader.

Ushauri
1. Jifunze moja wapo wa hizo machine nashauri grader kwavile ina masirahi makubwa ukipata sehemu nzuri na pia haina watu wengi kama excavator,.
2. Jifunze ili kupata leseni tu kisha tafuta sehemu ambayo unaweza jifunza kwa vitendo kwa mda mrefu ikibidi kwa kujitolea, ila kama utapata connection ni vizuri mana utatumia mda huo kujifunza kazi.
3. Wengi waliobobea kwenye hizo machine wamejifunza kwa vitendo kwanza then wajatafuta leseni mf. Mtu alikuwa kwenye kampuni fulani akatoa mda wake kidogo kujifunza au kuna washikaji zake wapo huko wakamfundisha kazi, mana kuna tofauti kubwa kati ya kujua machine na kujua kazi na watu wanataka ujue kazi.
3. Mwisho itakuchukua zaidi ya mwaka kuijua machine tena ukiwa unafanya kazi hivyo kuwa mpole, na kama hauna connection kwenye haya makampuni usitarajie hela yako kurudi kwa kipindi kifupi
 
Mitambo inayolipa vizuri ukipata kazi zake ni;

-Motor Grader
-Dozer
-Excavator.

Kama umepata chuo nenda na uhakikishe unaweka juhudi zote kwenye masomo.

Unahitaji ujuzi wa aina mbili
1) Jinsi ya kuutumia mtambo
2)Jinsi ya kufanya kazi za huo mtambo( Cutting,Mixing and Levelling/Grading yote hayo kwa vipimo maalum)

UKIWA DARASANI

Jifunze Operations zote za mtambo, Maintenance ya mtambo na Basic repairs hata kwa uchache. Ukishapata cheti na Leseni yako kama huna connection tafuta site za barabara ukiona Mtambo uko kazini omba kuonana na Oparator.

Ukionana na Oparator muombe ongea nae kama asipokupa mchongo/connection fanya kumuomba uwe msaidizi wake kwa garama zako. Akikubali basi kuwa nae beneti na ukiwa mvumilivu atakuwa anakuachia mtambo masaa machache kabla ya kazi au baada ya kazi na hapo utapata uzoefu wa kazi.

Hao maoparators wakikuamini wanaweza kukuunganisha na kampuni inyohitaji OP na ukaenda kukabidhiwa mtambo.

NOTE:
Ukipata kazi haikisha unakuwa Mwaminifu(usiibe mafuta/diesel), Usiwe mlevi na wala usiwe Mtu wa Papuchi kupita kiasi utaharibu jina lako.

Ukishajenga jina basi utakuwa na uhakika wa kazi itakuwa ni wewe tu kuchagua niende wapi.
 
Wadau,

Nimeomba nafasi ya kusoma katika chuo cha ku-operate mitambo mikubwa pale kijitonyama dsm na nimepata nafasi, mtihani unakuja ktk soko la izo fani baada ya kumaliza kozi yangu ya miezi miwili na ada yake bado sijalipa lakini naomba ushauri nisomee EXCAVATOR au GREDA?

Nakaribisha ushauri ili nijue fani ipi ina soko zuri ili nikimaliza masomo yangu nianze kula mapene.
Nadhani hao ni IHET - Institute of Heavy Equipment and Technology.

Nimeongea nao leo mchana nami pia napeleka kijana wangu pale mwezi February hii kwa ajili ya motor grader operator training. Nilitaka nimpeleke udereva kwa ajili ya malori lakini nimeona siku hizi madereva ni wengi sana mtaani.

Naimani akipambana vizuri, ataondoka na utaalamu kiasi wa kuanzia.
 
Mitambo inayolipa vizuri ukipata kazi zake ni;

-Motor Grader
-Dozer
-Excavator.

Kama umepata chuo nenda na uhakikishe unaweka juhudi zote kwenye masomo.

Unahitaji ujuzi wa aina mbili
1) Jinsi ya kuutumia mtambo
2)Jinsi ya kufanya kazi za huo mtambo( Cutting,Mixing and Levelling/Grading yote hayo kwa vipimo maalum)

UKIWA DARASANI

Jifunze Operations zote za mtambo, Maintenance ya mtambo na Basic repairs hata kwa uchache. Ukishapata cheti na Leseni yako kama huna connection tafuta site za barabara ukiona Mtambo uko kazini omba kuonana na Oparator.

Ukionana na Oparator muombe ongea nae kama asipokupa mchongo/connection fanya kumuomba uwe msaidizi wake kwa garama zako. Akikubali basi kuwa nae beneti na ukiwa mvumilivu atakuwa anakuachia mtambo masaa machache kabla ya kazi au baada ya kazi na hapo utapata uzoefu wa kazi.

Hao maoparators wakikuamini wanaweza kukuunganisha na kampuni inyohitaji OP na ukaenda kukabidhiwa mtambo.

NOTE:
Ukipata kazi haikisha unakuwa Mwaminifu(usiibe mafuta/diesel), Usiwe mlevi na wala usiwe Mtu wa Papuchi kupita kiasi utaharibu jina lako.

Ukishajenga jina basi utakuwa na uhakika wa kazi itakuwa ni wewe tu kuchagua niende wapi.
Shukrani mkuu, umeelezea vizuri sana.
 
sina uhakika na Bandari, ila Chuo kingine kipo shinyanga chini ya VETA na Ada ni 900,000 kwa kozi moja miezi miwili
Mkuu unaweza ukanipatia contact za mhusika VETA Shinyanga? Hii kitu ilikuwa inanifanya kufikiria kwenda huko nikacheki ratiba zao kuhusu operator courses
 
Loader kozi bei yake ni 570,000/ kwa miezi miwili
na Grader ni 570,000/ miezi miwili
Excavator 620,000/ miezi miwili
ila malazi milo mitatu kwa siku 300,000/
hapo ni Shanyanga Chuoni
contact nitakutumia PM
 
Samahan naomba contact za shinyanga kama hutojali kiongozi
 
Back
Top Bottom