LOOOK
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 3,466
- 822
umenena haswa!!uvumilivu na busara... Sioni kwenye list yako ila amini nakwambia bila hizi ingridients mbili hakuna ndoa itakayodumu na hata hayo yote ya kwenye list yako yakiwa hayapo
umenena haswa!!uvumilivu na busara... Sioni kwenye list yako ila amini nakwambia bila hizi ingridients mbili hakuna ndoa itakayodumu na hata hayo yote ya kwenye list yako yakiwa hayapo
Sawasawa Kamanda,hizi Nguvu zipo na zina athiri maeneo yote ya maisha ya mtu katika Ukoo huo!! Mfano wa Maagano ambayo mababu wa mababu wa babu zetu waliofanya ni pale wakati Wana Waisraeli walipotakiwa wachague kati ya Baraba na Yesu nani afunguliwe ana akasulubiwe,Wote kwa sauti kubwa wakasema YEEEEEESUUU,Halafu wakaweka Agano "Na damu yake iwe juu yetu na Watoto wa Watoto wetu". Lilie lilikuwa Agano zito sana,Tushukuru kwamba Kristo mwenyewe kwa Huruma yake alitengua agano lilie!! Sasa katika Jamii zetu za Kiafrika,katika koo zetu nyingi hasa kipindi ambacho hapakuwepo na dini yeyote hapa Afrika,Mababu zetu walifanya maagano mengi ya aina tofauti wakitaka "miungu" iwafanyie hili na lile,kama ilivyoada,Shetani naye huwa hatoi bure he wants sth in return to his wicked favours,hapo sasa ndipo "terms and conditions apply",Kwa baadhi ya koo walitakiwa kumtoa kila mzaliwa wa kwanza,wengine UGUMBA,Magonjwa makubwa hasa magonjwa ya moyo,wengine umasikini uliokithiri,n.k!!! Utasikia,"sisi kwetu lazima tuwe na pressure ya kupanda" Haijalishi kama unajua au haujui maagano haya yatakuandama siku zote za Maisha yako mpaka uamue kujisalimisha kwa Mamlaka iliyo juu kuliko zote(Mungu/Yesu kristo) ili kutengua Agano hilo!! Mungu atusaidie na kutuongoza tuwapate wenza sahihi;Amen!!Well said haya mamikasa yapo na yanakua yameota mizizi hayo maagano toka enzi na enzi. Sio kuoa na kuolewa tu hata mafanikio kuna koo nyingine hata mtu asome vipi mafanikio ni zero. Labda mtu ubahatike kuwa na uelewa na kukemea na kujiondoa katika hizo nguvu za maagano zilizofanywa na mababu/bibi zako.
mkuu kunamtoto nimekufa nimeoza naninampango wa kutangaza nia mbele ya jamii.tatizo mdogo wake uwa anasumbuliwa na sikocell na niyeye mwenyewe aliniambia wala nilikuwa sijui.kama ingekuwa wewe ungefanya je hapo?Mambo ya kuzingatia kabla hujaoa hasa kwa mwanaume1.Iman ya dini ya mkeo mtarajiwa,,,mcheki kivipi anamuofia mungu wake?kama ana imani madhubuti chukua jiko.2.Urembo/uzuri,anapaswa awe mrembo kwa mtazamo wako....maana hata ukirudi home umechoka na mihangaiko wyf atakufariji kwa urembo alonao na mashamsham ya mahaba.3.Nasaba yake,yaani angalia connection ya familia ya mkeo mtarajiwa.....je wana trend ya maradhi???acha....je wakorofi? acha.....je wana tabia za ajabu ajabu????....acha...wanaishije na majirani zao????4.Angalia kipato......inashauriwa mume uoe mke ambaye ana weza kuku-support ikitokea umefulia au una matatizo ya kiuchumi....ina maana utakaemuoa awe mtu wa kujishughulisha kwa kazi au shughuli yeyote ya halali
Mlango wa nane?familia au wanawake wenye nuksi ktk ndoa,.. Fafanua mtoa mada
Ndugu naunga mkono hilo ni kweli tena kwa aslilimia kubwa ukiona wazazi hawaishi pamoja Mara nyingi hiyo sio familia nzuri kuoa,Mimi nimeshuhudia hilo kwa mdogo wangu yaani familia aliyooa ni sampuli kama hiyo wote wameachika amebaki yeye tu mke wa mdogo wangu naye ndoa hipo ICU.tuwe makini sana tunapooa ndugu zangu tusikimbilie mwisho tukaingia ktk ndoa zisizo Salama.Wana MMU
Kuna rafiki yangu amekuwa kwenye ndoa karibia miaka 10 sasa .. Hivi majuzi ndoa yao imeanza kupata migogoro ambayo yeye binafsi hajui chanzo chake nini.. Mwazoni alihisi labda mkewe amepata "kidumu", kwahiyo akafanya uchunguzi lakini hajafanikiwa kuhakiki kama ndivyo au sivyo.
Kadri siku zinavyokwenda pale nyumbani panazidi kuwa pagumu kuishi.. Na hivi sasa ameaanza kuwa anakaa kwenye mabaa muda mrefu sana kuliko ilivyokuwa hapo awali maana ananiambia kuwa ni heri amkute mkewe ameshalala vinginevyo inakuwa na maneno ya kuudhi tu..
Jana tulikuwa baa moja mitaa ya Tegeta - Why Not PUB - tunapata biya na baada ya kuchangamka tukaanza kuongelea mahusiano ya ndoa - tulikuwa wanaume kama 8 hivi hapo kaunta na mmoja kati yetu ni mzee wa miaka karibia 60. Baada ya kutusikiliza kwa muda mrefu alitwambia sentensi moja halafu akaondoka. Hapa ninanukuu kauli ya mzee "..vijana sikilizeni..kuna familia ambazo haziolewi wala hazioi.."
Rafiki yangu alipofanya mahesabu ya haraka haraka upande wa familia ya mke wake aligundua kuwa katika watoto wa kike sita wa familia ya mke wake (mke wake ni nne), wote waliolewa na kuachika na wengine wawili wamezaa njee ya ndoa!
Je, ni kweli kuwa kuwa familia ambazo wazawa wa familia hizo ni lazima mahusiano yao ya ndoa hayawezi kudumu? (genetic/coincident/??)
Naomba kuwasilisha...
Wana MMU

Ngoja niende lunch nikirudi nitatoa mchango wangu
Ngoja niende lunch nikirudi nitatoa mchango wangu