TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Jana aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Edward Ngoyai Lowassa alitembelewa ofisini kwake na Wafanyabiashara wana mabadiliko wa Kariakoo. Moja ya kauli kubwa kabisa toka kwa LOWASSA kwa wafuasi wake hao ni hii ya kwamba mwaka 2020 atagombea urais na kuwataka wafanyabiashara hao kutokata tamaa huku akiapa kwamba mapambano ndiyo kwanza yameanza.
Ikumbukwe kuwa moja ya sababu zilizopelekea Lowassa kushindwa kabisa kwenye uchaguzi mkuu uliopita ukiachilia mbali ile ya UFISADI ni kudorora kwa afya yake. Ni udhaifu wa afya yake uliopelekea siku ya ufunguzi wa kampeni za CHADEMA pale JANGWANI, Lowassa kushindwa kabisa kuhutubia na kuwataka watanzania kusoma hotuba yake kwenye tovutu ya chama. Haikuishia hapo, siku 64 za kampeni Lowassa hakuwahi kuhutubia majukwaani kwa zaidi ya dakika nane(8).
Baba ni kichwa cha familia na pengine inakuwa vigumu kwa mmoja wa familia kutia neno kwa kichwa cha familia kwa kuhofia kufokewa. Binafsi nadhani familia ilitarajia baada ya purukushani za kampeni za urais mwaka jana, Mume/baba/babu/mjomba/shemeji yao angejikita zaidi kwenye kuhakikisha afya yake inaimarika ili waendelee kuvuna busara zake kama kichwa cha familia na siyo kutumia nguvu nyingi kwenye siasa huku akijua kabisa uwezekano wa kuwa rais wa Tanzania kupitia Chadema ni haupo kabisa. Pamoja na kwamba baba ndiye kichwa cha familia lakini bado familia inayo fursa ya kumshauri katika mambo ambayo yana maslahi mapana kwa familia na siyo vinginevyo. Familia tumieni Fursa hiyo kumshauri mzee.
Lowassa akumbuke kuwa chama chake chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa sasa(narudia, chini ya Mwenyekiti wa sasa) kitamhitaji zaidi kwa kipindi kingine cha miaka mitano siyo kwa maslahi ya chama na yeye kama yeye, la hasha. Nadhani kila mmoja wetu anajua ujio wa Lowassa Chadema ulichagizwa na nini, nani walinufaika na ujio huo n,k. Ndiyo maana baada ya azma ya wale wachache kufanikiwa walimuachia yeye mwenyewe na akina SUMAYE kufanya Kampeni, walijua wao kama wao wasingeweza kufua dafu kwa CCM.
Lowassa kafanya kubwa sana ambalo wenye CHADEMA yao wanaamini ni makosa yaliyofanywa na ZITTO KABWE na Dr. SLAA. Kwa mujibu wa kauli mbalimbali za wenye CHADEMA yao, ZItto alijua yeye ndiye angekiwa Mwenyekiti wa CHADEMA huku DR. SLAA akiamini yeye ndo angekiwa mgombea urais kupitia CHADEMA 2015. Wako wapi? LOWASSA ni nani mpaka jana 14/01/2016 ajitangaze kuwa ndiye anayefaa kuwa rais wa kupitia CHADEMA 2020, miaka 5 kabla ya uchaguzi? Watamvumilia kwa sababu ni MTAMBA ila sijui siku maziwa yakikauka kama atavumiliwa kwa kauli yake hiyo.
Lowassa anapaswa pia kutambua kuwa kwa historia ya CHADEMA sasa ilivyo, mgombea urais wao ni lazima atoke CCM na ni lazima aendane na Mazingira na mahitaji ya wakati huo. Lowassa ana uhakika kuwa atakuwa anaendana na mazingira na mahitaji ya CHADEMA 2020?
FAMILIA YA LOWASSA MTAMBUE HAYA MATATU:
1. WENYE CHADEMA YAO MIDOMO IKO WAZI KAMA YA SIMBA, WATAMEZA CHOCHOTE TOKA KWA LOWASSA KWA SASA(WATAMKAMUA SANA)
2. MGOMBEA WA CHADEMA ANATOKA CCM NA LAZIMA AENDANE NA MAZINGIRA NA MAHITAJI YA CHADEMA KWA WAKATI HUO