Familia ya Kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Familia ya Kwanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Apr 30, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Apr 30, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  1.Wale Baolojisti walioanzisha maisha Duniani,tokea walipoweka maisha ndani ya maji,mpaka binadamu wa kwanza wa utashi na akili alipotokea. walifurahihswa sana kuwaona hawa binadamu wa kwanza.
  2. Hawa mapacha wawli tutawaita Andon na Fonta. Pole pole akili zao zilianza kukua. Ili waitwe binadamu ilibidi kwanza zijitokeze roho saba zinazoisaidia akili. Kwanza roho ya intuition,roho ya kuhisi kwa sababu maisha yao yalikuwa magumu sana yenye hatari nyingi,na ilibidi waishi kwa kuhisi vitu. Halafu ikajitokeza roho ya kuelewa,wakati akili zao zilipoanza kuwa na uwezo wa kuunganisha mawazo,kuona kwamba jambo moja linahusiana na jambo lingine. Halafu ikatokea roho ya ujasiri,walihitaji kuwa na roho ya ujasiri katika yale maisha ya hatari waliyokuwa wanaishi porini. Halafu ikajitokeza roho ya elimu,spirit of knowledge,roho ya kutaka kuielewa Dunia,roho ya sayansi. Halafu ikajitokeza roho ya ushirikiano,spirit of counsel,kwa ajili maisha yao ilibidi wafanye mambo kwa kushirikiana.
  3. Kwa hiyo hizo ndizo roho tano za binadamu ambazo ni za wanyama wote,mammals. Kwa maana hiyo basi,binadamu hawawezi kuishi bila wanyama.
  Lakini ili wao kuwa binadamu ilibidi wawe na roho nyingine mbili,roho ya kuabudu,nayo roho hii ilianza kwa Fonta,yule mwanamke,halafu akawa nayo pia Andon. Baadaye wakapata roho ya hekima,pale walipoamua kuhama kwenda kuishi mbali na wale wenzao waliokuwa sio wastaarabu kama wao,wakaipata hiyo roho ya hekima.
  4. Hapo ndipo Dunia hii ikatangazwa kuwa wapo binadamu,hawa ndio walikuwa binadamu wa kwanza.
  5.Wazazi wao hawa mapacha hawakutofautiana sana na wenzao,lakini walikuwa kati ya wale waliokuwa wanjanja,wale ambao kwa mara ya kwanza walianza kupigana kwa kutumia mawe na marungu.
  6.Walitoroka,na walipotoroka pia walichukua mawe ya flint,mawe ambayo yakisuguliwa yanatoa cheche. Walijitahidi sana kutengeneza moto lakini walishindwa. Mpaka siku moja Fonta alipopanda juu ya mti na kuchukua nyasi kavu katika kiota cha ndege na kuyaweka katika zile cheche. Walifurahi sana walipoweza kuwasha moto,na wakaanza kutafuta kuni kuukoleza huo moto. Hawa siku zote walikuwa wanaweza kukoleza moto ulioanziswa na radi,lakini walikuwa hawawezi kuanzisha mto wao wenyewe.
  7.Miaka miwili baada ya wao kuondoka alizaliwa mtoto wao wa kwanza,tutamwita 'Sontad'. Huyu ndio mtoto wa kwanza kuzaliwa na kuzungushiwa vitu vya kumkinga. Jumla walikuwa na watoto kumi na tisa,na waliishi katika mapango. Waliwinda katika makundi.
  8.Andon na Fonta walipokuwa na miaka 42 walikufa katika tetemeko la ardhi. Watoto wao waliwazika katika pango na wakaliziba na mawe. Waliishi vizazi ishirini kabla ya kuanza kufarakana kwa ajili ya chakula na misuguano ya kijamii,
  9. Kabila lao lilikuwa lakini walikuwa na mawazo mawili tu katika akili zao;kuwinda kutafuta chakula na kupigana kulipiza kisasi wanapokosewa,au wakidhani wamekosewa.
  10. Siyo rahisi kuwafanya watu kama hawa kuishi kwa amani.Kama watu hawajastaarabika wataudhiana,ndio maana baadaye inabidi watu kuhama.
  11. Wakaanza kutawanyika,hawakwenda sana Asia,na Afrika,walikwenda Ufaransa na Uingereza.
  12. Wakaanza kuwa na akili ya kutengeneza vitu,na uwezo wa mikono yao kutumia vifaa ukaongezeka.
  13. Walipotawanyika utamaduni wao na maendeleo yao vikaanza kupunguka kwa muda wa miaka elfu kumi,mpaka alipofika mwalimu Onagar,ambaye aliyaongoza haya makabila na kuyaletea amani. Akawafundisha kumwabudu Anayetoa Pumzi. Sala aliyowafundisha ni,'' Ewe Pumzi ya maisha,tupe siku hii chakula,tuepushe na laana ya barafu,tuokoe na maadui wetu wa porini,na kwa huruma yako tupokee Ahera.''
  14.Onagar aliishi karibu na Bahari ya Caspian sehemu inaitwa Oban. Kutoka hapa alituma wamisionari wake kuwafundisha watu kuhusu Mungu na kuhusu maisha baada ya kufa.
  15. Na hawa wamisionari ndio walikuwa watu wa kwanza kupika nyama,kutumia moto kutayarisha chakula.Onagar alizaliwa miaka 983,323 iliyopita kutoka sasa 2010. Aliishi miaka sitini na tisa.
  16. Onagar akaanzisha dini yake. Andon na Fonta walikuwa na ruhani tayari,pamoja na vizazi vyao,lakini ni mpaka zilipofika siku za Onagar ndipo ruhani na serafi walinzi[seraphim]walipoanza kuja Duniani kwa wingi.
  17.Andon na Fonta sasa hivi wapo ahera na wanashiriki katika mapokezi ya watu wanaokufa Duniani. Hii ndio kazi yao ya kudumu. Walitaka kutuma salamu kwa watu wote Duniani,lakini ombi hili[kwa hekima] wamezuiwa.
  18. Na hii ndio hadithi ya hao watu wa kwanza.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  source?
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  May 9, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  The source is the Urantia Book
   
 4. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #4
  May 9, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mwandizhi wa hicho kitabu kajuaje kama hao wamezuiliwa kutuma salamu duniani kwa binadamu? au naye (mwandishi) yupo huko huko ahera?
   
Loading...