Familia ya kubenea chupuchupu zanzibar

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Leo niliona nyumba ya familia moja inayofahamika ina uhusiano wa karibu na mwandishi wa huko Dar ndugu Kubenea ikiwa imegongwa na gari na kuharibika huku watu kadhaa wakiwa ndani ya nyumba hiyo.

Nyumba hiyo iliopo mitaa ya daraja Bovu nje kidogo ya Unguja iligongwa na gari liloendeshwa na dereva akiwa amelewa Chakari na kusababisha mshindo mkubwa na kuwafanya watu kadhaa kukusanyika karibu na nyumba hiyo.

Gari hilo ambalo limepelekwa kituo cha Malindi kwa uchunguzi linadaiwa kuendeshwa na mmoja ndugu wa karibu na kigogo wa serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kuna hisia kadhaa kamba Polisi wanataka kuliendesha swala hilo kienyeji na kunyima kutenda haki.
Najiandaa kufuatilia tukio hilo kwa karibu, nachukua kamera kwenda Kituo cha malindi kutafuta undani wa swala hilo.
 
Leo niliona nyumba ya familia moja inayofahamika ina uhusiano wa karibu na mwandishi wa huko Dar ndugu Kubenea ikiwa imegongwa na gari na kuharibika huku watu kadhaa wakiwa ndani ya nyumba hiyo.
nyumba hiyo iliopo mitaa ya daraja Bovu nje kidogo ya Unguja iligongwa na gari liloendeshwa na dereva akiwa amelewa Chakari na kusababisha mshindo mkubwa na kuwafanya watu kadhaa kukusanyika karibu na nyumba hiyo.
Gari hilo ambalo limepelekwa kituo cha Malindi kwa uchunguzi linadaiwa kuendeshwa na mmoja ndugu wa karibu na kigogo wa serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kuna hisia kadhaa kamba Polisi wanataka kuliendesha swala hilo kienyeji na kunyima kutenda haki.
Najiandaa kufuatilia tukio hilo kwa karibu. nachukua kamera kwenda Kituo cha malindi kutafuta undani wa swala hilo

Hata wawagonge wote na magari haki itasimama tu hata siku ya hukumu-Endelea kutuhabarisha tulioko Mrima
 
Leo niliona nyumba ya familia moja inayofahamika ina uhusiano wa karibu na mwandishi wa huko Dar ndugu Kubenea ikiwa imegongwa na gari na kuharibika huku watu kadhaa wakiwa ndani ya nyumba hiyo.
nyumba hiyo iliopo mitaa ya daraja Bovu nje kidogo ya Unguja iligongwa na gari liloendeshwa na dereva akiwa amelewa Chakari na kusababisha mshindo mkubwa na kuwafanya watu kadhaa kukusanyika karibu na nyumba hiyo.
Gari hilo ambalo limepelekwa kituo cha Malindi kwa uchunguzi linadaiwa kuendeshwa na mmoja ndugu wa karibu na kigogo wa serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kuna hisia kadhaa kamba Polisi wanataka kuliendesha swala hilo kienyeji na kunyima kutenda haki.
Najiandaa kufuatilia tukio hilo kwa karibu. nachukua kamera kwenda Kituo cha malindi kutafuta undani wa swala hilo

wafuatilie labda kuna mambo ya siasa maana si unajua Kubenea wanamchukia anavyosema true, sasa yawezekana chuki hizo zinataka kusambazwa hadi kwa ndugu zake
 
Ni ajali kama ajali zingine, mbona jana sinza kuna mtu nyumba yake imegongwa na mlevi tena ana mahusiano ya karibu na kigogo lakini wamezungumza yameisha? kwa hili sitaki unafiki
 
Taarifa zinasema nyumba iliyogongwa ni ya dada yake Saed Kubenea, mwandishi wa habari na mmiliki wa Mwana HALISI. Dada yake huyu ndiye aliyemlea Kubenea na ndiye dada yake mkubwa katika familia yao ya watu saba – wanawake wawili na wanaume watano. Huyu dada ambaye nyumba yake imegongwa na gari ni kada wa Chama Cha Mapinduzi.

Kubenea mwenyewe yupo salama nyumbani kwake Dar es Salaam. Kuna habari kuwa jana alipanga kuja Zanzibar.
 
Jamani mkimbizeni na chata loliondo kama ameumia kidogo
pole kakangu kubenea
 
KITUO CHA POLISI MALINDI: Muhusika yaani dereva amekimbia na mwenye gari amedai eti atoe fidia ya sh elf 20 kama fidia ya nyumba iliobomoka. mwenyewe amekataa na ametaka aongezwe jambo ambalo lilileta mzozo. Plisi wameamua kulipeleka swala hilo mahakamani.
wasiwasi mkubwa umetanda kama kweli polisi watawatendea haki wa husika. kwani mhusika aliwahi kufika mapema na wanawasiwasi kwamba RUSHWA ikatumika kuzima tukio
 
Kubenea ni shujaa wa Tanzania hivyo yeyeto mwenye nia ya kumdhuru na ashindwe na alegee. Wanajamvi mvuatilie suala hilo mtujuze kwani hata mabadiliko ya Tunisia yalisababishwa na kutokuwepo kwa haki.
 
  • Familia ya kubenea chupuchupu!
  • Nyumba kugongwa na gari (dereva akiwa mlevi)
  • Dereva ndugu wa karibu wa kigogo!
  • Kubenea ilikua aje Zanzbar!
Ngoja nitafakari kidogo na kuchanganua mnyumbuliko huu!
 
Bajabiri heshima yako mkuu! Tumezoea kupewa milinganyo (eqns) ambazo tunapaswa kuzitafutia majibu..ila sio kanuni ya kudumu kwa kua wakati mwingine tunakua na majibu hivyo kulazimika kujiuliza maswali!..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom