Falsafa ya ng'ombe wawili

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
FALSAFA YA NG'OMBE WAWILI.
By Malisa GJ

Baada ya anguko kuu la uchumi wa dunia (Great Economic Depression) lililoanzia huko Marekani mwaka 1929-1933, kuliibuka dhana nyingi kuhusu mfumo ambao Marekani ilipaswa kuutumia ili isitumbukie tena kwenye anguko kama hilo.

November 29 mwaka 1935 Mwanasheria maarufu nchini humo Silas H. Strawn aliandika hadithi maarufu kama 'The parable of Isms' inayozungumzia mifumo mbalimbali ya kiuchumi duniani kwa kutumia Falsafa ya ng'ombe wawili. Nimefanya tafsiri isiyo rasmi kwa Kiswahili.

1. UKOMUNISTI
Una ng'onbe wawili, serikali inawachukua wote kisha inakugawia maziwa.

2. UJAMAA
Una ng'ombe wawili unampa jirani yako mmoja.

3. UFASHISTI
Una ng'ombe wawili, serikali inakunyang'anya wote, kisha inaanza kukuuzia maziwa.

4. UKIRITIMBA
Una ng'ombe wawili. Serikali inakunyang'anya wote. Inamuua mmoja, inamkamua aliyebaki, kisha inamwaga maziwa.

5. UBEPARI WA KALE
Una ng'ombe wawili. Unauza mmoja na kununua dume. Unamtumia kuzalisha jike. Mifugo inaongezeka, uchumi unaimarika. Unawauza wote, unatunza mafao ya uzeeni.

6. UBEPARI WA KISASA
Una ng'ombe wawili. Lakini unaenda kwenye soko la hisa na kuandikisha unao watatu. Unawauza. Kisha unatumia hati ya mkopo ya shemeji yako kufidia gharama na kudai ng'ombe wanne. Unachukua watano kwa kusamehewa kodi yule wa tano. Unapewa haki kisheria ya kukamua ng'ombe 6 kupitia kampuni ambayo imesajiliwa kisiri kukuuzia ng'ombe 7. Ripoti ya mwaka inaonesha una ng'ombe 8 na unatarajia kuongeza mmoja lakini kiuhalisia unao wawili tu.

7. UCHUMI WA KI-ITALIANO
Una ng'ombe wawili, lakini hujui walipo. Unaamua kwenda kula lunch.

8. UCHUMI WA KIFARANSA
Una ng'ombe wawili. Lakini unahamasisha mgomo na maandamano. Unafunga barabara kwa sababu unataka serikali ikupe ng'ombe wa tatu.

9. UCHUMI WA KIMAREKANI.
Una ng'ombe wawili. Unauza mmoja, halafu unamlazimisha aliyebaki atoe maziwa ya ng'ombe wanne, anakufa. Unaajiri mtaalamu kuchunguza chanzo cha kifo chake.

10. UCHUMI WA KISWISI
Una ng'ombe 500, lakini humiliki hata mmoja kati yao. Unawatunzia watu na unawatoza gharama za kuwatunzia.

11. UCHUMI WA KI-IRISH
Una ng'ombe wawili, lakini mmoja kati yao ni farasi.

12. UCHUMI WA KI-AUSTRALIA
Una ngombe wawili, wote unawakamua. Unauza maziwa. Biashara inakwenda vizuri, unaamua kufunga biashara upate muda wa kunywa bia.

13. UCHUMI WA KICHINA
Una ng'ombe wawili. Unaajiri watu 300 kuwakamua, kisha unajisifu umeongeza ajira na kukuza uzalishaji. Hutaki watu wajue hali halisi ilivyo. Na yeyote anayeripoti uhalisia unamkamata, ili kumfumba mdomo.

14. UCHUMI WA KIHINDI
Una ng'ombe wawili, unamua kuwaabudu.

15. UCHUMI WA KIIRAQ
Watu wanaamini una ng'ombe wengi. Unawaambia huna hata mmoja, hawaamini. Wanapiga bomu, wanavunja ukuta na kuvamia nyumba yako. Wanakuta kweli huna ngombe, lakini wanakusifu kwa kuwaruhusu kutekeleza demokrasia.
16. UCHUMI WA KIINGEREZA
Una ng'ombe wawili, lakini wote ni vichaa.

17. UCHUMI WA KIGIRIKI
Una ng'ombe wawili uliowakopa bank za Ujerumani na Ufaransa kwa makubaliano ya kupeleka maziwa. Unaamua kuwachinja na kuwala. Benki wanakuja kuchukua maziwa huna cha kuwapa. Unaamua kupiga simu IMF kuomba mkopo wa ng'ombe wengine wawili, wanakupa. Unawachinja na kuwala tena. IMF na benki wanaungana kuja kudai ng'ombe zao, unawaacha ndani, unaenda saluni kunyoa nywele.

18. UCHUMI WA KIAFRIKA
Huna ng'ombe. Jirani yako anakupa ng'ombe wawili. Unawakamua na kuwatia bakora lakini huwapi chakula wala maji. Wanakufa. Unaenda kwa mganga kupiga ramli, kujua mchawi aliyeua ng'ombe wako. Mganga anakuambia ni jirani yako aliyekupa ng'ombe.

Credit: GS Malisa
 
Ulichoandika unakijua mwenyewe. Jamani Kama Kuna mtu anayeelewa alichoandika huyu mleta mada atufafanulia .Mimi sijaambulia kitu na Sina credit ya kumpa.
 
Ulichoandika unakijua mwenyewe.Vipi Kuna nati imefyatuka kichwani? Jamani Kama Kuna mtu anayeelewa alichoandika huyu mleta mada atufafanulia .Mimi sijaambulia kitu na Sina credit ya kumpa.
Slow learner huwez kuelewa
 
Mwaka 1935 wakati huyo wakili anaandika hii falsafa.

IMF ilikuepo? Ilikua na nguvu kama iliyokua nayo baada ya 1945?

Iraq ilipigwa bomu kisa demokrasia? Hiyo miaka ya 1930s?

Hiyo miaka ya 1930s Ugiriki ilikua hovyo kiuchumi? Siyo wamekua hovyo miaka ya 2000s mpaka leo?

Au mambo mengine mleta uzi umejiongeza?
 
MAHITAJI YA ARDHI YALIPOKUWA MAKUBWA YAWEZEKANA YALISABABISHA UHURU WA NCHI MWAKA 1961 CHEKI HII ELIMU YA MAENDELEO LABDA IPO SIKU TUTATUMIA MBINU ZA ADOLF HITRA WA UJERUMANI


KILIMO/MIJI ==== a + b(MATUMIZI BORA YA ARDHI) + b(MATUMIZI BORA YA WATU NA ELIMU ZAO) + c(MIFUMO BORA YA USAFIRI KAMA MAGARI YA ABIRIA) + d(KULIDHIKA) + e(LIFESPANI YA VITU MAANA NYUMBA ZA WAZEE YAWEZEKANA NZURI KULIKO VIJANA/JENGA SIIPENDI) + f(KUTENGENEZA VIO...NGOZI WA KUWAFUATA) + g(MATUMIZI BORA YA MUDA/VIPAUMBELE VYA WAPI TUANZE NA WAPI TUMALIZIE) + ERROR TERM


KAMA UKIBISHA UNATAKIWA UPENDE KILA KITU ILI KUZIBA KELELE LA SIVYO HATA WEWE UNAUMUHIMU KWENYE STORY ZA ADOLF HITRA....

MAANA HATA UKIFA UTAITUMIA TU..


LA SIVYO UKIONGEA NI KAMA KATUNI TU
 
Ulichoandika unakijua mwenyewe. Jamani Kama Kuna mtu anayeelewa alichoandika huyu mleta mada atufafanulia .Mimi sijaambulia kitu na Sina credit ya kumpa.
Mjibu kulingana na akili yake ilivo!! yaani no; 18, mjanja kuliko! waliotangulia juu! kwa kuwa huyu number 18 ameenda kutafuta causes kwa mganga,(mweusi mwenzake) bila shaka Ramri itamgundulisha kuwa ''hawa ng'ombe wamekuwa-genetic engineered, huwawezi fuga wa ki-Africa'' ili upate faida hizi;

utachapa km kipimo/uimara hafi, watalima utakavyo, watakula kivyao, watakata majani,shambani na nyumbani kivyao, mbolea ipo, wabeba mizigo, utakula, wasaga nafaka, watateka maji mbali, utauza, utatumia maziwa matamu pasi kuchakachuliwa!

Pia siyo tija kivile, Why African afuge ng'ombe vichaa! wkt ng'ombe wanao jichunga wapo tele? mazingirani. hafi kwa fimbo! kituko ni kufuga ng'ombe mizigo, umchemshie maji ya kunywa,apelekwe hospitali, wakisemwa tu wanakufa .heee!

Ni ujinga hasa, na ku-waste his time by mere looking km aliweza chunga vitu adimu Duniani km Nyati, pundamilia, swala bila shida ya kulisha, watu wanaangalia kwa malipo, kwa nini apoteze muda kukatia ng'ombe wa Kizungu majani?

Mwafrica Muua ng'ombe wa kufugwa ana akili, aliua akijua kinacho mfaa kipo Why this rubbish? hii falsafa ni ya kizamani sana, walipewa Babu zetu wajione Duni/mafara. Hiyo Great Depression yako ililetwa maksudi na Shadow Global elitists! of NY Wall street wa USA na Ulaya yote. and they are still active today!

Mleta Mada lazima atakuwa ni Mtu mzima sana, hajui kufanya Book analysis za vijana wa kisasa, hivo kakurupuka na kutuletea humu alichofundishwa na Wakoloni, kifupi jua kuwa Authors, na Western medias za weupe wana lenga ku-entertain wazungu wenzao zaidi! kuliko weusi! Thenceforth; uki-refer kwa Author mweupe kuwa makini na unachofanya humo, sisemi usisome but waangalie kwa jicho la 3!!!! ''unasikia Babu''
 
Ulichoandika unakijua mwenyewe. Jamani Kama Kuna mtu anayeelewa alichoandika huyu mleta mada atufafanulia .Mimi sijaambulia kitu na Sina credit ya kumpa.


Akili ndogo huwezi kuambulia kitu.
 
"UKIRITIMBA
Una ng'ombe wawili. Serikali inakunyang'anya wote. Inamuua mmoja, inamkamua aliyebaki, kisha inamwaga maziwa."


Ukiritimba ni noma


Unforgetable
Yes! ni nzuri, ukome kufuga fuga fanya kingine ambacho hawakijui,
mfano; umeme wa Panya Buku kuendesha viwanda, atakunyang'anya wapi! km akichukua viwanda vinadoda! hakuna uzalishaji wa mali, atakurudishia kwa magoti na hela juu! hapa na wewe unampiga za uso alipe mara dufu! analipa na ng'ombe alochukua, bila kujua!
 

Hii ni nimeikubali mkuu,hapo hata umeme wa kutumia mikaratusi au bwn njenje unatosha kabisa kwa size 45" by 24' provided geo thermal iko partially immersed.

Na ng'ombe hao wanakua maradufu kama ni heifer au wale wenye kipenga kinachotumiwa kusindika malighafi adhimu,hapo hata kiwanda kina step down kwa production unless kuwe na extended torsion bar yenye msongo mkubwa wa 14KW kwa compression ratio ya 16:2 na itatakiwa kue na shift 3.
 
Mleta mada asante Sana! Inafikirisha. Mimi naona falsafa hii bado inaishi Hadi Leo with exception ya wachina.
Unaweza weka na English version.
Natanguliza shukrani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…