Kwani mpaka leo hamjajua falsafa ya CCM mbona iko wazi kabisa..
Angalia aliyofanya Lowana Kuchota mabilioni hadi Nyerere akamshtukia...
Ona aliyofanya Rostam na kampuni yake ya Caspian
Manji na kashfa ya Quality plaza
Mkapa na kiwira na hotel africa ya kusini
Jk na hotel ya serengeti na ikulu ya chalize
mramba na PrecisionAir wizi mtupu..
Mgonja na jengo refu kupita yote arusha next to Golden Rose hotel
yona na kuuwa General tyre na yeye kuwa agent wa tyres kutoka china na kwingineko..
KWA KIFUPI FALSAFA YA CCM NI CHUKUA CHAKO MAPEMA... KWANI WATANZANIA NI WAJINGA NA HAWAJASOMA..
SASA ITAWATOKEA PUANI...
Naomba kuuliza swali moja tu, hivi hii imesomwa na wale wasomi waliopo kwenye pay roll yenu kama akina baregu na Kitilla? hivi hata maana ya falsa nayo mfundishwe?
Ni Ujamaa gani na Azimio lipi la Arusha mnalolisema? ni ule mliounajisi kwa kuweka Azimio la Zanzibar na kuanza wimbi jipya la uporaji mali za serikali na nchi? Ni kichaa tu ndiye anayeweza kuaamini CCM ya sasa ni ya falsafa za kijamaa kutokana na yanayojiri ambayo yanathibitisha jambo moja tu, nalo ni kwamba falsafa ya Ujamaa ilishauwawa muda mfupi tu tangu mwasisi wake alipoachia ngazi yaani alipong'atuka.Ujamaa ni nini?:lol: Na azimio la Arusha bado lipo, maana nipo mbali na Tanzania.
Hebu some hapa chini:
Chama chetu ni miongoni mwa vyama vichache katika Afrika ambavyo vimefaulu kubuni nadharia ya ujamaa iliyo sahihi, wazi na ya kiwango cha juu. Nadharia hiyo ya Chama inajidhihirisha yenyewe katika Katiba, Azimio la Arusha, Mwongozo na maandishi mengine muhimu ya Chama. Nadharia hii ya siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea imetujengea msingi wa uelewano, umoja na ushirikiano wa aina mpya katika ujenzi wa taifa na kutufanya tueleweke na wengi kimataifa, jambo ambalo limetupa sifa na heshima duniani kote.
Falsafa ya Chama
- Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika Nguvu na Mamlaka ya Umma (The Peoples Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
- Aidha falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
- Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
- Historia inaonyesha kuwa UMMA wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
- CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka Nguvu ya Umma. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
- CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa kuchaguliwa kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza waliowachagua kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
- Hivyo basi, falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
- Falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
Jamani CCM kinavyoadhirika hivi sana kwa kudandia kila kitu hadi hoja za wengine tu inasikitisha kweli kweli.
Tangu chama hiki kijitangazie kule Zanzibar kwamba tangu wakati huo kimeachana na Sera tanzu ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA na kukumbatia mfumo mpya wa Soko Huria, nasema hadi leo hakijulikani kimatendo kwamba hasa wenzetu wanafuata dira na falsafagani kuleta maendeleo nchini.
Siku zote jitihada kubwa bila kuwa na malengo ni kazi bure, sijui kukifanyia tathmini hii serikali ya Kikwete ndio hasa watu tukaanzie wapi hivyo!!!!!
Falsafa ya Chama
- Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika Nguvu na Mamlaka ya Umma (The Peoples Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
- Aidha falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
- Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
- Historia inaonyesha kuwa UMMA wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
- CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka Nguvu ya Umma. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
- CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa kuchaguliwa kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza waliowachagua kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
- Hivyo basi, falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
- Falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
Ninavyofahamu mimi, falsafa ya CCM ni kuwa:
1) Chama cha Wakulima na Wafanyakazi (ingawa siku hizi hata wafanyabiashara ni chama chao)
1) Binadamu wote ni sawa (ingawa si sawasawa).
2) Ili tuendelee tunahitahi ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora.
3) Ujamaa na Kujitetea ndio njia pekee ya kujenga Taifa la watu walio sawa na huru.
Falsa ya CCM imejengeka katika imani ya Binadamu wote ni sawa, kuanzia hapo ndipo linakuja suala la ujamaa, sasa suala la kama CCm inaonekanaje kwa miwani yako hilo ni lako binafsi lakini kuna watu wengi bado wanaamini katika CCM na utu, japo kwenye kundi la mamba kenge hawakosi.
binadamu wote ni sawa ili litakua jambo jipya sana ndani ya ccm kwa sasa,kwanza kama falsafa yenu ni hii basi mmepoteza dira kama inavyosemekana
Sanga, kwa katiba ya ccm toleo la 2010 sidhani kama wana itikadi na sera, ila wana imani za chama, navyojua imani sio lazima ziwe itikadi, ila sera kama chama hawana kwa sababu hazijaainishwa katika katiba yao.
Kwa hayo yote uliyo yasema hapo juu niki summarize ni kuwa falsafa ya CHADEMA ni udini + ukabila + ukanda ! Hongera kwa kutujuza