Falsafa ni zao la burudani lililojikita katika udadisi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,673
698,670
Wana falsafa wa zamani walianza falsafa walipomaliza mahitaji ya kimsingi ya chakula na maji na makazi.

Ukiwa na njaa huwezi kuchanganua ni kipengele kipi cha kimetafizikia ndicho kisababishi kikuu na ujuzi wa kuwa na inzi na kuonyesha nini katika epistemolojia au phenomenolojia.

Vile vile pia ni azma inayofanywa na watalii hao walionaswa chini ya bahari. Karibu kila kitu kilichogunduliwa, kilikuja kupitia udadisi. Ikiwa una njaa, hutakuwa na kiwango bora cha udadisi wako.

Hii ndiyo sababu uchunguzi wao hautakuwa na maana kwa Waafrika wengi. Bado tuko kwenye kiwango cha msingi cha mahitaji.

Hata viongozi wetu wa kiafrika bado wanatafuta nyongeza ya mishahara na ziada ya mali.

Sisi tutulie tu bado tuko nyuma sana na hii ndiyo ilifamnya mzungu kujifanya kaichunguza dunia mpaka kudai kuwa ameigundua Afrika.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtanzania wa kawaida akipewa kofia ya CCM na elfu tatu anamchagua mgombea wa hovyo pasipo kulinganisha hoja.

Hata falsafa inayomuongoza kwenye maisha hana. Anaenda na 'beat' la matamko ya wanasiasa. Wakisema nitabadilisha maisha yenu na kuwajengea barabara wanawapata kama wote.
 
Mtanzania wa kawaida akipewa kofia ya CCM na elfu tatu anamchagua mgombea wa hovyo pasipo kulinganisha hoja.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…