Falsafa Mikataba Tanzania

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,306
Mikataba mingi Tanzania imekuwa ikilalamikiwa. Walalamikao wamekuwa wakituma shutuma na tuhuma za kukosa uzalendo na ubinafsi upande wa Watanzania wanaotuwakilisha kwenye mikataba hiyo. Hoja yangu: Falsafa ndio chanzo, katu si ubinafsi au makusudi. Angalia bit.ly/Ngombe kwa mfano.

Tuchukulie mfano wa helium.
  1. Hivi helium ilipo hapo chini ya ardhi. Mmiliki ni nani?
  2. Mitambo ya kuchimbua helium itakapoletwa nani anamiliki mitambo?
  3. Gesi ya helium ikishachimbuliwa ikaja juu ya ardhi, nani anaimiliki? Kwa nini?
Hapo kwenye masuali hayo ndipo kwenye matatizo kwenye mikataba mingi inayolalamikiwa. Na mikataba isipoweza kujibu vizuri masuali hayo, matatizo kwenye mikataba ya rasilmali asilia yataendelea kuwa changamoto.

Sivyo?

Mlenge
 
Nchi nyingi zilizoendelea zinatumia udhaifu wa teknolojia kwa nchi zinazoendelea Kama silaha ya kupata umiliki wa rasilimali wanazochimba kwa kuweka vipengele vinavyowanufaisha Wao kwenye mikataba mingi.

Ilitakiwa nchi zinazoendelea ziwe Na msimamo mmoja wa kuzitaka nchi zilizoendelea kutoa huduma ya kuchimba Tu, suala la kuuza liwe Ni la nchi inayotoa malighafi husika kwa kuwa Na Wao wanahutaji hiyo malighafi.

Ikishindikana basi tukose wote, jambo ambalo haliwezekani kwa kuwa nchi nyingi za ulaya, Asia Na amerika zinategemea nchi za Afrika kwa malighafi ambayo ndiyo nguzo ya maendeleo yao.

Tatizo sisi tuna tamaa Sana, hayati baba wa taifa aliweza kusimamia hili
 
...
Ilitakiwa nchi zinazoendelea ziwe Na msimamo mmoja wa kuzitaka nchi zilizoendelea kutoa huduma ya kuchimba Tu, suala la kuuza liwe Ni la nchi inayotoa malighafi husika kwa kuwa Na Wao wanahutaji hiyo malighafi.
...
Ni kweli tuwaite waje kuchimba tu. Malipo yao ni sehemu ya kile kitakachochimbuliwa.

Kwa mfano,

Mchimbaji atachukua asilimia X. Tanzania itachukua asilimia Y. Mchimbaji atapata kurudisha gharama zake za uwekezaji, gharama za uendeshaji, ikiwemo kodi na mrabaha, kutoka kwenye hiyo asilimia yake X. Nchi itaamua cha kuifanyia hiyo asilimia Y yake. Siyo tena Tanzania inanunua gesi (iliyokuwa) yake yenyewe.

Wawekezaji wanaleta zabuni zao kwa vigezo hivyo hapo juu.

Tatizo kwisha.
 
Back
Top Bottom