Falsafa: Baruch Spinoza

Falsafa: Baruch Spinoza

Radium

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2022
Posts
490
Reaction score
871
Baruch Spinoza ni mwanafalsafa wa karne ya 17 wa Dutch aliyejaribu kuivumbua dini kivingine, kuiondoa kutoka kitu kilichopo kishirikina, kisicho kisayansi lakini wakati huohuo chenye kupooza nafsi za watu.

"Baruch" neno la ki Hebrew lenye maana ya "Blessed", alizaliwa katika kota za kiyahudi huko Amsterdam mwaka 1632, na alikua kwa mfumo na mawazo yote ya kiyahudi. Mababu zake walihusiana pia na mayahudi na walishiriki katika safari za peninsula ya Spain wakati wa kuueneza ukatoliki mwaka 1492.

Baruch, msomi na aliyekuwa na akili nyingi alisomeshwa kwa kina elimu ya tamaduni za kiyahudi, akisoma shule ya kiyahudi (The Yeshiva) na alitii sikukuu na miiko yote ya dini.

Lakini taratibu alianza kujitenga mbali na imani za mababu zake.

Anasema
"ALTHOUGH I HAVE BEEN EDUCATED FROM BOYHOOD IN THE ACCEPTED BELIEF CONCERNING SCRIPTURE" anaandika kusema "I HAVE FELT BOUND IN THE END TO EMBRACE OTHER VIEWS"

"JAPOKUWA NIMEFUNDISHWA TOKA UTOTONI KATIKA IMANI ILIYOKUBALIKA KULINGANA NA MAANDIKO, MWISHO NIMEONA NIFUATE MITAZAMO MINGINE"

Kwa kina hiyo mitazamo mingine ilionekana kupitia kazi yake kubwa katika kitabu cha "THE ETHICS" kilichokuwa katika lugha ya ki Latin na kuchapishwa mwaka 1677.

Katika kitabu hicho Spinoza anapinga nguzo kuu za Judaism(Dini ya ki Abrahamia) na kuipangilia upya dini kwa mitazamo yake.

Anasema
1. Mungu sio kiumbe au mashine au nguvu fulani iliyopo huko nje ya ulimwengu(nature).
2. Hakuna wa kusikia eti maombi yetu au kututendea miujiza.
3. Hakuna wa kutuadhibu kwa madhambi yetu.
4. Hakuna maisha baada ya kufa.
5. Mwanadamu sio kiumbe kilichochaguliwa na mungu.
6. Bibilia iliandikwa na watu wa kawaida.
7. Mungu sio mjuzi wala architect wala mfalme na wala sio mwenye majeshi eti anayewaita waumini kushika upanga wampiganie.
8. Mungu haoni chochote wala hategemei chochote .
9. Hahukumu wala hana zawadi ya kutoa kwa watenda mema eti baada ya kufa.
" EVERY REPRESENTATION OF GOD AS A PERSON IS A PROJECTION OF THE IMAGINATION, AND EVERYTHING IN THE TRADITIONAL LITURGICAL CALENDAR IS PURE SUPERSTITION AND MUMBO-JUMBO"

Lakini baada ya yote haya, Spinoza hakuwahi kusema yeye ni Atheist, alisisitiza kuwa yeye atabaki kuwa mtetezi kisiki kabisa wa Mungu na Mungu ana nafasi kubwa kabisa kwenye Ethics ya Spinoza. Ila sio Mungu huyu wa kwenye Bibilia.

Mungu wa Spinoza yeye si mbinafsi wakuwajaribu viumbe kwa matatizo na hana tofauti na hivi tunavyoviita Nature au Existence au A World Soul.
"GOD IS UNIVERSE AND IT'S LAWS"
Kwamba Mungu ni ulimwengu mzima na sheria zake.
"GOD IS REASON AND TRUTH"
"GOD IS AN ANIMATING FORCE IN EVERYTHING THAT IS AND CAN BE. HE IS NOT IN TIME AND HE CAN NOT BE INDIVIDUATED"

Kwamba mungu ni sababu ya jambo kutokea na ukweli. Mungu ni nguvu zilizopo kwenye kila kitu kilichopo na kinachoweza kuwepo. Hayupo katika muda na hauwezi kumpoint na kumpwekesha.

Ninaposema nguvu zote namaanisha hizi gravity light heat sound etc hizo ndio mungu kwasababu ndizo zinazoendesha dunia.

Anaandika
"Whatever is, is in God and nothing can exist or be conceived without God"

Katika kitabu chake alikataa zaidi hili wazo la maombi.
Katika maombi, mtu huomba kuwa mungu eti abadilishe jinsi ulimwengu na asili vinavyofanya kazi. Lakini Spinoza anapinga kwa kuwa hii ni njia potofu kabisa kuwahi kutokea.

Kazi ya mwanadamu ni kudadavua na kuelewa ni vipi na ni kwanini ulimwengu unafanya kazi jinsi unavyofanya, na kisha akubali badala ya kukaa na kulalamika juu ya utendaji kazi wa "Nature" na kutuma viji ujumbe juu angani(Maombi) eti ili mungu avisikie halafu abadilishe utendaji wa ulimwengu.

Anasema anayempenda Mungu asikae kusubiri kupendwa na Mungu halafu eti mtu anatoa labda sadaka au anasaidia watu wasiojiweza akitegemea Mungu apindishe sheria za kiasili ili ayaboreshe maisha ya mtu huyu kwa namna fulani.

Spinoza aliifuata falsafa ya Stoics ya wagiriki na waroma wa zamani waliosema kuwa wisdom sio kulalamika juu ya mambo jinsi yalivyo mabaya bali ni kupambana kujifunza uhalisia wa dunia na maisha ulivyo kisha usujudu au ukubali tu kiroho safi juu ya uhalisia wa taabu ambao ni walazima kwa kila mtu.

Kumuelewa Mungu kwa tamaduni zetu ni kwa kusoma vitabu vitakatifu, lakini Spinoza anasema ili umuelewe Mungu inabidi usome na uelewe jinsi ulimwengu unavyofanya kazi
 
Baruch Spinoza ni mwnafalsafa wa karne ya 17 wa Dutch aliyejaribu kuivumbua dini kivingine, kuiondoa kutoka kitu kilichopo kishirikina ,kisicho kisayansi lakini wakati huohuo chenye kupooza nafsi za watu.

"Baruch" neno la ki Hebrew lenye maana ya "Blessed", alizaliwa katika kota za kiyahudi huko Amsterdam mwaka 1632, na alikua kwa mfumo na mawazo yote ya kiyahudi. Mababu zake walihusiana pia na mayahudi na walishiriki katika safari za peninsula ya spain wakati wa kuueneza ukatoliki mwaka 1492.

Baruch, msomi na aliyekuwa na akili nyingi alisomeshwa kwa kina elimu ya tamaduni za kiyahudi, akisoma shule ya kiyahudi (The Yeshiva) na alitii sikukuu na miiko yote ya dini.

Lakini taratibu alianza kujitenga mbali na imani za mababu zake.
Anasema
"ALTHOUGH I HAVE BEEN EDUCATED FROM BOYHOOD IN THE ACCEPTED BELIEF CONCERNING SCRIPTURE" anaandika kusema "I HAVE FELT BOUND IN THE END TO EMBRACE OTHER VIEWS"

"JAPOKUWA NIMEFUNDISHWA TOKA UTOTONI KATIKA IMANI ILIYOKUBALIKA KULINGANA NA MAANDIKO, MWISHO NIMEONA NIFUATE MITAZAMO MINGINE"

Kwa kina hiyo mitazamo mingine ilionekana kupitia kazi yake kubwa katika kitabu cha "THE ETHICS" kilichokuwa katika lugha ya ki Latin na kuchapishwa mwaka 1677.

Katika kitabu hicho Spinoza anapinga nguzo kuu za Judaism(Dini ya ki Abrahamia) na kuipangilia upya dini kwa mitazamo yake.

Anasema
1. Mungu sio kiumbe au mashine au nguvu fulani iliyopo huko nje ya ulimwengu(nature).
2. Hakuna wa kusikia eti maombi yetu au kututendea miujiza.
3. Hakuna wa kutuadhibu kwa madhambi yetu.
4. Hakuna maisha baada ya kufa.
5. Mwanadamu sio kiumbe kilichochaguliwa na mungu.
6. Bibilia iliandikwa na watu wa kawaida.
7. Mungu sio mjuzi wala architect wala mfalme na wala sio mwenye majeshi eti anayewaita waumini kushika upanga wampiganie.
8. Mungu haoni chochote wala hategemei chochote .
9. Hahukumu wala hana zawadi ya kutoa kwa watenda mema eti baada ya kufa.
" EVERY REPRESENTATION OF GOD AS A PERSON IS A PROJECTION OF THE IMAGINATION , AND EVERYTHING IN THE TRADITIONAL LITURGICAL CALENDAR IS PURE SUPERSTITION AND MUMBO-JUMBO"

Lakini baada ya yote haya, Spinoza hakuwahi kusema yeye ni Atheist, alisisitiza kuwa yeye atabaki kuwa mtetezi kisiki kabisa wa Mungu na Mungu ana nafasi kubwa kabisa kwenye Ethics ya Spinoza. Ila sio Mungu huyu wa kwenye Bibilia.

Mungu wa Spinoza yeye si mbinafsi wakuwajaribu viumbe kwa matatizo na hana tofauti na hivi tunavyoviita Nature au Existence au A World Soul.
"GOD IS UNIVERSE AND IT'S LAWS"
Kwamba Mungu ni ulimwengu mzima na sheria zake.
"GOD IS REASON AND TRUTH"
"GOD IS AN ANIMATING FORCE IN EVERYTHING THAT IS AND CAN BE. HE IS NOT IN TIME AND HE CAN NOT BE INDIVIDUATED"

Kwamba mungu ni sababu ya jambo kutokea na ukweli. Mungu ni nguvu zilizopo kwenye kila kitu kilichopo na kinachoweza kuwepo. Hayupo katika muda na hauwezi kumpoint na kumpwekesha.
Ninaposema nguvu zote namaanisha hizi gravity light heat sound etc hizo ndio mungu kwasababu ndizo zinazoendesha dunia.

Anaandika
"Whatever is, is in God and nothing can exist or be conceived without God"

Katika kitabu chake alikataa zaidi hili wazo la maombi.
Katika maombi, mtu huomba kuwa mungu eti abadilishe jinsi ulimwengu na asili vinavyofanya kazi. Lakini Spinoza anapinga kwa kuwa hii ni njia potofu kabisa kuwahi kutokea.

Kazi ya mwanadamu ni kudadavua na kuelewa ni vipi na ni kwanini ulimwengu unafanya kazi jinsi unavyofanya, na kisha akubali badala ya kukaa na kulalamika juu ya utendaji kazi wa "Nature" na kutuma viji ujumbe juu angani(Maombi) eti ili mungu avisikie halafu abadilishe utendaji wa ulimwengu.

Anasema anayempenda Mungu asikae kusubiri kupendwa na Mungu halafu eti mtu anatoa labda sadaka au anasaidia watu wasiojiweza akitegemea Mungu apindishe sheria za kiasili ili ayaboreshe maisha ya mtu huyu kwa namna fulani.

Spinoza aliifuata falsafa ya Stoics ya wagiriki na waroma wa zamani waliosema kuwa wisdom sio kulalamika juu ya mambo jinsi yalivyo mabaya bali ni kupambana kujifunza uhalisia wa dunia na maisha ulivyo kisha usujudu au ukubali tu kiroho safi juu ya uhalisia wa taabu ambao ni walazima kwa kila mtu.

Kumuelewa Mungu kwa tamaduni zetu ni kwa kusoma vitabu vitakatifu, lakini Spinoza anasema ili umuelewe Mungu inabidi usome na uelewe jinsi ulimwengu unavyofanya kazi
Naunga mkono hoja mkuu .Hata Albert Einstein alipoulizwa ana amini Mungu yupi alijibu kwamba "I believe in God of Spinoza"
 
Back
Top Bottom