Fally Ipupa vs Ferre Gola.

Nani mkali?


  • Total voters
    29
Inachanganya sana,sijui ni kwa sababu hawa ni wanafunzi wa mwalimu mmoja? i.e koffi charles anthony olomide.
Fere sio Mwanafunzi wa Koffi, acha matusi. Alijiunga nae kama amesha hit vibaya with Balndine na Vita Imana, from Wenge Musica Maison Mere... aliingia Kwa koffi from his own band (Les Marquis). He is a pair to Koffi (kumbuka Insecticide)
 
EBWANA NIMESHINDWA KUPIGA KURA,MAANA WOTE NAWAKUBALI.
FERRE GOLA KWA ZUKU YUPO VYEMA,HATA KWA UCHEZAJI YUPO VYEMA,JARIBU KUMCHEK TANGU AKIWA NA WERRASON
FALLY NAYE YUPO VYEMA KWENYE NYANZA HIZO NILIZOSEMA NA KWINGINEKO.
KIFUPI NAONA KAMA WANALINGANA KWENYE KILA SEKTA.
kuna awards za mwaka juzi zilifanyika DRC,ferre gola alipata award huku fally akiambulia patupu.
 
siwajui wote.Mkongomani wa mwisho kumjua alikuwa Yondo sista
 
Mh!watu wanachambua bwana!,thanks mr.romantic you are bombastic and fantastic.
 
Last edited by a moderator:
I do acknowledge the importance of understanding lyrics but again music is bigger than this and way complex to settle for artistic evaluations.Kuna wanamuziki wanaimba vitu ambavyo ni vigumu kueleweka na wengine wana-compose ala za muziki tu na bado wanapata mashabiki.
You can listen to different genres in different languages but still you can find taste in every piece of music.
Lets take Fally's- 'Bicarbonate',Lil Wayne's-Amili,John Legend's-Heaven Only Knows,Dystan's-Raz W Ryciu,Marashi ya Pemba-International Orchestra Safari Sound,Bob Marley's-Natural Mystic,Cabo Snoop's-Windeck,Beethoven's-Symphony 9 to name few.
Now ask me if i do understand what they sing in like half of the list....
Again ask me if i enjoy listening to all these...
My replies might sound a bit inexplicable.


As to why some pick Ferre Gola and others pick Fally Ipupa the answer lies in the variation of vibes and rhythms from these two artists and people translate good music out ot these in different ways.
 
Fally ni mtoto mdogo sana kwa FERRE GOLA sema fally ana bahati na pia good management lakini muziki wake hauna message ni sebene tu,ni sawasawa na jb mpiana na werrason,werrason hana message zaidi ni sebene jb ana message na pia anapiga sana congo rhumba muziki unaopendwa na wacongoman walio wengi.

Tatizo muziki wa congo kutoka ni ngumu sana yani kukubalika,ndio mana watu wanamsifu fally ipupa kwa kuwa amewezza kutoka na kwenda sambamba na kaka zake kina koffi,jb na werra ambayo ndio majina makubwa congo,ferre nae pia hayuko vibaya kazi anapata za kutosha tu. Kuna vipaji vingi ambavyo vilikua na majina makubwa kwenye bendi kabla ya kina fally lakini vimeshindwa kusimama licha ya kujaribu,mfano suzuki 4x4 ni mtu mwenye kipaji cha hali ya juu na aliibeba sana Quartier latin huko nyuma kipindi fally bado mtoto lakini alijaribu kuachana na koffi kusimmama mwenyewe kachemsha akarudi kwa koffi,pia watu kama alain mpela,aimelia,tutu kaludji,bileku mpasi,blaize bula,adolphe dominguez na kadhalika bado wanasota wakati wadogo zao hawa kina fally na ferre wameweza,yupo mwingine anaitwa KABOSE alikua kwa defao zamani badae kwa bozi boziana sasa hivi ana bendi yake pia anajitahidi kufanya vizuri ndani ya congo lakini hajamudu kuvuka mipaka ila anakuja vizuri.

Ferre Gola alianzia huku kipibdi hiki sijui fally alikua kijijini kwa may be.Hapa anaimba sauti ya JB MPIANA ambae hakuwepo siku hiyo

 
Last edited by a moderator:
Done for you mkuu...
Lazima watu watampenda Fally coz ndio wanamjua, na pia hawaelewi lyrics zao, so game yote inaishia kwenye kuakta kiuno tu, wala sio artistic evaluation.

Yani napata Faraja kuona ninachokipenda wapo wanachokipenda na ulichiksema hapo mkuu ndio ukweli wenyewe.............Kwa mauno Fally ni mzuri tu sasa tukizungumzia mziki basi Ferre ni mwanamuziki
 
Twende mbele turudi nyuma haitakuja kutokea kama wenge musica ile ya ukweli yenyewe ikiwa kamili..

 
Last edited by a moderator:
HAPA JB MPIANA HAPA WERRASON PALE BLAIZE BULA HUKU ADOLPHE DOMINGUEZ,PEMBENI TUTU CALUDJI...HII NDANI YA PARIS PAMOJA NA PAPA WEMBA.

 
Last edited by a moderator:
wote ni wanamuziki wazuri lakini kwa mtazamo wangu mimi,Fally ni zaidi as yuko more dynamic.anaweza ku-fit kwingi mno na kufanya muziki wa aina tofauti tofauti na pia kuuchanganya na kupata kitu kizuri tu bado!so, kwa hilo,fally has got an edge over chetani gorra!
 
Kusema ukweli wote wapo juu sema tu itategemea unawaangalia na kuwa hukumu kutoa kona gani.
kwa mtazamo wangu Fally yupo vizuri zaidi kwenye nyanja nyingi zaidi kuliko Ferre Gola
Ferre Gola anapiga muziki wa asili zaidi wa kikongo na anawashabiki wengi zaidi wa kongo tofauti ya Fally ipupa ambaye amelenga zaidi na soko la nje zaidi ya congo na paris
Fally anafit sehemu nyingi, yupo flexble na amepiga makolabo ya kufa mtu na wasanii kibao walio muweka zaidi kimataifa zaidi ya Gola
Kwa sauti Fally bado anaaminika ni mmoja wa wacongo wenye sauti tamu mno lakini linapokuja swala la tungo za mantiki Gola anatunga nyimbo zenye ujumbe zaidi ya Fally ipupa
Kwenye kucheza Bado Fally ipupa yupo juu zaidi ya Gola ingawa na yeye yumo
Kwa upande wa proffesional Fally yupo juu, ana management ya uhakika kuendesha muziki wake kisasa na kimataifa zaidi compare to Gola
Lakini ndani ya Congo yenyewe Gola anakubalika zaidi ya fally ipupa wakiamini anapiga muziki halisi wa kwao
So kama utahukumu kwa ukongwe basi utampa Ferre Gola
 
Kwa wale wenzangu wapenzi wa miziki ya lingala,naomba view zenu.Mimi binafsi ninawakubali sana hawa wasanii wote wawili kiasi ninashindwa kuamua yupi zaidi.Naomba mtazamo wako,nani mkali zaidi kati ya Fally na Ferre.

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…