Fake goods, tunawasafishia mazingira yao!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fake goods, tunawasafishia mazingira yao!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Jul 1, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Ingawaje ninamiliki chumba kimoja bila sebule huku nikiwa na vifaa vichache kabisa vya umeme, lakini tayari chumbani kwangu kuna EXTENSION CABLES mbili ambazo ni mbovu!! Je, wewe ndani kwako zipo ngapi hata kama ni zile ulizotupa jalalani ndani ya mwaka mmoja uliopita? Umeshawahi kujiuliza nchini China peke yake kuna extension cables ngapi ambazo ni mbovu?Umeshwahi kujiuliza nchi hii yenye watu zaidi ya bilioni moja kuna TV na Computer Monitors ngapi ambazo ni mbovu zinazotafuta disposing venue? Hiyo ni intro, tuje kwenye mada yenyewe!!! Nazani wengi wetu tunaikubali theory inayosema kwamba the most risky business ndizo zenye higher return! Kwa hapa tulipofikia ndani ya TZ, inatosha kabisa kuita biashara ya bidhaaa bandia ni among the risky business in country! Tumeshuhudia mara kwa mara bidhaa hizi zikipigwa moto kwenye madampo yetu!! Na kwavile hii sasa ishakuwa risky business ambayo mtu ukifanikiwa kuuingiza sokoni utatengeneza pesa ya kutosha basi sina shaka kwamba bidhaa bandia zitaendelea kuingia nchini mwetu! Kama hivyo ndivyo, tutarajie bidhaa hizi kuendelea kuteketezwa kwa moto kila wakati nchini mwetu. Swali langu ni kwamba, is it best practice kwa mazingira yetu? Nyingi ya bidhaa hizi ni plastic materials ambazo hata ukizichoma hazipotei katika sura ya dunia kama ambavyo zingepotea mbao na karatasi zinapochomwa. Hakika bidhaa hizi zinapokamatwa na kuchomwa moto, inaonekana ni kama tumeshawakoma tayari!!! Ni kweli kwa kiasi Fulani, but what about mazingira yetu?! Hakuna asiyejua kwamba kila nchi hivi sasa (industrialized countries) ina shida ni wapi ika-dispose waste materials zake. Sasa hofu yangu ni kwamba, hata kama hawajagundua opportunity hii, kesho na kesho kutwa watagundua kwamba kinachotokea Tanzania hivi sasa ni njia nzuri ya ku-dispose waste materials zao. Look this way, wachina huko kwao wana-collect TV zote ambazo ni mbovu, wanarekebisha kidogo mfumo wa umeme huko ndani ili angalau iweze kuwaka! Lile ganda la nje linasafishwa kitaalamu kabisa then una-export to Tanzania!! Tume ya biashara huru wakizikamata, wanazi-consider kama FAKE GOODS na wao wanazipiga moto, biashara imeisha, TUMESHAMKOMOA ALIYEZILETA!!! Je, hatuoni kuna ulazima wa kubadili aina hii ya kuteketeza bidhaa feki kwavile zinaweza zikaleta uharibifu mkubwa wa mazingira huko mbeleni? IS IT BEST PRACTICE? Mimi sio mtaalamu, kwa wanaofahamu kwani badala yake bidhaa hizi haziwezi kuwa recycled badala ya kuzichoma moto? Kama haiwezekani, kwanini hao wanaokamatwa nazo wasilazimishwe kuzirudisha walikozitoa, ikibidi UNDER ESCOURT? Since itÂ’s risky business, then zitakuwa na high return! Since zinatoa high return, watu wataendelea kuzileta na mazingira yetu kuendelea kuharibika kwavile bidhaa za plastic hata ukizichoma ni kazi bure!!!
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kuna methali moja inasema, ganda la mua la jana chungu kaona kivuno,tulipofika ni pabaya sana,wauza viatu vya mitumba wanasema vinalipa,nguo za mitumba zinalipa,ma-TV used yanalipa,magari used yanalipa,ukienda duka fulani pale kamata kuna kuku wa kutoka kwa madiba,sasa sijui nani anajua walichinjwa lini,orodha ni ndefu sana. Tutaendelea kusafisha kwa wenzetu na kuchafua kwetu mpaka tutakapojitambua.
   
Loading...